X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 12/Sep 05:54

WAZIRI JAFO ATAKA WATANZANIA KUJIAMINI NA KUWEKEZA KATIKA VIWANDA NCHINI

 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Selemani Jafo (Mb) akioneshwa na Mkurugenzi wa Hill Group Bw. Hillary Shoo jinsi mchakato wa uzalishaji nyama ya kuku wa kisasa kupitia mtambo wa Grader ambao unatumika kupima kilo ya nyama kabla ya kuwekwa kwenye vifungashio alipotembelea Kiwanda cha Hill Farm kilichopo Matimbwa Bagamoyo Pwani Septemba 11, 2024........Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo ametoa rai kwa Watanzania kujiamini kuwa wananaweza kuanzisha viwanda na kufanya biashara ili kuongeza ajira, pato la Taifa na uchumi wa nchi.Vilevile, ametoa wito kwa Watanzania kupenda kununua na kutumia bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vilivyopo nchini ili kuviwezesha kuendelea na uzalishaji, na kutowavunja moyo wawekezaji.Dkt Jafo ameyasema hayo Septemba 11, 2024 alipotembelea Kiwanda cha Hill Farm kilichopo Matimbwa Bagamoyo Pwani kujionea shughuli za uzalishaji na kisikiliza na kutatua changamoto zao.Aidha, Dkt. Jafo amepongeza uwekezaji huo uliofanywa na hill group ambao umesaidia kuleta mapinduzi katika sekta ya uzalishaji nyama ya kuku wakisasa na kutoa wito kwa wadau wengine kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ambayo inatoa mikopo nafuu kwa wawekezaji katika sekta ya kilimo.Naye Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) nchini Bw. Frank Nyabundege, amewashauri wafanyabiashara na wawekezaji wengine kuwekeza katika viwanda vinavyochakata mazao ya kilimo na mifugo kwa kuwa kuna fursa nyingi za uwekezaji huku akitoa wito kwa wawekezaji hao kuweza kutumia vizuri fedha za udhamini wanazopata kutoka benki hiyo“ Hapa leo tumeshuhidia uwekezaji wa kisasa ambao pengine Tanzania nzima hakuna katika sekta ya uzalishaji nyama ya kuku wa kisasa , hivyo nitoe pongezi kwa Wizara ya Viwanda na Biashara kuwashika mkono wawekezaji pamoja na Rais wetu ambae ametoa zaidi ya bilioni 100 kwa wawekezaji, nitoe wito kwa wadau wengine kuja Benki ya Maendeleo ya kilimo" Bw. Frank Nyabundege,Kwa upande wake Mkurugenzi wa Makampuni ya Hill Group Bw. Hilary Shoo, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwapa mazingira wezeshi ya kufanya biashara na uwekezaji huku wakipata msamaa wa kodi mbalimbali kutoka Serikalini na TADB kwa mkopo wa gharama nafuu  Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Selemani Jafo (Mb) akioneshwa na Mkurugenzi wa Hill Group Bw. Hillary Shoo jinsi mchakato wa uzalishaji nyama ya kuku wa kisasa kupitia mtambo wa Grader ambao unatumika kupima kilo ya nyama kabla ya kuwekwa kwenye vifungashio alipotembelea Kiwanda cha Hill Farm kilichopo Matimbwa Bagamoyo Pwani .  2.Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Selemani Jafo (Mb) akiangalia chumba maalumu uchakatati wa mabaki yanayotokana uzalishaji wa nyama ya kuku ambayo hutumika kutengenezea chakula cha mifugo mingine kama kuku na nguruwe alipotembelea Kiwanda cha Hill Farm kilichopo Matimbwa Bagamoyo Pwani Septemba 11, 2024

Articles similaires

WAZIRI JAFO AMUWAKILISHA RAIS SAMIA MKUTANO WA COMESA NCHINI BURUNDI

msumbanews.co.tz - 31/Oct 14:49

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani S. Jafo leo tarehe 31 Oktoba 2024 amemuwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Wakuu wa...

CHANDE ASHAURI MABENKI KUTANUA WIGO WA MASOKO NJE YA NCHI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:25

 Na. Peter Haule na Josephine Majura, WF, Dodoma Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), ameitaka Akiba Commercial Bank Plc (ACB)...

DKT NCHEMBA AHIMIZA MATUMIZI YA KISWAHILI MIKUTANO YA BENKI YA DUNIA NA IMF

msumbanews.co.tz - 28/Oct 07:45

 Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba madelu (Mb), akiteta jambo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika...

SERIKALI ITAENDELEA KUWATUMIA WATAFITI NCHINI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 16:47

 Na : Jusline Marco : ArushaWaziri wa nchi,ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawane amesema serikali ya...

KATIBU TAWALA MKOA WA SONGWE ATEMBELEA MAADHIMISHO WIKI YA FEDHA KITAIFA

msumbanews.co.tz - 26/Oct 05:45

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda (Kushoto), akimsikiliza Afisa Usimamizi Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Jackson Mushumba,...

TANZANIA MBIONI KUZALISHAJI MADINI YA NIOBIUM

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:21

 Imeelezwa kwamba Tanzania ipo mbioni kuanza uzalishaji wa madini ya Niobium ambayo ni moja ya madini adimu yanayotumika katika mitambo mbalimbali...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA ILI KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO YA WANANCHI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:02

 Na. Joseph Mahumi, WF, MorogoroSerikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo...

Benki ya CRDB Yatunukiwa Tuzo za 'Benki Bora' na 'Benki Salama' Tanzania na Jarida la Global Finance

msumbanews.co.tz - 28/Oct 05:58

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto), akipokea tuzo ya 'Benki Bora Tanzania' kutoka kwa Joseph Giarraputo, Mwanzilishi...

KONGAMANO LA JOTOARDHI AFRIKA KULETA UWEKEZAJI NA UBUNIFU MPYA TANZANIA -MHE. KADUARA

msumbanews.co.tz - 26/Oct 05:49

 Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Shaibu Kaduara amesema Kongamano la Kimataifa la Jotoardhi Afrika...

Wagonjwa wa moyo kutoka Malawi kutibiwa JKCI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:38

 Serikali ya Jamhuri ya Malawi imeahidi kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ili wagonjwa wa moyo waliopo nchini humo hasa watoto...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément