X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 19/Sep 06:15

AIRTEL TANZANIA YAENDELEA KUPANUA WIGO VIJIJINI

Kampuni ya simu za mkononi Airtel kupitia kwa Mkurugenzi wa Biashara Joseph Muhele amesema kuwa mtandao huo mwaka huu 2024 unaendelea kufangua huduma  zake za mawasiliano katika miji na Vijiji ambapo kwa mjini kuwezesha kupata huduma ya 3G,4G,5G na Kampuni inaendelea na Uwekezaji na upanuzi wa mtandao maeneo ya Vijiji ili kuwezesha kupata huduma ya 3G 4G na 5G.Aidha ameeleza kuwa kwa mwaka 2013 kampuni hiyo ilifunga mtambo mpya Submarinecable ambao ni mkubwa wenye uwezo wa kupokea na kutumia data kwa kiwango kikubwa ,uwekezaji huo umefanywa kwa ajili ya Watanzania na nchi jirani kwajili ya mawasiliano. Muhele ameendelea kufafanua kuwa lengo la Mkutano huo wa 8 ni kuwaleta Wadau wote pamoja katika teknolojia, ambapo kampuni hiyo inaendelea kuvifikia Vijiji vyote ambavyo havijafikiwa na huduma hiyo ambapo sasa wanajenga huduma ya 5G kwa ajili ya wateja Ujenzi ambao unaenda sambamba na kuhakikisha gharama zinakuwa nafuu.Kwa upande wake Waziri wa Habari ,Mawasiliano Teknolojia ya habari Jerry Slaa akifungua kogamano hilo la siku mbili (Connect2Connect Summit) ambapo limewakutanisha wadau wote wa Mawasiliano nchini pamoja na wadau wengine ambapo amesema Watanzania zaidi ya Mil.75 wana simu za mkononi 35% wanamtandao wa intaneti ambapo mwaka mei 2023 Serikali ilizindua mkakati wa ujenzi wa minara 758 kupitia USAF mfuko uliotengenezwa na seeikali ambapo kila mtoa huduma anachangia ili kupeleke huduma Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo Mhe. Always alisema minara mingine 636 mradi huo utaanza Oktoba 2024 huku akiwatak wananchi wanaofanya shughuli zao kupitia mitandao wapo salama zaidi na Serikali imetunga Sheria ya kulinda data za mtu binafsi katika matumizi ya mtandao na kila mtumiaji analindwa na hairuhusiwi kutumia data za mtu bila ridhaa yake.Aidha Waziri Slaa,amesema hadi sasa 89% ya Watanzania wanapata huduma mtandao lengo likiwa Wananchi wote wapate huduma ya mtandao  wa Internet,simu ,habari ,redio na televisioni yakuwemo maeneo ya Utalii ambayo yamepewa kipaumbele Kwa upande wake injinia Cecil Mkomola Francis  mkurugenzi wa ufundi na Uendeshaji wa Shirika la mawasiliano Tanzania TTCL amesema wanadhamana kubwa ya kutoa huduma ya mawasiliano, kupitia mkongo wa mawasiliano wa Taifa kwani wameendelea kufanya kazi na kuhakikisha kuwa nchi inaongea kwa kuunganishwa mikoa wilaya ambapo jumla ya wilaya 106 zimeunganishwa Tanzanzania bara Kati ya wilaya 139,mkongo huo ndio kiungo kikuu cha  Mawasiliano na Intaneti. Amesema kuwa kazi kubwa waliyonayo kama Shirika ni kutoa mchango mkubwa wa mawasiliano kuhakikisha kwamba wanafikisha huduma kwa Wananchi na kupungiza gharama za matumiziupande wake  ,Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la mhandis Francis Mkomola,amesema Shirika hilo lina dhamana kubwa ya kutoa huduma bora za mawasiliano kupitia mkongo wa taifa  ambao ulianza kutekeleza mwaka 2013.Vilevile wameunda mkongo huo na nchi jirani za Kenya,Uganda ,Rwanda,Burundi ,Zambia,Malawi na kuna maunganusho yanayoenda kwenye mpaka na Msumbijina sasa wanaanza kushughulikia maunganusho na nchi ya DRC Congo,kupitia ziwa Tanganyika hadi mji wa Kalemii Nchini DRC pia wanashugulikia maunganisho  kwenda kwenye kituo  kilichopo baharini hadi Mombasa Nchini Kenya.TTCL inaendelea kutoa mchango wa mawasiliano kuhakikisha mkongo unaojengwa inakuwa na ubora wa hali ya juu kwa lengo la kufikisha huduma  kwa Wananchi na kupunguza gharama ambapo Tanzania ni kiunganishi kikuu cha Mawasiliano kwenye ukanda wa nchi za EAC na SADC, wilaya ambazo  hazijaunganishwa kwenye mkongo wa taifa zitaunganishwa mwaka huu na wakandarasi wapo wanaendelea na shughuli hiyoMkutano huu umehusisha wadau wote wa mawasiliano nchini  Tanzania chini ya kauli mbiu ya ‘Meaningful Connectivity’

Articles similaires

PUMA ENERGY TANZANIA YATAKIWA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUFANIKISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

msumbanews.co.tz - 26/Oct 16:32

 PUMA Energy Tanzania imetakiwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini kufanikisha azma ya Serikali ya kuhakikisha inatekeleza ipasavyo mkakati wa...

REA YAFIKISHA UMEME KWA WANANCHI 2400 NJOMBE

msumbanews.co.tz - 31/Oct 09:15

 Imeelezwa kuwa, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umepeleka umeme kwa wananchi wapatao 2,400 wa vijiji nane (8) vya Tarafa ya Lupembe, Wilaya ya...

SERIKALI YAFIKIA ASILIMIA 85 KATIKA UPATIKANAJI WA DAWA

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:32

 Na : Jusline Marco;ArushaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu upatikanaji wa...

REA KUPELEKA UMEME VISIWA VYOTE TANZANIA BARA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:27

 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...

ZAIDI YA WANANCHI 32,000 WA VIJIJI VYA WILAYA ZA MOROGORO NA MVOMERO KUANZA KUPATA MAWASILIANO

msumbanews.co.tz - 04/Nov 18:47

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi MaryPrisca Mahundi (Mb), amesema Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia...

REA YATOA KIPAUMBELE UJENZI MIRADI YA NISHATI JADIDIFU

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:22

 Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa kipaumbele kwenye ujenzi wa miradi ya nishati jadidifu nchini ili kusaidia utunzaji wa mazingira, kuzalisha...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA ILI KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO YA WANANCHI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:02

 Na. Joseph Mahumi, WF, MorogoroSerikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo...

AICC NI MUHIMILI WA SEKTA YA UTALII NCHINI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 09:36

 Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kimeelezwa kuwa ni moja ya muhimili muhimu katika kufanikisha agenda ya Rais Samia Suluhu Hassan...

AIRTEL WAZINDUA DUKA KATIKA KITUO CHA TRENI YA SGR DAR ES SALAAM

msumbanews.co.tz - 08/Nov 06:52

 Mtendaji Mkuu wa TRC, Masanja Kadongosa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la Airtel katika kituo cha Treni ya Kisasa kilichopo jijini Dar es...

NAIBU WAZIRI MWANAIDI AWATAKA WADAU KUJIKITA VIJIJINI, ELIMU YA KUPINGA UKATILI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:24

  Na WMJJWM-DodomaNaibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amewataka wadau wanaotoa elimu ya...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément