X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 10/Sep 04:10

KIPAUMBELE CHA SERIKALI NI KUONA IDADI YA WATUMIAJI WA DATA WANAONGEZEKA- MHANDISI MARYPRISCA

 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi alipotembelea kituo cha Mkongo wa Baharini cha 2 Africa.Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi  akimsikiliza Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano alipotembea mkongo wa Baharini uliopo Mbezi Beach Tangibovu jijini Dar es Salaam.SERIKALI imesema Kipaumbele chake ni kuona idadi ya watumiaji wa data  inaongezeka katika jamii ya Watanzania.Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi wakati alipotembelea Airtel Tanzania na mkongo wa Baharini wa 2 Africa uliopo Mbezi Beach Tangibovu jijini Dar es Salaam leo Agosti 09, 2024. Amesema kuwa kwa sasa watu wachache wamefikiwa na matumizi ya data.Amesema ili matumizi ya mkongo wa Baharini uwe mkubwa lazima simu janja ziwafikie watu wengi zaidi hadi vijijini."Watanzania wakishaweza kupata simu janja hizi kwa gharama nafuu basii matumizi ya mkongo huu wa baharini utakuwa ni makubwa zaidi." Amesema Mhandisi MarypriscaAmesema manufaa zaidi yataonekana na vilevile kituo cha Airtel kitandelea kuwa Cha manufaa zaidi kwasababu watumiaji nao watakuwa wameongezeka kila iitwapo leo.Pia imetoa wito kwa wadau mbalimbali ambao waweza kuingiza simu janja kwa gharama nafuu ili Kila mmoja aweza kupata  na kuongeza matumizi ya mkongo wa 2 Africa yaweze kuwa makubwa zaidi.Amesema serikali inatoa ushirikiano mkubwa ambao unawezesha kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi."Kama hapo zamani walikuwa wanatumia 2G kwamana watu walikuwa wanaweza kupata tu sauti kwahio Sasa wamekuja kuupgrade kwa 3G paka 5G kwalengo la kuboresha matumizi ya data Kama wananchi wanaweza kutumia intaneti kwa wingi lakini vilevile wanaweza kuboresha maisha na kuwa ya kidijitali zaidi." Ameeleza Mhandisi MarypriscaKwa upande wa Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano amefurahishwa na ziara ya naibu waziri Maryprisca Mahundi kutembelea Airtel Kama kampuni ya simu za mkononi."Ziara yake ilianzia hapa kwenye mkongo wa baharini wa 2 Africa Kama mnvyofahamu ni kwamba huu mkongo ambao ulizinduliwa na Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan mwaka jana mwezi wa nane sisi kwetu ni fahari kubwa Sana kwasababu mkongo huu unaunganisha mabara matatu nikimaanisha Afrika, Asia na Europe lakini vilevile una ukubwa wa km zaid ya 45 elfu." AmelezaAmesema kuwa mkongo huu utaisaidia Tanzania kwa kuifungua na kumekuwa na mikakati mingi  pia  wanakukaribisha wawekezaje kuja nchini kwani miundombinu hiyo ni muhimu sana na inatoa mawasiliano lakini pia inaunganisha mabara mbalimbali.Pia amewakaribisha wadau wote wa mawasiliano kwenda kununua 'capacity' uwezo kutoka kwenye kituo mkongo wa baharini wa 2 Africa kilichopo Mbezi Beach Tangibovu jijini Dar Es Salaam.

Articles similaires

TTCL YAUNGANISHA WILAYA 106 KWENYE MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO

msumbanews.co.tz - 05:32

Mkurugenzi wa Ufundi na Undelezaji kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL,Mhandisi Cecil Francis ameeleza kuwa wamefanikiwa kuunganisha wilaya...

AIRTEL TANZANIA YAENDELEA KUPANUA WIGO VIJIJINI

msumbanews.co.tz - 06:15

Kampuni ya simu za mkononi Airtel kupitia kwa Mkurugenzi wa Biashara Joseph Muhele amesema kuwa mtandao huo mwaka huu 2024 unaendelea kufangua...

WAZIRI MAHUNDI AITAKA UCSAF KUTANGAZA SHUGHULI KUPITIA VYOMBO VYA HABARI

msumbanews.co.tz - 11/Sep 05:11

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), amewataka viongozi wa Mfuko wa Mawasiliano...

WAZIRI MAHUNDI AHITIMISHA ZIARA YA KUTEMBELEA WATOA HUDUMA ZA MAWASILIANO DAR

msumbanews.co.tz - 12/Sep 16:57

Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amehitimisha ziara yake ya siku tatu kutembelea...

WAZIRI MAHUNDI AHITIMISHA ZIARA YA KUTEMBELEA WATOA HUDUMA ZA MAWASILIANO DAR

msumbanews.co.tz - 12/Sep 16:57

Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amehitimisha ziara yake ya siku tatu kutembelea...

NAIBU WAZIRI MAHUNDI ATEMBELEA OFISI ZA UCSAF

msumbanews.co.tz - 10/Sep 20:25

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi MaryPrisca Mahundi (Mb), ametembelea Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote...

DKT. BITEKO ASISITIZA MAADILI, WELEDI NA UWAJIBIKAJI KATIKA UNUNUZI WA UMMA

msumbanews.co.tz - 09/Sep 13:54

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezitaka Mamlaka za Udhibiti na Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki kuzingatia weledi,...

TANZANIA YAWEKEZA KIMKAKATI KATIKA SEKTA YA TEHAMA ILI KUKUZA UCHUMI WA KIDIJITALI

msumbanews.co.tz - 08:01

Tanzania ina mifumo kadhaa ya kisheria na udhibiti inayoongoza sekta ya mawasiliano na TEHAMA ili kuhakikisha huduma ya intaneti ya kasi inawafikia...

HOSPITALI ZOTE NCHINI ANZENI KUTUMIA SIMU ZA UPEPO

msumbanews.co.tz - 14/Sep 05:11

 Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amezitaka Hospitali zote nchini kuanzisha mfumo wa matumizi ya simu za upepo ili kupunguza matumizi ya siku za...

MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA ELIMU ATEMBELEA MRADI WA EASTRIP, NIT

msumbanews.co.tz - 14/Sep 05:06

 KUPITIA Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) inatekeleza mradi wa EASTRIP (East Africa Skills for...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément