X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 13/Sep 06:08

MAIPAC KUJA NA MKAKATI WA KUELIMISHA MADHARA YA UKEKETAJI

 LSF nao kuendelea kusaidia vikundi wanawake Longido.Shirika la Wanahabari la usaidizi wa.jamii za pembezoni(MAIPAC) linatajia  kuzindua mradi kabambe  wa kuelimisha juu ya athari za ukeketaji kwa watoto wa kike katika jamii ya kifugaji ya kimasai ikiwa ni pamoja na kuwajengea wanawake uwezo wa kutetea haki zao.Mradi huo unafadhiliwa na shirika la  Cultural Survival na unatarajiwa kusaidia pia kupaza sauti za vijana wanaopinga vitendo vya ukeketaji.Mkurugenzi wa Shirika la MAIPAC Mussa Juma alitoa taarifa hiyo katika ziara iliyofanywa na Asasi za kirai katika wiki ya Asasi hizo iliyofanyika wilayani Longido ."MAIPAC imebaini kuwa watoto wa miaka miwili hukeketwa katika Jamii ya Kimasai hivyo tunampango wa kuzindua mradi wa kuelemisha kuhusu masuala mazima ya ukeketaji na ukatili kwa watoto wa kike , lakini pia kuwajengea Uwezo wa kujiamini wanawake wa kimasai na kuweza kutetea haki zao za msingi hasa katika kukemea Ukatili" amesema.Katika Ziara iliyofanywa na Asasi za kiraia (CSO) wadau wa asasi hizo wamepata wasaa wakutembelea kikundi cha wanawake wanaofadhiliwa na shirika la Legal Service Facility(LSF) na Vodacom Foundation.Akizungumza na ziara hiyo mkurugenzi wa LSF ,Lulu Ng'wanakilala alisema shirika hilo limekuwa likisaidia vikundi 11 vya wanawake wa jamii ya kifugaji kata Kimokoa wilaya ya Longido.Ng'wanakilala alisema  wanawake wa jamii za kifugaji bado wanakaniliwa na changamoto ikiwepo changamoto za kiuchumi,ushiriki katika siasa na changamoto za kiafya.Hata hivyo alisema kupitia mradi wanaotekeleza longido wameweza kusaidia jamii ya wanawake kiuchumi kwa kuwa na miradi midogo,ushiriki katika masuala ya kisiasa na kupambana na changamoto za kiafya ikiwepo ikeketaji.Katika wiki ya CSO hufanyika mara moja kila mwaka ambapo zaidi ya Wadau 600 wameweza kushiriki na kushirikishana Masuala mbalimbali ya kijamii kwa njia ya midahalo na Majadiliano ya kina yanayolenga Mchango wa CSOs hizo kwa maendeleo ya Taifa.

Articles similaires

MAIPAC KUJA NA MKAKATI WA KUELIMISHA MADHARA YA UKEKETAJI

msumbanews.co.tz - 13/Sep 06:08

 LSF nao kuendelea kusaidia vikundi wanawake Longido.Shirika la Wanahabari la usaidizi wa.jamii za pembezoni(MAIPAC) linatajia  kuzindua mradi...

MAIPAC KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE KUTETEA HAKI ZAO

msumbanews.co.tz - 12/Sep 10:31

 MAIPAC kuzindua mradi wa kuelimisha ukeketaji kwa watoto wa kike katika jamii ya kifugaji ya kimasai ikiwa ni pamoja na kuwajengea wanawake uwezo wa...

MAIPAC KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE KUTETEA HAKI ZAO

msumbanews.co.tz - 12/Sep 10:31

 MAIPAC kuzindua mradi wa kuelimisha ukeketaji kwa watoto wa kike katika jamii ya kifugaji ya kimasai ikiwa ni pamoja na kuwajengea wanawake uwezo wa...

WATUMIA SHEREHE ZA UBATIZO KUKEKETA WATOTO SERIKALI YAONYA

msumbanews.co.tz - 17/Sep 09:34

Baadhi ya familia za Jamii ya kimasai wilaya ya Longido mkoa Arusha,zinadaiwa kutumia sherehe za Ubalozi kukeketa watoto wadogo ili kukwepa kukamatwa...

WANAWAKE LONGIDO WAJENGEWA UWEZO KUTAMBUA HAKI ZAO

msumbanews.co.tz - 12/Sep 06:22

 Wanawake kutoka jamii ya kimaasai katika Tarafa ya Longido wilaya ya Longido mkoa wa Arusha wameonyesha furaha yao baada ya shirika la Legal...

BoT, AZAKI WAJADILI KUBORESHA HUDUMA JUMUISHI ZA FEDHA KWA JAMII

msumbanews.co.tz - 08:23

 Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema itaendelea kufanya jitihada mbalimbali za kusaidia ukuaji wa huduma za malipo kidigitali kwa kuweka miundombinu...

MBUNGE WA MSALALA ASISITIZA UWT KUJIANDIKISHA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA CCM

msumbanews.co.tz - 16/Sep 19:13

 MBUNGE  wa Jimbo la Msalala, Mheshimiwa Iddi Kassim Iddi, amewataka wanawake wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) Kijiji cha Kakola, Kata ya...

WANANCHI LONGIDO WATAKA SHULE ZA BWENI KUIMARISHWA ULINZI

msumbanews.co.tz - 07/Sep 11:12

Wananchi wa Wilaya ya Longido Mkoani Arusha wameiomba serikali kujengea uzio shule zote za serikali za bweni zilizopo katika wilaya hiyo lengo ni...

CPA MAKALLA AWATAKA WATENDAJI MPAKA WA NAMANGA KUONGEZA UFANISI WA UTENDAJI

msumbanews.co.tz - 06/Sep 08:44

 KATIBU wa NEC,Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa, CPA Amos Makalla, amewaelekeza watendaji katika kituo kilichopo katika...

Kamati ya Bunge Yaipongeza UDSM kwa Maboresho ya Mitaala na Utekelezaji wa Mradi wa HEET

msumbanews.co.tz - 11/Sep 04:51

 KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepongeza juhudi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kuboresha mitaala yake ili kukidhi...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément