Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan zaidi ya Shilingi Bilioni 500...
Vous n'êtes pas connecté
Na. Catherine Sungura, BabatiImeelezwa kwamba ujenzi na matengenezo ya barabara na madaraja unaofanywa na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wilayani Babati unaenda kufungua shughuli za utalii.Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuella Kaganda ameeleza hayo alipofanya mahojiano na waandishi wa habari ofisini kwake wilayani humo, Mkoani Manyara hivi karibuni.Mhe. Kaganda amesema kufunguka kwa mtandao wa barabara kumeweza kuvutia watalii katika mbuga za Taifa za Tarangire na Manyara, utalii wa kitamaduni, Ziwa Manyara pamoja na milima ambayo wananchi hufanya shughuli za kitalii.“Babati inaenda kufunguka kwani mtandao wa barabara unaendelea kuongezeka kwa kuwa na Kilomita 1,548.792 ambapo Mji wa Babati una Km. 595.102 na Halmashauri ya Babati Km. 953.69”, Alisema na kuendelea,“Hakika kazi kubwa inafanyika na Serikali ya Awamu ya Sita kwani Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kutupatia pesa za kuwekeza kwenye miundombinu.” Alisisitiza.Ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2024/2025 TARURA wilaya ya Babati imepanga kutumia zaidi ya shilingi bilioni 4.9 kwaajili ya kuchonga barabara, kutengeneza barabara za changarawe, kujenga madaraja na Papu Kalavati.Aidha, amesema katika kipindi cha miaka mitatu wamepokea jumla ya shilingi bilioni 12 kwaajili ya kuimarisha mtandao wa barabara ambapo awali TARURA walikuwa wakipokea bilioni 1 hivyo ongezeko la bilioni 3.5 ni ongezeko kubwa katika wilaya hiyo.“Ongezeko hili sio kidogo na tumeona namna Mhe. Rais alivyoamua kuibadilisha Babati yetu.” Aliongeza kusema.Hata hivyo Mhe. Kaganda alisema katika matengenezo hayo wanatarajia kufunga taa zipatazo 90 katika barabara ya kuelekea hospitali ya wilaya ya Mrara ili kulinda usalama wa wananchi wakati wakielekea kupata huduma nyakati za usiku.Hivyo ametoa rai kwa wananchi wa wilaya hiyo kuitunza miundombinu inayojengwa na Serikali na kuepuka kufanya shughuli za kilimo kandokando ya barabara na kupitisha majembe yanayokokotwa na wanyama ili kuepuka mmomonyoko wa ardhi.Pia aliwataka wananchi kusafisha mitaro iliyopo mbele za nyumba zao, kutokutupa taka hovyo na hivyo kutunza mitaro ya maji hususani kipindi hiki cha mvua ili kuepuka mafuriko na magonjwa mbalimbali yanayotokana na uchafu.Naye, Bw. Hamis Rajabu Mkazi wa Mtaa wa Mrara amesema madaraja waliyojengewa katika barabara hiyo ambayo ni kiunganishi kati ya Babati Mjini na Vijijini yameweza kuwaondolea kero mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili hususan kipindi cha masika ambapo magari na vyombo vingine vya moto vilikuwa vikipita kwa kupokezekana.
Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan zaidi ya Shilingi Bilioni 500...
Na Gideon Gregory, Dodoma.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa kipaumbele kwenye ujenzi wa miradi ya nishati jadidifu nchini ili kusaidia utunzaji wa mazingira, kuzalisha...
Geita,Tanzania Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita limekutana kujadili na kupitisha mpango wa wajibu wa Kampuni ya Mgodi wa Dhahabu...
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Geophrey Mizengo Pinda ameshiriki mazishi ya kuuanga Mwili wa marehemu Jaji Kipenka...
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameshiriki Misa Takatifu katika Parokia ya Mtakatifu Paulo na kuongoza harambee ya kumalizia ujenzi wa jengo la...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa neno la utangulizi kabla ya...
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...
Imeelezwa kuwa, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umepeleka umeme kwa wananchi wapatao 2,400 wa vijiji nane (8) vya Tarafa ya Lupembe, Wilaya ya...
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba, amewahimiza wananchi wa wilaya hiyo kujikita zaidi katika lishe bora na kuachana na tabia ya ulaji usiofaa...