X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - Hier 05:32

TTCL YAUNGANISHA WILAYA 106 KWENYE MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO

Mkurugenzi wa Ufundi na Undelezaji kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL,Mhandisi Cecil Francis ameeleza kuwa wamefanikiwa kuunganisha wilaya 106 katika mkongo wa Taifa wa Mawasiliano  Tanzania Bara kati ya Wilaya 139.Hayo yamejiri katika ufunguzi wa kongamano la Connect2Connect lililofunguliwa na Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Jerry Silaa,na limewakutanisha wadau wa mawasiliano wa ndani na nje ya nchi.Amesema kuwa wilaya 33 ambazo bado hazijafikiwa na mkongo wa taifa wa mawasiliano,mwaka huu wa fedha wa 2024/2025,serikali imeshatenga bajeti ya kwenda kukamilisha shughuli hiyo,ili kuhakikisha wilaya zote zinaunganishwa na zianze kupata huduma bora.Alisema mkongo wa mawasiliano wa taifa ni kiungo kikuu cha mawasiliano ya sauti na Intaneti ambapo inaunganishwa na mikongo ya baharini ambayo inaleta Intaneti nchini.“Mkongo wetu wa taifa wa mawasiliano ni kiungo kikuu cha mawasiliano ya sauti,lakini vilevile na Intaneti na tunaunganisha na mikongo ya baharini ambayo inatuletea Intaneti hapa nchini na sisi pia tunaunganisha na nchi za jirani za Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi,Zambia na Malawi.“Tunamaunganisho yamekwenda mpaka Msumbiji na tumeanza kuingia maunganisho yatakayofanya tuingie hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),kupitia Ziwa Tanganyika.alisema Mkurugenzi huyo wa Ufundi”Pia alisema shirika hilo,linaendelea kuboresha maunganisho ya mkongo kwa kusogeza kwenye vituo vya baharini vilivyoko Mombasa nchini Kenya.“Kazi kubwa tuliyonayo TTCL,ni kuhakikisha tunatoa mchango wa mawasiliano kwa mkongo tunayojenga inafika kila sehemu ikiwa na ubora wa hali ya juu kwa ajili ya kufikisha huduma kwa wananchi na kupunguza gharama za matumizi,”alisema.Alisema shirika hilo,kupitia mkongo wa taifa wa mawasiliano wamefanya kazi ya kuunganishwa kwa mawasiliano mikoa kwa mikoa na wilaya kwa wialaya.“Sisi TTCL,tukiwa kama chombo cha serikali tumepewa dhamana ya kutoa huduma za mawasiliano hapa nchini,”alisema.  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Helios towers,Gwakisa Stadi,alisema kampuni hiyo kwa hapa nchini inasimamia minara zaidi ya 400 na wana wateja zaidi ya 10000 ambao ni watumiaji wa minara hiyo.Alisema kazi kubwa ya mirana hiyo,ni kuunganisha huduma za mawasiliano na wateja wao wakubwa ni makampuni ya simu,kampuni za usambazaji wa Inteneti na televisheni zilizoweka vifaa vyao vya mawasiliano kwenye minara hiyo.

Articles similaires

AIRTEL TANZANIA YAENDELEA KUPANUA WIGO VIJIJINI

msumbanews.co.tz - 06:15

Kampuni ya simu za mkononi Airtel kupitia kwa Mkurugenzi wa Biashara Joseph Muhele amesema kuwa mtandao huo mwaka huu 2024 unaendelea kufangua...

KIPAUMBELE CHA SERIKALI NI KUONA IDADI YA WATUMIAJI WA DATA WANAONGEZEKA- MHANDISI MARYPRISCA

msumbanews.co.tz - 10/Sep 04:10

 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa...

KAMATI ZA MAAFA WILAYA ZATAKIWA KUWEKA MIPANGO YA DHARURA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 08:04

Serikali imezitaka Kamati za Usimamizi wa Maafa Ngazi ya Wilaya kuhakikisha zinajiandaa kikamilifu na kuweka mpango wa dharula wa utendaji na uratibu...

KAMATI ZA MAAFA WILAYA ZATAKIWA KUWEKA MIPANGO YA DHARURA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 08:04

Serikali imezitaka Kamati za Usimamizi wa Maafa Ngazi ya Wilaya kuhakikisha zinajiandaa kikamilifu na kuweka mpango wa dharula wa utendaji na uratibu...

TANAPA yaanza na mkakati wa kuboresha barabara zilizopo Hifadhi za Taifa hususani barabara ya Serengeti

msumbanews.co.tz - 05/Sep 06:02

 WADAU wa Utalii katika Hifadhi ya Taifa Serengeti wameiomba Serikali kupatia suluhisho la kudumu la ujenzi wa barabara katika Hifadhi za Taifa...

WAZIRI MAVUNDE AYATAKA MAKAMPUNI YA MAKAA YA MAWE KUWEKEZA KATIKA UZALISHAJI WA UMEME

msumbanews.co.tz - 17/Sep 05:17

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde amezipongeza Kampuni za uzalishaji wa makaa ya mawe kwa kuongeza uzalishaji na kuzitaka kuelekeza zaidi...

TANZANIA YAWEKEZA KIMKAKATI KATIKA SEKTA YA TEHAMA ILI KUKUZA UCHUMI WA KIDIJITALI

msumbanews.co.tz - 08:01

Tanzania ina mifumo kadhaa ya kisheria na udhibiti inayoongoza sekta ya mawasiliano na TEHAMA ili kuhakikisha huduma ya intaneti ya kasi inawafikia...

WAZIRI MAHUNDI AITAKA UCSAF KUTANGAZA SHUGHULI KUPITIA VYOMBO VYA HABARI

msumbanews.co.tz - 11/Sep 05:11

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), amewataka viongozi wa Mfuko wa Mawasiliano...

SERIKALI NA SHIRIKA LA IFAD KUIMARISHA MIFUMO YA UPATIKANAJI WA CHAKULA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 05:30

 Na. Peter Haule na Chedaiwe Msuya, WF, Dodoma Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na...

BILLIONI 3.9 KUIMARISHA MIUNDOMBINU HIFADHI YA TAIFA IBANDA-KYERWA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 05:32

 Na.Edmund Salaho - Kyerwa KageraSerikali imetoa kiasi cha Tsh. Billioni 3.9 kwa ajili ya kuimarisha miundombinu katika Hifadhi ya Taifa Ibanda -...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément