X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 17/Sep 09:34

WATUMIA SHEREHE ZA UBATIZO KUKEKETA WATOTO SERIKALI YAONYA

Baadhi ya familia za Jamii ya kimasai wilaya ya Longido mkoa Arusha,zinadaiwa kutumia sherehe za Ubalozi kukeketa watoto wadogo ili kukwepa kukamatwa na kufikishwa Mahakama ni.Watoto wengi  wadogo chini ya miaka miwili wamebainika kufanyiwa ukatili wa kukeketwa katika baadhi ya vijiji wilaya ya Longido.Wakizungumza katika uzinduzi wa mradi wa kupaza sauti kupinga matukio ya ukeketaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilaya ya Longido ambao unatekelezwa na Shirika la wanahabari la MAIPAC kwa ufadhili wa Shirika la Cultural Survival, viongozi wa Serikali na halmashauri ya Longido walionya serikali kuendelea kuwachukulia hatua wanaokeketa watoto.Afisa Maendeleo wa halmashauri ya wilaya ya Longido,Rashid Hussein alisema baada ya serikali kuimarisha msako wa wanaokeketa watoto mbinu mpya imeibuka kwa watoto kukeketwa kwa Siri katika sherehe za ubatizo."Tayari tumebaini hili na tumetoa maelekezo kwa viongozi kuanzia ngazi za kitongoji kufatilia na wakibaini ukeketaji kwenye sherehe za Ubatizo watupe taarifa mapema "alisema Alisema hata hivyo wamebaini kumekuwepo na tatizo la baadhi ya viongozi kumaliza kesi kwa mazungumzo vijijini na akaonua viongozi ambao watafumbia macho ukeketaji katika maeneo Yao serikali itawachukulia hatua.   Wanawake wazuiwa kula wakiwa na ujauzito.Katika haya nyingine mganga Mkuu wa wilaya ya Longido,Dk Methew Majani amesema wamebaini wanawake kuwa dhaifu wanapofikishwa hospitali kujifungua kutokana na kutopewa chakula ili eti waje kujifungua watoto wadogo.Dk Majani alisema kwa kuwa wanawake wamekeketwa na ili kusipate shida zaidi wanapofika hospitali kujifungua wanazuia vya vyakula jambo ambalo limekuwa likisababisha uzazi pingamizi jambo ambalo ni hatari kwa maisha Yao na watoto."Lakini kibaya zaidi wanacheleweshwa kufika vituo vya afya akina mama wajawazito hili jambo halifai kwani serikali ya Rais Samia Suluhi imejitahidi kujenga vituo vya afya na hospitali ili wanawake wapate huduma nzuri na mapema zaidi"alisemaAlisema ukeketaji umekuwa ukisababisha Vifo vya akina mama na watoto  kutokana na kutokwa damu nyingi lakini pia kukosa nguvu za kujifungua Salama.Mkurugenzi wa Shirika la MAIPAC,Mussa Juma alisema mradi huo umekuja baada ya waandishi kufanya utafiti katika wilaya hiyo na kubaini licha ya kazi kubwa ya Serikali na halmashauri kupinga ukeketaji lakini bado watoto wadogo wabakeketwa."Tuliwatuma waandishi vijijini kwenda kufanya uchunguzi nanwalitupa taarifa ambayo tulitumia kutafuta wafadhili kupata fedha ya kutoa elimu zaidi ya Kupambana na ukeketaji napaza sauti na tunamshukuru Cultural Survival kutufadhili"alisema           Wahanga wa ukeketaji watoa ushuhuda.Merikinoi orkesyanye alitoa ushuhuda kuwa amekeketwa na amezaa watoto wanane lakini wakati akijifungua Mtoto wa nane alipata tatizo la festura kutokana na kufanyiwa ukeketaji."Tumepata hii Shida kutokana na ukeketaji na ninashukuru mganga huyu wa wilaya na wengine wamenisaidia Sasa nimeona na naomba wanawake wenzangu na wazee wa Mila tuache ukeketaji kwani no hatari kwa afya zetu na watoto "alisemaAkitoa mafunzo ya athari za ukeketaji , Mary Laizer alisema ukeketaji alisema yeye amekeketwa na anachokifanya kuhakikisha watoto hawakeketwi na ameweza kuvusha Mtoto wake wa kike Rika bila kukeketwa.Mary alisema ukeketaji una madhara makubwa ikiwepo kutokwa damu nyingi,kuondoka starehe na kubwa kueleza kupoteza maisha ya mama na Mtoto.Mary akionesha aina mbalimbali za ukeketaji na madhara yake na kuwataka wanawake na wanaume kuungana kupiga vita ukeketaji.Katika mradi huo wa MAIPAC kwa kushirikiana na wadau ikiwepo shirika la Tembo na halmashauri wanatarajiwa kufika vijiji mbalimbali kupinga ukeketaji na kuunda kamati za vijiji kupinga ukeketaji.

Articles similaires

NAIBU WAZIRI MWANAIDI AWATAKA WADAU KUJIKITA VIJIJINI, ELIMU YA KUPINGA UKATILI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:24

  Na WMJJWM-DodomaNaibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amewataka wadau wanaotoa elimu ya...

RUWASA Tanga yaagizwa kusimamia Wananchi kuanzisha vitalu vya miti.

msumbanews.co.tz - 01/Nov 10:58

Na Denis Chambi, Tanga.MKUU wa mkoa wa Tanga  Balozi Dkt. Batilda Buriani  ameuwagiza Wakala wa Maji vijijini 'RUWASA' kuhakikisha wanasimamia...

REA KUPELEKA UMEME VISIWA VYOTE TANZANIA BARA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:27

 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...

MKUU WA WILAYA GEITA AWAONYA WANANCHI KUHUSU ULAJI USIOFAA NA MAGONJWA

msumbanews.co.tz - 31/Oct 15:42

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba, amewahimiza wananchi wa wilaya hiyo kujikita zaidi katika lishe bora na kuachana na tabia ya ulaji usiofaa...

CCM DODOMA MJINI YAANZA KUWANOA MABALOZI KUJIANDAA NA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

msumbanews.co.tz - 06/Nov 16:57

Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Dodoma Mjini kimeanza mikutano ya ndani ya kuwajengea uwezo wenyeviti wa mashina(Mabalozi) kuelekea Uchaguzi wa...

MIRADI YA TACTIC KUIMARISHA MAZINGIRA YA UFANYAJI WA BIASHARA NCHINI- MHE. KATIMBA.

msumbanews.co.tz - 02/Nov 16:02

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema kukamilika kwa Miradi ya TACTIC mkoani...

MABALOZI WA CCM BUKOBA MJINI WATUMA SALAAM KWA RAIS SAMIA

msumbanews.co.tz - 08/Nov 19:56

 Semina ya Sheria za Uchaguzi na Vyama Vya Siasa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Ushiriki wa Wanawake katika Siasa  imefanyika Novemba 7...

Jakaya Kikwete aipongeza NMB kwa Bil. 1 za Matibabu ya Watoto JKCI

msumbanews.co.tz - 04/Nov 08:09

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete, amekiri kuvutiwa na mchango mkubwa wa Benki ya NMB wa Sh. Bilioni 1 kati ya Sh. Bil....

UJENZI WA SOKO LA MWANGA NA KATONGA UTAIMARISHA MAZINGIRA YA BIASHARA KIGOMA- MHE. KATIMBA.

msumbanews.co.tz - 02/Nov 16:10

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema ujenzi wa Soko la Kisasa la Mwanga na Soko la...

NLD watoa wito kwa TAMISEMI kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.

msumbanews.co.tz - 05/Nov 13:38

 Na Denis Chambi, Tanga.CHAMA cha National league for Democracy 'NLD' kimeitaka  Ofisi ya Rais tawala za mika na Serikali za mitaa 'TAMISEMI'...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément