Na Gideon Gregory, Dodoma.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...
Vous n'êtes pas connecté
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amemaliza mgogoro wa Ardhi wa Familia ya Bw. Emmanuel Corneli Mbunda na Mzee Broma Michael Mtega.Mhe. Pinda amemaliza mgogoro huo tarehe 31 Oktoba 2024 katika ofisi yake iliyopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma, kwa kufanya kikao na pande zote mbili zenye mgogoro na kisha kufikia maridhiano.Mgogoro huo unahusisha kiwanja Namba 109 na 110 vilivyopo katika Kitalu D eneo la Swaswa Ng'ambo Jijini Dodoma ambapo Msingi wa Mgogoro huo ni Bwn. Emmanuel Cornery Mbunda Mwenye Kiwanja 109 kujenga ukuta kwenye eneo la Bw. Broma Michael Mtega mwenye kiwanja Namba 110.Mara baada ya kusikiliza pande zote kwa kuchambua nyaraka za wamiliki hao, Mhe Pinda alibaini kuwa Bw Emmanuel Mbunda aliuziwa eneo la mita za mraba 650, hata hivyo eno ambalo amelitumia kujenga ukuta lina ukubwa wa mita za mraba 986 ikiwa ni zaidi ya eneo lake kwa mujibu wa nyaraka ikiwemo ramani inayoonesha Kiwanja Na.109 kina Ukubwa wa mita za mraba 467 na kiwanja Na. 110 kina ukubwa wa mita za mraba 519.Pande zote katika mgogoro huo zimeridhia kwa kauli moja kwa kusaini mbele ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ardhi kwa kufanya marekebisho ya mipaka kwa kuhusisha wataalamu wa ardhi ili kumaliza mgogoro huo ambapo Mhe. Pinda ameelekeza marekebisho hayo yafanyike Kuanzia tarehe 01/11/2024.
Na Gideon Gregory, Dodoma.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kimeelezwa kuwa ni moja ya muhimili muhimu katika kufanikisha agenda ya Rais Samia Suluhu Hassan...
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Geophrey Mizengo Pinda ameshiriki mazishi ya kuuanga Mwili wa marehemu Jaji Kipenka...
Na. Lusungu Helela Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu amesema Mamlaka ya Serikali...
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amekabidhi kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege kiwanja cha kisasa cha michezo ya...
Na. Joseph Mahumi, WF, Dar es SalaamTanzania imeishukuru Umoja wa Ulaya (EU) kwa kuendelea kuwa miongoni mwa washirika wakubwa wa kimkakati wa...
Na. Joseph Mahumi, WF, Dar es SalaamTanzania imeishukuru Umoja wa Ulaya (EU) kwa kuendelea kuwa miongoni mwa washirika wakubwa wa kimkakati wa...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa neno la utangulizi kabla ya...
Na, Elizabeth Paulo; Dodoma Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mh. Halima Okash ametoa Rai kwa Viongozi wa Halmashauri kusimamia sheria,...
Na. Peter Haule na Josephine Majura, WF, Dodoma Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), ameitaka Akiba Commercial Bank Plc (ACB)...