X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 13/Sep 08:04

KAMATI ZA MAAFA WILAYA ZATAKIWA KUWEKA MIPANGO YA DHARURA

Serikali imezitaka Kamati za Usimamizi wa Maafa Ngazi ya Wilaya kuhakikisha zinajiandaa kikamilifu na kuweka mpango wa dharula wa utendaji na uratibu wa mawasiliano katika kukabiliana na maafa kwenye maeneo yao.Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga, wakati akifungua mafunzo kwa Kamati ya Maafa Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Menejimenti ya maafa kwa kushirikiana na Shirika la World Vision Tanzania.Aidha, Mhe. Nderiananga amezitaka taasisi zinazohusika na masuala ya usafiri, nishati pamoja na maji, kujiimarisha wakati wote ili kuhakikisha huduma za kijamii haziathiriki wakati wa maafa.“Serikali ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga vyema kuhakikisha inakabiliana na maafa, tumeweza kununua vifaa vya kisasa kabisa ambavyo vinaweza kutupatia taarifa yoyote ya hali ya hewa inayotusaidia kujiandaa kabla ya maafa, wakati wa maafa na kurejesha hali,” alisema Naibu Waziri.Sambamba na hilo Mhe. Nderiananga, ameipongeza Idara ya Menejimenti ya Maafa katika ofisi hiyo kwa namna inavyoshirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha inakabiliana na maafa pamoja na kurejesha hali katika baadhi ya mikoa iliyokumbwa na maafa ikiwemo mikoa ya Manyara- Hanang na Pwani.Mbali na hayo, Naibu Waziri huyo amesema kuwa ikiwa kamati za usimamizi wa maafa pamoja na taasisi nyingine zinazohusika katika utoaji wa huduma za kijamii, zitaweza kuweka mikakati ya mapema gharama za kupambana na maafa zitakuwa kidogo na wananchi hawatakuwa na hofu.Aidha, amebainisha kuwa serikali ya Rais Samia imefanya maboresho makubwa katika suala la utolewaji wa taarifa sahihi za utabiri wa hali ya hewa, ambapo kamati hizo zimetakiwa kutumia taarifa hizo katika kuweka mikakati hiyo.Nae Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Oparesheni na Uratibu Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Luteni Kanali Selestine Masalamado alieleza kuwa, serikali kwa kushirikiana na Shirika la World Vision wanatoa mafunzo kwa kamati za maafa za wilaya ili kukabiliana na matukio hayo kwa ufanisi.“Tunawashukuru sana World Vision kwani wao ndiyo wanafadhili mpango huu, katika mafunzo haya kamati hizi tunawaelezea namna sheria ya mifumo ya maafa ngazi ya Taifa hadi Kijiji inavyofanya kazi na majukumu ya kila kamati,” alisema Luteni Kanali Masalamando.Vilevile Mkurugenzi wa Uetetezi, Imani na Maendeleo kutoka Shirika la World Vision Dkt. Joseph Mitinje alieleza kwamba shirika hilo limeshirikiana na serikali kutoa mafunzo hayo kwa kamati hizo ili kupunguza madhara yanayotokana na maafa.Alisema, katika mpango wa mwaka huu, World Vision imepanga kutoa mafunzo kwa kamati za usimamizi wa maafa katika Wilaya 8 za Mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Tabora.“ Tunatambua kuwa kamati hizi zikipewa elimu ya namna ya kuweka mipango ya mapema katika kupambana na maafa, kuelezwa majukumu yao katika kupambana na maafa, hatua hii itapunguza madhara yanayotokea kwa wananchi kutokana na maafa,” alisema Dkt. Mitinje.Mwenyekiti Kamati ya Usimamizi wa Maafa Wilaya hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge, ameishukuru serikali pamoja na Shirika la World Vision Tanzania kwa mafunzo hayo, kwani yatawaongezea ujuzi, uwezo na maarifa katika kupambana na maafa kwenye Wilaya hiyo.

Articles similaires

NAIBU WAZIRI MWANAIDI AWATAKA WADAU KUJIKITA VIJIJINI, ELIMU YA KUPINGA UKATILI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:24

  Na WMJJWM-DodomaNaibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amewataka wadau wanaotoa elimu ya...

OUT YATOA MAFUNZO KUIMARISHA UFUATILIAJI NA USIMAMIZI WA MIRADI SERIKALINI

msumbanews.co.tz - 27/Oct 08:36

Mafunzo ya ufuatiliaji na tathmini yanayoendeshwa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa watumishi wa mamlaka za serikali za mitaa pamoja tawala za...

WALIMU WAKUU 17,793 WANOLEWA KUSIMAMIA SHULE KWA UFANISI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 05:54

Serikali kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) imewezesha mafunzo Walimu Wakuu 17,793 katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara kuhusu...

MAKAMANDA TFS WATAKIWA KUTUMIA TEHAMA KUBORESHA UTENDAJI KAZI

msumbanews.co.tz - 05/Nov 14:13

 Na Happiness Shayo- ArushaWaziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa...

KONGAMANO LA JOTOARDHI AFRIKA KULETA UWEKEZAJI NA UBUNIFU MPYA TANZANIA -MHE. KADUARA

msumbanews.co.tz - 26/Oct 05:49

 Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Shaibu Kaduara amesema Kongamano la Kimataifa la Jotoardhi Afrika...

SERIKALI INAENDELEA KUTEKELEZA MRADI WA KUPELEKA UMEME WA GRIDI MTWARA NA LINDI- MHE.KAPINGA

msumbanews.co.tz - 04/Nov 10:54

 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali inatekeleza mradi wa kuiunganisha Mikoa ya Mtwara na Lindi na  umeme wa gridi kutokea...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBU YA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA.

msumbanews.co.tz - 04/Nov 11:16

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali imeendelea kuboresha miundombu ya kutolea...

MADIWANI WAONGEZE KASI YA USIMAMIZI WA UKUSANYAJI WA MAPATO

msumbanews.co.tz - 04/Nov 05:05

 Na, Elizabeth Paulo; Dodoma Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mh. Halima Okash ametoa Rai kwa Viongozi wa Halmashauri kusimamia sheria,...

TGNP YATOA MAFUNZO KWA WANAWAKE WAGOMBEA SERIKALI ZA MITAA

msumbanews.co.tz - 28/Oct 07:43

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umefanya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji ...

SERIKALI YAFIKIA ASILIMIA 85 KATIKA UPATIKANAJI WA DAWA

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:32

 Na : Jusline Marco;ArushaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu upatikanaji wa...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément