X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - Hier 07:00

DKT. KIRUSWA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA YA UTOAJI HUDUMA MGODINI

 Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameshuhudia Utiaji Saini wa Mikataba ya usambazaji na utoaji wa huduma mgodini katika mgodi wa uchimbaji Madini ya Urani uliopo katika Kijiji cha Likuyu kilichopo Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma.Mikataba hiyo imesainiwa Septemba 18, 2024 ambayo imehusisha Kampuni ya Ako Group Tanzania Limited ambayo ni mzabuni wa Kampuni ya Mantra na vikundi vilivyoundwa na wazawa vitakavyo toa mahitaji mbalimbali kwa mzabuni huyo. Ako Group wanatoa huduma ya chakula na usafi katika mradi huo, hivyo mikataba hiyo itasaidia ununuzi wa mahitaji muhimu ya chakula na usafi kufanyika ndani ya Wilaya ya Namtumbo na kukuza uchumi wa jamii hiyo.  Aidha, Dkt. Kiruswa amekagua maendeleo ya mradi wa uchimbaji Madini ya Urani katika mgodi wa Mantra ambapo ameridhishwa na maendeleo ya mradi na kuahidi kushughulikia mikwamo iliyopo kwa haraka ili uzalishaji wa madini hayo uanze kama inavyo tarajiwa. Naye, Meneja wa Uendelevu Mradi wa Mantra, Majani Wambura amesema mpaka sasa mradi huo umetumia zaidi ya dola za Kimarekani milioni 240 katika ujenzi wa mradi na inategemewa mpaka kukamilika kwake dola za Kimarekani zaidi ya bilioni moja zitatumika na ajira zaidi ya 700 zitatengenezwa kwa jamii. Pamoja na mambo mengine, Dkt. Kiruswa ametatua na kumaliza mgogoro uliodumu kwa muda mrefu kati ya Kampuni ya Mantra na Kikundi cha Kuza Uchumi wa Namtumbo (KUNA) ambacho kinadai fidia ya eneo ulipo mradi kwasasa, wakidai kuwa eneo hilo lilikiwa linamilikiwa na babu zao ambao waliondolewa kwa nguvu na Wakoloni kati ya mwaka 1940 - 1945 na baadae eneo kutwaliwa na Serikali na kulifanya kuwa hifadhi ya Taifa.  Dkt. Kiruswa amesema fidia ni haki ya Kisheria kwa mtu atakaye hamishwa katika eneo lake kupisha mradi, hata hivyo, madai ya fidia ya Kikundi hiki hayana msingi thabiti wa Kisheria kama ulivyo wasilishwa, hivyo amewashauri wanakikundi hao kuangalia kwa upana faida watakazo nufaika nazo kwa uwepo wa mradi huu ikiwa ni pamoja na fursa ya Kisheria ya wajibu wa Mmiliki wa Leseni kwa Jamii (CSR) pamoja na Ushiriki wa Watanzania kwenye Uchumi wa Madini (Local Content). Aidha, Dkt. Kiruswa amekutana na kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed kwa lengo la kupata taarifa za shughuli za madini Mkoani humo ambapo ameupongeza Mkoa huo kwa kuvuka malengo ya makusanyo ya maduhuli ya Serikali kwa asilimia 119 katika robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2024/25.Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Abbas amempongeza Dkt. Kiruswa kwa kufanya ziara Mkoani humo na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa. Awali, Dkt. Kiruswa aliungana na Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa kukagua ujenzi wa miundombinu ya Uwanja wa Ndege inayoendelea Mkoani humo iliyoghalimu kiasi cha shilingi bilioni 37 ambapo maboresho yaliyofanyika ni pamoja na jengo la kuongoza ndege, uzio wa uwanja, taa za kuongoza ndege, eneo la urukaji wa ndege na lami katika barabara za uwanja wa ndege.

Articles similaires

NI MARUFUKU BIASHARA YEYOTE YA MADINI KUFANYIKA MAJUMBANI WILAYANI TUNDURU – WAZIRI MAVUNDE

msumbanews.co.tz - 17/Sep 16:46

 Waziri wa Madini Anthony Mavunde amepiga marufuku biashara ya madini kufanyika majumbani kwa watu na kusisitiza kwamba hatua kali za kisheria...

SERIKALI YAVUNA TRILIONI 1.8 KUPITIA SEKTA YA UZIDUAJI NCHINI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 10:22

 SERIKALI imepata  jumla ya shilingi Trilioni 1.877 kutoka  kwenye kampuni 44  zilizolinganishwa katika sekta ya madini, mafuta na gesi ikiwa na...

SERIKALI YAVUNA TRILIONI 1.8 KUPITIA SEKTA YA UZIDUAJI NCHINI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 10:22

 SERIKALI imepata  jumla ya shilingi Trilioni 1.877 kutoka  kwenye kampuni 44  zilizolinganishwa katika sekta ya madini, mafuta na gesi ikiwa na...

MAKAMU WA RAIS DKT. PHILIP MPANGO ATOA WITO WA MABORESHO KATIKA USIMAMIZI WA MAZINGIRA

msumbanews.co.tz - 10/Sep 05:59

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma...

KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA UWEKEZAJI KIWANDA CHA MKULAZI

msumbanews.co.tz - 09/Sep 06:59

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatuma Toufiq akizungumza wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua...

WAZIRI MAVUNDE AYATAKA MAKAMPUNI YA MAKAA YA MAWE KUWEKEZA KATIKA UZALISHAJI WA UMEME

msumbanews.co.tz - 17/Sep 05:17

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde amezipongeza Kampuni za uzalishaji wa makaa ya mawe kwa kuongeza uzalishaji na kuzitaka kuelekeza zaidi...

AHADI YA RAIS SAMIA YA UJENZI WA KIWANDA CHA CHUMVI YAANZA KUTEKELEZWA

msumbanews.co.tz - 18/Sep 10:04

 Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema kuwa Ujenzi wa Kiwanda cha kusafisha madini ya chumvi kinachojengwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)...

AHADI YA RAIS SAMIA YA UJENZI WA KIWANDA CHA CHUMVI YAANZA KUTEKELEZWA

msumbanews.co.tz - 18/Sep 10:04

 Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema kuwa Ujenzi wa Kiwanda cha kusafisha madini ya chumvi kinachojengwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)...

DKT. BITEKO ASISITIZA MAADILI, WELEDI NA UWAJIBIKAJI KATIKA UNUNUZI WA UMMA

msumbanews.co.tz - 09/Sep 13:54

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezitaka Mamlaka za Udhibiti na Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki kuzingatia weledi,...

KISHINDO CHA TAMASHA LA UTAMADUNI RUVUMA,RAIS SAMIA APONGEZWA

msumbanews.co.tz - 14/Sep 11:05

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Ahmed Abbas Ahmed ,akizungumza na wamiliki wa hoteli kuhusu fursa za Tamasha la Kitaifa la Utamaduni Baadhi ya wamiliki wa...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément