X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 12/Nov 07:33

BASHUNGWA AONGOZA HARAMBEE JIMBO KATOLIKI BUNDA, MILIONI 272.6 ZAKUSANYWA

 Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameshiriki Misa Takatifu katika Parokia ya Mtakatifu Paulo na kuongoza harambee ya kumalizia ujenzi wa jengo la ofisi za Jimbo Katoliki la Bunda ambapo jumla ya Shilingi Milioni 272.6 imekusanywa. Harambee hiyo imefanyika leo Novemba 10, 2024 Wilayani Bunda Mkoani Mara ambapo pamoja na mambo mengine, Waziri Bashungwa amezindua ofisi ya Askofu wa Jimbo Katoliki la Bunda, Mhashamu Simon Chibuga Msondole ambayo itaanza kutoa huduma za kijamii na kiroho. “Jimbo letu la Bunda ni changa lina miaka 13, tunahitaji kubadilisha sura ya Jimbo letu, ili itakapofika Jubilei ya miaka 25, Jimbo liwe limepiga hatua kubwa na lenye kupendeza, lenye miundombinu mbalimbali kwa ajili ya huduma kwa watu wa Mungu na nchi yetu”, amesema Bashungwa Bashungwa amelishukuru Kanisa Katoliki nchini kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika shughuli za ustawi na maendeleo ya jamii katika Sekta ya Elimu, Afya, na Sekta za uzalishaji hususani kilimo, uwekezaji katika viwanda, Hoteli pamoja na bima za aina mbalimbali. Aidha, Bashungwa amemshukuru na kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha miundombinu ya barabara, madaraja, mizani, vivuko na Kiwanja cha Ndege katika Mkoa wa Mara ambapo amebainisha baadhi ya miradi iliyokamilika, inayoendelea kutekelezwa na ambayo ipo katika hatua za upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Akitaja miradi hiyo, Amesema ujenzi wa barabara ya Nyamuswa – Bulamba (km 56.4) umekamilika kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Shilingi Bilioni 67.8 na kukamilika kwa ujenzi mzani wa kupima magari yakiwa kwenye mwendo (Weigh in Motion) katika eneo la Rubana kwa Shilingi Bilioni 22.2 Bashungwa amebainisha miradi mingine ni ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Sanzate - Nata (km 40) kwa gharama ya Shilingi Bilioni 51.08 ambao umefikia asilimia 55, ujenzi wa barabara ya Mogabiri - Nyamongo (km 25) kwa gharama ya shilingi Bilioni 34.6 na ujenzi umefikia asilimia 52. Kadhalika, Bashungwa ameongeza kuwa Serikali inaendelea na ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege Musoma kwa Shilingi Bilioni 35.048 na utekelezaji wake umefikia asilimia 57. Kwa upande wake, Askofu wa Jimbo Katoliki la Bunda, Mhashamu Simon Chibuga Msondole amewashukuru viongozi wote wa Serikali, vyama vya kitume, waumini wa Parokia hiyo, marafiki na jamaa kwa majitoleo yao katika kufanikisha ujenzi wa ofisi za Parokia ya Bunda. Naye, Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Chacha Maboto ametoa rai kwa uongozi wa Jimbo Katoliki la Bunda kuhakikisha wanasimamia kikamilifu michango yote iliyotolewa katika harambee hiyo ili ziweze kutimiza malengo yaliyokusudiwa. Akisoma Risala, Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee Jimbo la Bunda, Kulwa Kahabi amesema kuwa harambee hiyo imehusisha waumini wa Parokia 23, vyama vya kitume, watu binafsi na kufafanua harambee hiyo imekusanywa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza mwaka 2022 na walikusanya Milioni 240, awamu ya pili mwaka 2023 walikusanya Milioni 130 na katika mwaka 2024 matarajio yao ni kukusanya Milioni 350.

Articles similaires

RAIS SAMIA AIPA TANROADS ZAIDI YA BIL 500 UJENZI MIUNDOMBINU DAR ES SALAAM

msumbanews.co.tz - 10/Nov 08:34

Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan zaidi ya Shilingi Bilioni 500...

UJENZI WA BARABARA NA MADARAJA BABATI KUFUNGUA UTALII

msumbanews.co.tz - 12/Nov 12:59

 Na. Catherine Sungura, BabatiImeelezwa kwamba ujenzi na matengenezo ya barabara na madaraja unaofanywa na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini...

CCM WAHIMIZWA KUHAMASISHA WATANZANIA KUENDELEZA UMOJA NA MSHIKAMANO

msumbanews.co.tz - 11/Nov 06:19

 Na Gideon Gregory, Dodoma.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...

REA YATOA KIPAUMBELE UJENZI MIRADI YA NISHATI JADIDIFU

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:22

 Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa kipaumbele kwenye ujenzi wa miradi ya nishati jadidifu nchini ili kusaidia utunzaji wa mazingira, kuzalisha...

MRADI WA TACTIC KIGOMA UJIJI KUKUZA PATO LA WAFANYABIASHARA NA WAVUVI WA MKOA WA KIGOMA.

msumbanews.co.tz - 02/Nov 15:59

 Jumla ya Shilingi Bilioni 16 na Milioni 495 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi na Maboresho makubwa ya Masoko ya Kimkakati Kata ya Mwanga na Soko...

REA KUPELEKA UMEME VISIWA VYOTE TANZANIA BARA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:27

 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...

ZAIDI YA WANANCHI 32,000 WA VIJIJI VYA WILAYA ZA MOROGORO NA MVOMERO KUANZA KUPATA MAWASILIANO

msumbanews.co.tz - 04/Nov 18:47

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi MaryPrisca Mahundi (Mb), amesema Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia...

BUNGE LARIDHIKA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MISITU NA NYUKI

msumbanews.co.tz - 12/Nov 12:47

 Na John MapepeleKamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili  na Utalii imeridhika na miradi mbalimbali  ya misitu na nyuki  inayotekelezwa  na...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBU YA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA.

msumbanews.co.tz - 04/Nov 11:16

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali imeendelea kuboresha miundombu ya kutolea...

SERIKALI YAFIKIA ASILIMIA 85 KATIKA UPATIKANAJI WA DAWA

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:32

 Na : Jusline Marco;ArushaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu upatikanaji wa...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément