Na Happiness Shayo- ArushaWaziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa...
Vous n'êtes pas connecté
Na John MapepeleKamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeridhika na miradi mbalimbali ya misitu na nyuki inayotekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mfuko wa Misitu na Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Tabora (BTI) na kupongeza kwa kazi nzuri inayofanyika.Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Timotheo Mnzava (Mb) ametoa pongezi hizo leo katika siku yake ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Tabora wakati ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya sekta ya misitu na nyuki huku akitaka juhudi hizo ziongeze ili kukamilisha kabisa kazi zilizobaki kwa baadhi ya miradi.Kamati imefika jana ambapo inaendelea kesho kwa mkoa wa Tabora na Singida imeambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dustan Kitandula (Mb), Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi na baadhi ya Watendaji wa Wizara na taasisi zilizo chini ya Wizara.Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Mheshimiwa Deusdedith Katwale pia ameipongeza na kuishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuleta ubunifu na wa kuanzisha nembo (trade mark) maalum inayotambulisha asali kimataifa.“Napenda kuishukuru na kuipongeza Wizara ya Maliasili na utalii kwa mapinduzi makubwa kwenye sekta hii kwa kuanzisha nembo ya asali yetu ambayo itasaidia kuitambulisha asali ya Tanzania kwenye masoko ya kimataifa hivyo kuuza asali kwenye masoko ya kimataifa tofauti na awali.” Amefafanua Mhe. KatwaleKatika miradi hiyo Mfuko wa Misitu Tanzania umetoa ruzuku kwa miradi 56 katika Mkoa wa Tabora pekee yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 2.2 Miradi hiyo inatekelezwa katika Wilaya zote 7 za Mkoa wa Tabora ambazo ni Tabora, Uyui, Nzega, Igunga, Sikonge, Urambo na Kaliua. Aidha, kati ya miradi hiyo ipo miradi ya ufugaji nyuki inayotekelezwa zaidi na vikundi vya kijamii, viwanda vya mazao ya nyuki na miradi ya kuimarisha Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji nyuki Tabora (BTI). Pia Mfuko unagharamia ujenzi wa kiwanda na ununuzi wa mitambo kwa ajili mafunzo ya kuchakata na kufungasha mazao ya nyuki katika Chuo cha BTI kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi. Kamati, pia imepata bahati ya kutembelea na kujionea mradi wa ukarabati wa jengo la utawala la Chuo, ujenzi wa jengo la karakana ya mbao kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa mafunzo ya utengenezaji wa mizinga bora ya nyuki, ujenzi wa jengo la ukumbi wa mihadhara (lecture theatre) kwa matumizi wanafunzi wa BTI na Kituo cha ufugaji nyuki kibiashara kilianzishwa kama mkakati wa kuongeza kipato cha jamii kwa uboreshaji wa uchumi na kupunguza uharibifu wa misitu ya hifadhi katika Mkoa wa Tabora.
Na Happiness Shayo- ArushaWaziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa...
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema kukamilika kwa Miradi ya TACTIC mkoani...
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameshiriki Misa Takatifu katika Parokia ya Mtakatifu Paulo na kuongoza harambee ya kumalizia ujenzi wa jengo la...
Na. Joseph Mahumi, WF, MorogoroSerikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo...
Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan zaidi ya Shilingi Bilioni 500...
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema ujenzi wa Soko la Kisasa la Mwanga na Soko la...
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...
Na Gideon Gregory, Dodoma.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...
Na : Jusline Marco : ArushaWaziri wa nchi,ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawane amesema serikali ya...
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2024) amefanya ziara jijini Dodoma ili kukagua utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi...