X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 13/Sep 05:32

BILLIONI 3.9 KUIMARISHA MIUNDOMBINU HIFADHI YA TAIFA IBANDA-KYERWA

 Na.Edmund Salaho - Kyerwa KageraSerikali imetoa kiasi cha Tsh. Billioni 3.9 kwa ajili ya kuimarisha miundombinu katika Hifadhi ya Taifa Ibanda - Kyerwa iliyoko mkoani, Kagera.Akikagua miradi ya ujenzi wa miundombinu hiyo Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Musa Juma Kuji alisema Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imetupa upendeleo wa kutupatia fedha za kujenga lango la kuingilia watalii (Complex gate), pamoja na Nyumba za kisasa za Watumishi eneo la Kifurusa hii yote kuhakikisha tunapata mazingira mazuri ya kufanyia kazi zetu.“Hili ni deni ambalo Mhe.Rais wetu ametupa sisi TANAPA na hususani watumishi wa Hifadhi hii na tutamlipa kwa kuchapa kazi na kujituma zaidi katika kulinda na kutunza Rasilimali hizi kwa faida ya kizazi cha sasa na kile cha baadae” alisema Kamishna Kuji.Naye, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Fredrick Mofulu, ambaye ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ibanda - Kyerwa, alisema ujenzi wa lango hilo la Hifadhi unahusisha sehemu ya ukaguzi wa nyaraka na malipo, ofisi za wahasibu, ofisi za askari upande wa kuingia na kutokea, ofisi ya Afisa Utalii na msaidizi wake, ofisi ya Tehama, ujenzi wa barabara kilometa mbili, na mifumo ya umeme.Pia, ujenzi wa vyoo upande wa kuingia, na kutokea vyenye mashimo 7 ya kawaida 1 walemavu kwa kila jengo, uchimbaji wa visima viwili, fensi ya umeme mita 400, Nyumba 2 za watumishi (Jengo 1 kwa familia 2), Nyumba 3 za watumishi (Jengo 1 kwa familia 4), vimbweta 08, sehemu ya kupaki magari makubwa na madogo upande wa kutoka na kuingia lenye ukubwa wa kilometa za mraba 5400, mfumo wa umeme jua, pamoja na eneo la kupumzikia wageni. Kazi ambayo inatekelezwa na Kampuni ya MJT Crew Co. Ltd na JV Sumry’s Enterprises Ltd za hapa nchini ambapo mpaka sasa ujenzi uko asilimia 55 na inatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.Msimamizi wa Mradi kutoka kampuni ya MJT Crew Co. Mhandisi Issa Mfaume aliishukuru menejimenti ya Shirika kwa kuwapatia malipo ya mradi kwa wakati na kupelekea kazi kufanyika kwa ubora unaotakiwa na kuahidi kukamilisha kazi hiyo kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vilivyopo kwenye mkataba wa kazi.Vilevile, Kamishna Kuji alizungumza na Maafisa na Askari wa Jeshi la Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa Ibanda - Kyerwa na Hifadhi ya Rumanyika - Karagwe na kusitiza utendaji kazi imara ili kusukuma mbele gurudumu la Uhifadhi na Utalii ambalo tumekabidhiwa na Serikali.“Wapiganaji ndio nguzo ya kupeleka mbele Shirika letu nitoe pongezi zangu za dhati kwa askari wetu ambao jua ni lao na mvua ni yao kuhakikisha Rasilimali hizi zinalindwa na kuwa urithi kwa vizazi vilivyopo na vijavyo” alisema Kamishna KujiAidha, Kamishna Kuji alisisitiza kuwa kila mtumishi ana haki ya kujiendeleza kielimu, haki ya kulipwa posho kwa kila kazi aliyoifanya, haki ya matibabu, likizo, haki ya kupandishwa cheo pale unapotimiza vigezo vyote vya kiutumishi pamoja na haki ya kuthaminiwa kutokana na kazi unayofanya.Wapiganaji kwa namna mbalimbali wamepongeza jitihada zinazofanywa taasisi katika kutatua changamoto zao na kupongeza namna viongozi wanawafikia katika maeneo yao, wanasikiliza na kutatua changamoto hizo.“Nikupongeze Afande Kamishna Kuji licha ya majukumu uliyonayo unatoka na kuja kuzungumza na askari, tumekuona Serengeti, tumekuona uko Saanane, sasa Ibanda Kyerwa na Rumanyika Karagwe ukaribu huu kwetu kama askari na kiongozi wa juu wa taasisi unatia hamasa na morali zaidi ya kuchapa kazi“ alisema askari wa uhifadhi daraja la kwanza Henry Joseph Msabila.

Articles similaires

BILLIONI 3.9 KUIMARISHA MIUNDOMBINU HIFADHI YA TAIFA IBANDA-KYERWA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 05:32

 Na.Edmund Salaho - Kyerwa KageraSerikali imetoa kiasi cha Tsh. Billioni 3.9 kwa ajili ya kuimarisha miundombinu katika Hifadhi ya Taifa Ibanda -...

TANAPA yaanza na mkakati wa kuboresha barabara zilizopo Hifadhi za Taifa hususani barabara ya Serengeti

msumbanews.co.tz - 05/Sep 06:02

 WADAU wa Utalii katika Hifadhi ya Taifa Serengeti wameiomba Serikali kupatia suluhisho la kudumu la ujenzi wa barabara katika Hifadhi za Taifa...

ASKARI UHIFADHI NGORONGORO WATAKIWA KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA WANANCHI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 15:13

 Askari Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) wametakiwa kujenga mahusiano mazuri na wananchi wanaozunguka Hifadhi ya...

ASKARI UHIFADHI NGORONGORO WATAKIWA KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA WANANCHI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 15:13

 Askari Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) wametakiwa kujenga mahusiano mazuri na wananchi wanaozunguka Hifadhi ya...

DKT. KIRUSWA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA YA UTOAJI HUDUMA MGODINI

msumbanews.co.tz - 07:00

 Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameshuhudia Utiaji Saini wa Mikataba ya usambazaji na utoaji wa huduma mgodini katika mgodi wa uchimbaji...

MAKAMU WA RAIS DKT. PHILIP MPANGO ATOA WITO WA MABORESHO KATIKA USIMAMIZI WA MAZINGIRA

msumbanews.co.tz - 10/Sep 05:59

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma...

WANANCHI WENGINE 228 WAHAMA NGORONGORO

msumbanews.co.tz - 08/Sep 07:50

Katika muendelezo wa hamasa ya wananchi wa Ngorongoro kujiandikisha kuhama kwa hiari, leo tarehe 7 Septemba, 2024 jumla ya kaya 58 zenye wananchi 228...

ZOEZI LA KUHAMA KWA HIARI LIPO PALEPALE - WAZIRI CHANA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 05:54

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amesisitiza kuwa zoezi la kuhama kwa hiari kwa wananchi wa Ngorongoro linaendelea...

ZOEZI LA KUHAMA KWA HIARI LIPO PALEPALE - WAZIRI CHANA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 05:54

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amesisitiza kuwa zoezi la kuhama kwa hiari kwa wananchi wa Ngorongoro linaendelea...

WAZEE TUNDURU WAOIMBA SERIKALI KUFUNGUA SOKO JIPYA LA MADINI YA VITO

msumbanews.co.tz - 12/Sep 07:54

Baadhi ya majengo katika soko jipya la madini ya vito yanayoendelea kujengwa na Halmashauri ya wilaya Tunduru kwa kushirikiana na wadau wa madini...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément