X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 12/Sep 05:50

WMA kutoa gawio la sh. Bilioni 7.7 mwaka wa Fedha 2025/2026

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Alban Kihulla akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari katikq Mkutano mwendelezo ya Mikutano inayoratibiwa na Msajili wa Hazina ,Jijini Dar es Salaam.Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri akizungumza kuhusiana mikutano kati Mashirika ya Umma yaliyo chini ya Msajili wa Hazina na Wahariri wa Vyombo vya HabariWahariri na Waandishi wakipitishwa kuangalia uhalisia wa vipimo katika Mkutano ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina Jijini Dar es Salaam.AFISA  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Alban Kihulla amesema kuwa Wakala huo unatarajia kutoa Gawio la Serikali Sh.Bilioni 7.7 katika mwaka wa Fedha 20025/2026.Kihulla ameyasema hayo wakati akizungumza na wa Wahariri na Waandishi katika Mkutano ulioandaliwa na Msajili wa Hazina na kufanyika jijini Dar es Salaam.Amesema katika miaka mitano wameendelea kutoa gawio katika kuhakikisha maendeleo yakapatikana kwa wananchi ambapo mwaka wa fedha 2018/2019 gawio la sh.Bilioni 4.2.,2019/2020 gawio la sh.bilioni5.3.,2020/2021 gawio la sh.bilioni6.2.,2021/2022 gawio la sh bilioni 4.2.,2022/2023 gawio la sh bilioni 4.3Amesema hadi kufikia hapo WMA imepita hatua tofauti tofauti Kwa kuanzia Ukoloni ikiwa katika Idara ya Wizara ya Mambo ya Ndani ambapo sasa ipo Wizara ya Viwanda na Biashara.Amesema majukumu ya WMA ni kumlinda mlaji kupitia uhakiki na udhibiti wa vipimo vinavyotumika katika biashara na huduma nyingine pamoja na kuhakikisha kuwa vipimo hivyo viko sahihi na vinatumika kwa usahihi kulingana na sheria ya vipimo.Amesema kuwa wameendelea kutoa elimu kuhusiana na vipimo na kuwa na Ofisi katika mikoa yote ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya vipimo na pale wanapowazika kutoa taarifa.Kihulla amesema kuwa wamejenga Ofisi Mkoa wa Pwani wa Kupima Mita za Maji ,Mita za Umeme pamoja na kupima matanki ya mafuta yanayoenda mikoani na nchi jirani Mafuta katika kupata uhalisia wa ujazo.Aidha amesema wameweka mikakati mbalimbali ambapo mikakati hiyo wamejenga jengo la Makao Makuu jijini Dodoma pamoja na kuendelea kuelimisha wananchi kuhusiana na vipimo ambao ndio walaji wa mwisho.Amesema kuwa mpango mwingine ni kwenda katika michezo ya kubahatisha vipimo vinavyotumika pamoja na vifurushi vinavyotolewa na Mitandao ya Simu za Mkononi.

Articles similaires

WMA YAHIMIZA USHIRIKIANO KUTOKA SEKTA BINAFSI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 08:08

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...

WMA YAHIMIZA USHIRIKIANO KUTOKA SEKTA BINAFSI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 08:08

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...

WMA, TAKUKURU WATEKELEZA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA

msumbanews.co.tz - 09/Sep 07:07

 Na Veronica Simba, WMA DodomaWakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Dodoma imetoa elimu ya vipimo kwa Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa...

WAZIRI JAFO: WIZI WA KUCHEZEA VIPIMO NI KOSA KISHERIA

msumbanews.co.tz - 12/Sep 07:50

 WAZIRI  wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo amehimiza wananchi jijini Mwanza kuzingatia matumizi sahihi ya vipimo kila mara wanapofanya...

Wakala Wa Vipimo Tanzania watoa msaada wa vifaa kwa jeshi la polisi

msumbanews.co.tz - 11/Sep 05:52

 JESHI la polisi limesema kuwa limedhamiria kuboresha huduma zake ikiwa ni pamoja na kubadili fikra juu ya jeshi hilo, kusimamia sheria kikamilifu...

UGONJWA WA FMD WAJADILIWA KUTOVUKA MIPAKA YA NCHI ZA EAC NA SADC

msumbanews.co.tz - 10/Sep 17:36

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Abdul Mhinte akizungumza jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mkutano wa wataalamu kutoka...

TANZANIA YAAHIDI KUENDELEA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 05:55

 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii yaahidi kuendelea kuimarisha juhudi za mazingira za kikanda na...

SERIKALINI YAKEMEA UCHAFU WA MASHUKA HOSPITALINI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 10:16

Serikali imesema kuwa itaanza kuchukua hatua kwa wahudumu wa afya watakaobainika kuzembea katika usafi na kusababisha mashuka ya vitanda vya wagonjwa...

SERIKALINI YAKEMEA UCHAFU WA MASHUKA HOSPITALINI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 10:16

Serikali imesema kuwa itaanza kuchukua hatua kwa wahudumu wa afya watakaobainika kuzembea katika usafi na kusababisha mashuka ya vitanda vya wagonjwa...

WMA YATOA MSAADA WA VIFAA VYA TEHAMA KWA JESHI LA POLISI ILALA

msumbanews.co.tz - 11/Sep 10:54

  Na Mahamudu Jamal, WMAWakala wa Vipimo (WMA) imekabidhi msaada wa vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa Jeshi la Polisi Mkoa...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément