X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 05/Nov 16:50

DKT. MWAMBA ATETA NA UJUMBE KUTOKA EU

 Na. Joseph Mahumi na Chedaiwe Msuya, WF, DodomaKatibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Timu ya Wataalamu kutoka Shirika la Umoja wa Ulaya iliyoongozwa na Mkuu wa Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Marc Stalmans, katika ukumbi wa Mikutano wa Katibu Mkuu, jijini Dodoma.Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni tathmini ya utekelezaji wa maeneo ya vipaumbele vya ushirikiano vilivyokubalika katika kipindi cha Miaka 7 kuanzia mwaka 2021 hadi 2027, Mpango wa kijani (Green Deal), Mtaji wa Watu na Ajira (Human Capital and Employment) na Utawala (Governance)) maarufu kama Multiannual Indicative Programme 2021-2027. Aidha walikubaliana juu ya mwelekeo wa uandaaji wa miradi mipya kwa mwaka 2025 (Annual Action Plan 2025 - AAP 2025). Pamoja na Mambo mengine walitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa awamu ya kwanza kwa miaka minne (4) ambao umetekelezwa kwa mafanikio makubwa, ambapo jumla ya EURO 366 Millioni (sawa na trilioni 1.075 za kitanzania) zimetengwa kwenye miradi 6 ya kitaifa na EURO 141 Milioni (sawa bilioni 414.17 za kitanzania) zimetengwa kwenye miradi ya kikanda inayoendelea. Hadi sasa Umoja wa Ulaya umeidhinidha utekelezaji wa awamu ya pili wa mpango huo ambapo kiasi cha EURO 219 Millioni (sawa bilioni 641.95 za kitanzania) zitaelekezwa kwenye vipaumbele vya awali pamoja na Miradi inayohusu Malighafi Muhimu (Critical Raw Materials).Kikao hicho kilihudhuriwa na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. James Msina, Mkuu wa Masuala ya Msaada kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya, Kitengo cha Uratibu na Ushirikiano, Bw. Jonathan Mpuya, Mkuu wa Fedha na Utawala - Kitengo cha Uratibu na Ushirikiano, Bw. Ibrahim Muhazi, Afisa wa Mpango wa Rasilimali Asili, Bw. Leonard Lema, na maafisa wengine kutoka Umoja wa Ulaya nchini.

Articles similaires

TANZANIA NA EU KUIMARISHA USHIRIKIANO

msumbanews.co.tz - 13:07

 Na. Joseph Mahumi, WF, Dar es SalaamTanzania imeishukuru Umoja wa Ulaya (EU) kwa kuendelea kuwa miongoni mwa washirika wakubwa wa kimkakati wa...

TANZANIA NA EU KUIMARISHA USHIRIKIANO

msumbanews.co.tz - 13:07

 Na. Joseph Mahumi, WF, Dar es SalaamTanzania imeishukuru Umoja wa Ulaya (EU) kwa kuendelea kuwa miongoni mwa washirika wakubwa wa kimkakati wa...

REA KUPELEKA UMEME VISIWA VYOTE TANZANIA BARA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:27

 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...

TANZANIA NA UGANDA ZAKUTANA KUJADILI UIMARISHAJI MPAKA WA KIMATAIFA

msumbanews.co.tz - 05/Nov 17:11

Na Munir Shemweta, WANMM Bukoba Kikao cha Kamati ya Pamoja cha Wataalamu wa Tanzania na Uganda (JTC) kimeanza mkoani Kagera nchini Tanzania...

REA YATOA KIPAUMBELE UJENZI MIRADI YA NISHATI JADIDIFU

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:22

 Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa kipaumbele kwenye ujenzi wa miradi ya nishati jadidifu nchini ili kusaidia utunzaji wa mazingira, kuzalisha...

CCM WAHIMIZWA KUHAMASISHA WATANZANIA KUENDELEZA UMOJA NA MSHIKAMANO

msumbanews.co.tz - 06:19

 Na Gideon Gregory, Dodoma.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...

CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WA UMMA ZITATULIWE ILI KUKUZA SEKTA YA UMMA KIUCHUMI NA KIJAMII

msumbanews.co.tz - 05/Nov 09:20

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa neno la utangulizi kabla ya...

SERIKALI ITAENDELEA KUWATUMIA WATAFITI NCHINI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 16:47

 Na : Jusline Marco : ArushaWaziri wa nchi,ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawane amesema serikali ya...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA ILI KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO YA WANANCHI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:02

 Na. Joseph Mahumi, WF, MorogoroSerikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo...

JKCI, MOI NA MNH zaitwa Comoro kwenda kutoa huduma za matibabu ya kibingwa

msumbanews.co.tz - 05/Nov 10:24

Na Mwandishi Maalumu – Dar es Salaam 04/11/2024 Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Watu wa Comoro Mhe. Yousoufa Mohamed Ali ameziomba Taasisi ya...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément