X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 07/Nov 04:34

PINDA ASHIRIKI MAZISHI KUMUAGA JAJI KIPENKA

 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Geophrey Mizengo Pinda ameshiriki mazishi ya kuuanga Mwili wa  marehemu Jaji Kipenka Msemembo Mussa ambaye alikuwa Jaji Msataafu wa Mahakama kuu ya Tanzania na aliyewahi kushika Nyadhifa mbalimbali Serikalini enzi za Uhai wake ikiwemo Katibu Wa Bunge.Hafla ya Mazishi yamefanyika leo Tarehe 06 November 2024 katika Kijiji cha Kinampanda Kilichopo katika wilaya ya Iramba Mkoani SingidaMhe. Pinda ameshiriki Mazishi hayo akimwakilisha Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye ameeleza kwa masikitiko juu ya kuondokewa na Marehemu. Jaji Kipenka Msemembo Mussa.Mazishi hayo yametanguliwa na Ibada ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Wilayani Kinampanda na kuongozwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kati, Dk. Cyprian HilintiAkitoa salamu za rambirambi, Naibu Waziri Pinda amesema kuwa Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba pamoja na Serikali nzima wanaungana na familia katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.Mhe. Pinda amesema marehemu Jaji Kipenka  alikuwa kiungo muhimu cha Maendeleo kwa Wananchi wa Kinampanda enzi za uhai wake alikuwa akishirikiana vema na Dkt Mwigulu katika Shughuli mbalimbali za Maendeleo."Nimesimama hapa kwa niaba ya mhe. Mwigulu ambaye anatoa pole nyingi sana kwa familia na ameindokewa kwa maelezo yake na mtu muhimu ambaye kilikuwa Kiungo cha Maendeleo cha Kinampanda". Amesema Mhe PindaAidha Mhe. Pinda ametoa wito kwa familia ya Jaji Kipenka hasa watoto wa marehemu kuacha kugombania mali zilizokuwa zinamilikiwa na Marehemu Jaji Kipenka kwani Kifanya hivyo kutawaingiza matatizoni zaidi."Kikubwa kwenye familia mtulie wakati wa pito hilo katika kukusanya mali za marehemu", Amesema Mhe Pinda"Nimeona baba ana watoto wanne lakini watoto kokote waliko wasisahau Mwenza wa Marehemu Jaji Kipenka yupo hai". Amesema Mhe PindaMarehemu Jaji Kipenka Msemembo Mussa alizaliwa tarehe 28, Desemba 1954 ambapo aliugua kwa muda kabla ya kufariki tarehe 2 November 2024.Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

Articles similaires

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MAZISHI YA BABA MZAZI WA TUTUBA

msumbanews.co.tz - 06/Nov 13:45

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 06 Novemba 2024 ameshiriki mazishi ya marehemu John Tutuba ambaye...

CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WA UMMA ZITATULIWE ILI KUKUZA SEKTA YA UMMA KIUCHUMI NA KIJAMII

msumbanews.co.tz - 05/Nov 09:20

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa neno la utangulizi kabla ya...

MAMENEJA RASILIMALIWATU KATIKA SEKTA YA UMMA AFRIKA WAMUUNGA MKONO RAIS DKT. SAMIA KUTANGAZA SEKTA YA UTALII WA TANZANIA

msumbanews.co.tz - 08/Nov 09:31

Rais wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na...

PINDA AMALIZA MGOGORO WA ARDHI DODOMA

msumbanews.co.tz - 01/Nov 18:00

 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amemaliza mgogoro wa Ardhi wa Familia ya Bw. Emmanuel Corneli Mbunda na Mzee...

CCM WAHIMIZWA KUHAMASISHA WATANZANIA KUENDELEZA UMOJA NA MSHIKAMANO

msumbanews.co.tz - 11/Nov 06:19

 Na Gideon Gregory, Dodoma.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA ILI KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO YA WANANCHI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:02

 Na. Joseph Mahumi, WF, MorogoroSerikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo...

PICHA 10 : MAKAMU WA RAIS AKIONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA MAENDELEO YA JAMII YA BARAZA LA MAWAZIRI

msumbanews.co.tz - 04/Nov 11:30

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiongoza Kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Jamii ya Baraza la Mawaziri...

BASHUNGWA AONGOZA HARAMBEE JIMBO KATOLIKI BUNDA, MILIONI 272.6 ZAKUSANYWA

msumbanews.co.tz - 12/Nov 07:33

 Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameshiriki Misa Takatifu katika Parokia ya Mtakatifu Paulo na kuongoza harambee ya kumalizia ujenzi wa jengo la...

WAJASIRIAMALI WA NCHI WANACHAMA EAC WAHAMASISHWA KUWA WABUNIFU

msumbanews.co.tz - 05/Nov 18:44

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulrmavu, Zuhura Yunus akizungumza wakati hafla ya Siku ya Tanzania iliyofanyika...

WAZIRI KIJAJI AOMBA WWF ISAIDIE KULINDA MAZINGIRA

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:28

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameliomba Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément