X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 01/Nov 08:22

REA YATOA KIPAUMBELE UJENZI MIRADI YA NISHATI JADIDIFU

 Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa kipaumbele kwenye ujenzi wa miradi ya nishati jadidifu nchini ili kusaidia utunzaji wa mazingira, kuzalisha umeme wa uhakika na kutoa ajira kupitia miradi hiyo. Hayo yamebainishwa leo Oktoba 31, 2024 na Mkurugenzi wa Teknolojia Mbadala na Nishati Jadidifu kutoka REA, Mha. Advera Mwijage alipotembelea mradi wa Mwenga Hydro unaozalisha umeme wa maji wa megawati nne (4) uliopo katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. Mha. Mwijage amesema kuwa, mradi huo umewezeshwa na Serikali kupitia REA kwa kutoa kiasi cha fedha takribani shilingi bilioni 16.6 ikiwemo shilingi bilioni 10 ya kuwaunganisha wateja na shilingi bilioni 6.6 ya utekelezaji wa mradi huo. "Sisi kama wakala tunaendelea kufadhili hii miradi kwa kuhamasisha na kuwawezesha wanaojenga miradi ili kuendeleza shughuli za kiuchumi nchini," amesema Mha. MwijageVile vile, ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fursa kwa wabia wa maendeleo ambao wanaisaidia Serikali katika kutekeleza uzalishaji wa umeme kwenye gridi, kusambazia wananchi na kutoa ajira. Naye, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mwenga Hydro, Deograsias Massawe amesema mradi huo umewezesha wananchi wa vijiji 32 vya Wilaya ya Mufindi kupata umeme wa uhakika hivyo, kuwawezesha kufanya shughuli zao za kiuchumi.Ameongeza kuwa, mradi huo umekuwa na faida kwa wajasiriamali kwa kutoa ajira na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi ambao umepunguza gharama za uendeshaji shughuli za kiuchumi kutokana na kuachana na matumizi ya mafuta na kuhamia kwenye matumizi ya nishati ya umeme. Aidha, ameipongeza REA kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 16.6 ambazo zimefanya maunganisho kwa wateja zaidi ya 8000 wa majumbani, hospitalini, mashuleni na kwenye vituo vya afya.Amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha utekelezaji wa mradi zikiwemo utoaji wa fedha za kuendesha mradi na Sera wezeshi katika nishati jadidifu.Mradi umeanza uzalishaji rasmi mwaka 2012 katika Wilaya ya Mufindi na umelenga kuongeza wateja wapatao 2,900 katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Articles similaires

REA YAFIKISHA UMEME KWA WANANCHI 2400 NJOMBE

msumbanews.co.tz - 31/Oct 09:15

 Imeelezwa kuwa, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umepeleka umeme kwa wananchi wapatao 2,400 wa vijiji nane (8) vya Tarafa ya Lupembe, Wilaya ya...

REA KUPELEKA UMEME VISIWA VYOTE TANZANIA BARA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:27

 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...

GGML YAKABILIWA NA SHINIKIZO KUKAMILISHA MIRADI YA MAENDELEO YA CSR GEITA

msumbanews.co.tz - 12/Nov 12:17

Geita,Tanzania Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita limekutana kujadili na kupitisha mpango wa wajibu wa Kampuni ya Mgodi wa Dhahabu...

DC MPOGOLO APONGEZA JUHUDI ZA ELIMU KABLA YA MIKOPO KWA WAJASIRIAMALI

msumbanews.co.tz - 12/Nov 05:32

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa utekelezaji wa maagizo ya serikali ya kuhakikisha utoaji...

SERIKALI INAENDELEA KUTEKELEZA MRADI WA KUPELEKA UMEME WA GRIDI MTWARA NA LINDI- MHE.KAPINGA

msumbanews.co.tz - 04/Nov 10:54

 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali inatekeleza mradi wa kuiunganisha Mikoa ya Mtwara na Lindi na  umeme wa gridi kutokea...

CCM WAHIMIZWA KUHAMASISHA WATANZANIA KUENDELEZA UMOJA NA MSHIKAMANO

msumbanews.co.tz - 11/Nov 06:19

 Na Gideon Gregory, Dodoma.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...

WAZIRI MKUU AKAGUA MIUNDOMBINU YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI DODOMA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:01

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2024) amefanya ziara jijini Dodoma ili kukagua utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi...

ZAIDI YA WANANCHI 32,000 WA VIJIJI VYA WILAYA ZA MOROGORO NA MVOMERO KUANZA KUPATA MAWASILIANO

msumbanews.co.tz - 04/Nov 18:47

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi MaryPrisca Mahundi (Mb), amesema Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia...

DC MPOGOLO AWATAKA WABUNIFU NA WAKADIRIAJI MAJENZI KUWA WAZALENDO

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:38

 Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ametoa wito kwa Wabunifu na Wakadiriaji majenzi nchini kuwa Wazalendo, Waadilifu na Wabunifu kwa Taifa katika...

RAIS SAMIA AIPA TANROADS ZAIDI YA BIL 500 UJENZI MIUNDOMBINU DAR ES SALAAM

msumbanews.co.tz - 10/Nov 08:34

Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan zaidi ya Shilingi Bilioni 500...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément