Mkurugenzi wa Gesi Asilia EWURA, Mha. Poline Msuya, akizungumza na watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini, kwa niaba ya...
Vous n'êtes pas connecté
SERIKALI imepata jumla ya shilingi Trilioni 1.877 kutoka kwenye kampuni 44 zilizolinganishwa katika sekta ya madini, mafuta na gesi ikiwa na tofauti ya kati ya malipo na mapato ya shilingi milioni 402.41 kwa mwaka kwa mwaka wa fedha 2021/22.Hayo yamebainishwa na Waziri wa wa Madini Mheshimiwa Anthony Mavunde katika uzinduzi wa ripoti ya 14 ya Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji Katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) uliofanyika jijini Dar es Salaam.Mheshimiwa Mavunde amesema kati ya kampuni hizo, kampuni 26 ni za Madini; Kampuni saba ni za gesi asilia na mafuta; na Kampuni 11 ni kampuni zinazotoa huduma katika sekta ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia. Amesema, kampuni zilionesha kuwa zililipa kiasi cha shilingi trillion 1.878 serikalini na kupelekea kuwepo na tofauti kati ya malipo na mapato ya shilingi milioni 402 sawa na asilimia asilimia 0.021 ya mapato yote yaliyoripotiwa na Serikali. Mheshimiwa Mavunde ameelekeza, tofauti hiyo sh milioni 402 kufanyiwa uchambuzi wa kina ili kujua visababishi vilivyosababisha kutofautiana ili Kamati iweze kuzipa makampuni na serikaliushauri wa nini kifanyike ili tofauti hizo zisiendelee kujitokeza kwenye linganishi zitakazofuata.Amesema, pamoja na masuala mengine yaliyomo ripoti hiyo ya TEITI pia imeweka wazi taarifa mbalimbali ili kutekeleza matakwa ya Viwango vya Kimataifa vya EITI pamoja na Sheria inayosimamia shughuli za TEITI nchini. Mheshimiwa Mavunde amesema, taarifa hizo ni pamoja na takwimu za uzalishaji na usafirishaji wa rasilimali madini, mafuta na gesi asilia (Production and export data), takwimu za ajira katika sekta ya uziduaji, michango ya kampuni kwa jamii (Corporate Social Responsibilities-CSR) na ushiriki wa wazawa katika sekta ya uziduaji ikijumuisha kutoa huduma kwenye kampuni za uziduaji (Local content).Akizungumza katika hafla hiyo,Mwenyekiti wa kamati ya TEITI Ndg. Ludovick Utouh amesema lengo la uzinduzi wa ripoti hiyo ni kuweka wazi kwa ajili ya wananchi nawadau mbalimbali ili waweze kutumia takwimu zilizomo kufanya mijadala ya kuboresha na kuongeza mchango wa sekta ya madini, mafuta na gesi asilia katika Pato la Taifa.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dkt. David Mathayo ameipongeza serikali kwa kutoa taarifa ya wazi ya ulinganisho wa mapato yatokanayo na sekta ya uziduaji na kutumia fursa hiyo kuwataka watanzania waipitie na kuona namna ambavyo sekta hii ya uziduaji inavyochangia kukuza uchumi wa nchi na kuwataka pia wananchi kutumia taarifa hii kushauri na kutoa maoni yao.
Mkurugenzi wa Gesi Asilia EWURA, Mha. Poline Msuya, akizungumza na watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini, kwa niaba ya...
Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA); tarehe 24 Oktoba 2024 imemtambulisha rasmi mkandarasi; kampuni ya CCC (Beijing) Industrial &...
Imeelezwa kwamba Tanzania ipo mbioni kuanza uzalishaji wa madini ya Niobium ambayo ni moja ya madini adimu yanayotumika katika mitambo mbalimbali...
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa kipaumbele kwenye ujenzi wa miradi ya nishati jadidifu nchini ili kusaidia utunzaji wa mazingira, kuzalisha...
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi MaryPrisca Mahundi (Mb), amesema Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia...
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2024) amefanya ziara jijini Dodoma ili kukagua utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi...
Na : Jusline Marco;ArushaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu upatikanaji wa...
Na;Jusline Marco :ArushaWaziri wa Afya nchini Jenista Mhagama amewataka wadau wa afya kuendelea kushirikiana na serikali katika kuimarisha utoaji wa...
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...
PUMA Energy Tanzania imetakiwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini kufanikisha azma ya Serikali ya kuhakikisha inatekeleza ipasavyo mkakati wa...