X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 12/Sep 10:22

SERIKALI YAVUNA TRILIONI 1.8 KUPITIA SEKTA YA UZIDUAJI NCHINI

 SERIKALI imepata  jumla ya shilingi Trilioni 1.877 kutoka  kwenye kampuni 44  zilizolinganishwa katika sekta ya madini, mafuta na gesi ikiwa na tofauti ya kati ya malipo na mapato ya shilingi milioni 402.41 kwa mwaka kwa mwaka wa fedha 2021/22.Hayo yamebainishwa na Waziri wa   wa Madini Mheshimiwa Anthony Mavunde katika uzinduzi wa ripoti ya 14 ya Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji Katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) uliofanyika jijini Dar es Salaam.Mheshimiwa Mavunde amesema kati ya kampuni hizo, kampuni 26 ni za Madini; Kampuni saba  ni za gesi asilia na mafuta; na Kampuni 11 ni kampuni zinazotoa huduma katika sekta ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia. Amesema,  kampuni zilionesha kuwa zililipa kiasi cha shilingi trillion  1.878 serikalini na kupelekea kuwepo na tofauti kati ya malipo na mapato ya shilingi milioni 402 sawa na asilimia asilimia 0.021 ya mapato yote yaliyoripotiwa na Serikali. Mheshimiwa Mavunde ameelekeza, tofauti hiyo sh milioni 402 kufanyiwa uchambuzi wa kina ili kujua visababishi vilivyosababisha kutofautiana ili Kamati iweze kuzipa makampuni na serikaliushauri wa nini kifanyike ili tofauti hizo zisiendelee kujitokeza kwenye linganishi zitakazofuata.Amesema, pamoja na masuala mengine yaliyomo  ripoti hiyo ya  TEITI pia imeweka wazi taarifa mbalimbali ili kutekeleza matakwa ya Viwango vya Kimataifa vya EITI pamoja na Sheria inayosimamia shughuli za TEITI nchini. Mheshimiwa Mavunde amesema, taarifa hizo ni pamoja na takwimu za uzalishaji na usafirishaji wa rasilimali madini, mafuta na gesi asilia (Production and export data), takwimu za ajira katika sekta ya uziduaji, michango ya kampuni kwa jamii (Corporate Social Responsibilities-CSR) na ushiriki wa wazawa katika sekta ya uziduaji ikijumuisha kutoa huduma kwenye kampuni za uziduaji (Local content).Akizungumza katika hafla hiyo,Mwenyekiti wa kamati ya TEITI Ndg. Ludovick Utouh amesema lengo la uzinduzi wa ripoti hiyo ni kuweka wazi kwa ajili ya wananchi nawadau mbalimbali ili waweze kutumia takwimu zilizomo kufanya mijadala ya kuboresha na kuongeza mchango wa sekta ya madini, mafuta na gesi asilia katika Pato la Taifa.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dkt. David Mathayo ameipongeza serikali kwa kutoa taarifa ya wazi ya ulinganisho wa mapato yatokanayo na sekta ya uziduaji na kutumia fursa hiyo kuwataka watanzania waipitie na kuona namna ambavyo sekta hii ya uziduaji inavyochangia kukuza uchumi wa nchi na kuwataka pia wananchi kutumia taarifa hii kushauri na kutoa maoni yao.

Articles similaires

EWURA YAHAKIKI TAARIFA ZA MAMLAKA ZA MAJI 82 NCHINI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:56

Mkurugenzi wa Gesi Asilia EWURA, Mha. Poline Msuya, akizungumza na watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini, kwa niaba ya...

BILIONI 15 KUSAMBAZA UMEME KWENYE VITONGOJI 105 VYA MKOA WA SIMIYU

msumbanews.co.tz - 26/Oct 05:36

 Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA); tarehe 24 Oktoba 2024 imemtambulisha rasmi mkandarasi; kampuni ya CCC (Beijing) Industrial &...

TANZANIA MBIONI KUZALISHAJI MADINI YA NIOBIUM

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:21

 Imeelezwa kwamba Tanzania ipo mbioni kuanza uzalishaji wa madini ya Niobium ambayo ni moja ya madini adimu yanayotumika katika mitambo mbalimbali...

REA YATOA KIPAUMBELE UJENZI MIRADI YA NISHATI JADIDIFU

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:22

 Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa kipaumbele kwenye ujenzi wa miradi ya nishati jadidifu nchini ili kusaidia utunzaji wa mazingira, kuzalisha...

ZAIDI YA WANANCHI 32,000 WA VIJIJI VYA WILAYA ZA MOROGORO NA MVOMERO KUANZA KUPATA MAWASILIANO

msumbanews.co.tz - 04/Nov 18:47

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi MaryPrisca Mahundi (Mb), amesema Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia...

WAZIRI MKUU AKAGUA MIUNDOMBINU YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI DODOMA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:01

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2024) amefanya ziara jijini Dodoma ili kukagua utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi...

SERIKALI YAFIKIA ASILIMIA 85 KATIKA UPATIKANAJI WA DAWA

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:32

 Na : Jusline Marco;ArushaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu upatikanaji wa...

WAZIRI JENISTA ASISITIZA ULAJI WA LISHE BORA YENYE KUZINGATIA VIRUTUBISHI

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:39

 Na;Jusline Marco :ArushaWaziri wa Afya nchini Jenista Mhagama amewataka wadau wa afya kuendelea kushirikiana na serikali katika kuimarisha utoaji wa...

REA KUPELEKA UMEME VISIWA VYOTE TANZANIA BARA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:27

 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...

PUMA ENERGY TANZANIA YATAKIWA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUFANIKISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

msumbanews.co.tz - 26/Oct 16:32

 PUMA Energy Tanzania imetakiwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini kufanikisha azma ya Serikali ya kuhakikisha inatekeleza ipasavyo mkakati wa...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément