X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 15/Sep 05:02

OSHA YAWAWEZESHA WACHIMBAJI, WAPONDAJI KOKOTO DAR ES SALAAM

 Wajasiriamali wadogo wapatao 500 wanaojihusisha na uchimbaji na uchakataji kokoto Jijini Dar es Salaam wamewezeshwa vifaa kinga na kupatiwa mafunzo ya usalama na afya ili kujiepusha na ajali, magonjwa na vifo vinavyoweza kusababishwa na vihatarishi vilivyopo katika mazingira ya kazi.Uwezeshaji huo umefanywa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ikiwa ni utekelezaji wa jukumu lake la msingi la kujenga uelewa wa masuala ya usalama na afya miongoni mwa waajiri, wafanyakazi na wananchi kwa ujumla.Makundi yaliyonufaika na uwezeshaji huo kwa hatua ya awali ni wale ambao wanafanya shughuli zao katika maeneo ya Boko Magereza, Kata ya Bunju katika Wilaya ya Kinondoni na maeneo ya Mjimwema katika Wilaya ya Kigamboni.Akifungua program hiyo ya uwezeshaji wa wachimbaji wadogo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete, amesema pamoja na changamoto zinazowakumba wachimbaji na wachakataji wadogo wa kokoto ikiwemo matumizi ya teknolojia duni na ukosefu wa mitaji, mchango wa wachimbaji hao katika uzalishaji wa malighafi za ujenzi ni mkubwa.“Ninapenda kuwatia moyo kwamba changamoto zilizopo katika sekta hii hazitakuwa za kudumu. Hivyo, niwaombe tushirikiane kuchukua hatua za kuleta mabadiliko chanya katika sekta hii ikiwemo kuhakikisha kwamba shughuli zote zinafanyika katika mazingira salama na tija inaongezeka kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa,” ameeleza Waziri Kikwete na kuongeza:“Kwa upande wetu kama serikali tumeshaanza kuchukua hatua kwa kuanzia na kuwapa elimu kama inavyofanyika leo lakini tutaendelea na hatua nyingine ikiwemo kutengeneza mazingira wezeshi yatakayopelekea tija kuongezeka ikiwemo kuhakikisha mnapata mitaji kwa ajili ya kununua zana za kisasa ikiwa ni pamoja na kuanzisha shughuli mbadala.”Katibu Mkuu wa Wizara yenye dhamana ya Masuala ya Kazi, Bi. Mary Ngelela Maganga, aliyehudhuria baadhi ya madarasa ya semina iliyokuwa ikiendeshwa na wataalam wa OSHA, amesema kwa kuzingatia mchango wa wajasiriamali wadogo katika maendeleo ya nchi, Taasisi yake ya OSHA imeona ni muhimu kuwapa elimu ya usalama na afya wachimbaji hao ili waweze kuchukua tahadhari dhidi ya ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, amesema mafunzo yanayotolewa na wataalam wake kwa wachimbaji wadogo yamejikita katika kuwawezesha kutambua vihatarishi vinavyoambatana na shughuli zao ikiwemo vumbi, joto kali na mtindo wa ufanyaji kazi usiozingatia taratibu za igonomia.Aidha, Kiongozi huyo Mkuu wa Taasisi ya OSHA ameeleza kuwa mafunzo hayo yanaambatana na utoaji wa vifaa kinga muhimu vilivyogharamiwa na serikali ili kuwahamasisha wachimbaji hao kuzingatia matumizi sahihi ya vifaa kinga katika kazi zao.Vifaa kinga vilivyotolewa kwa wajasiriamali hao ni pamoja na barakoa, vikinga mikono (gloves), vizibao vinavyoakisi mwanga (reflective vests) kutambulisha uwepo wa mfanyakazi mahali pa kazi pamoja na masunduku ya huduma ya kwanza.Wajasiriamali walionufaika na uwezeshaji huo akiwemo Bi.Berena Bilal, wameishukuru serikali kupitia OSHA kwa uwezeshaji waliopata.“Kwa niaba wajasiriamali wenzangu naishukuru OSHA kwa kutuelimisha na kutuletea vifaa kwani awali tulikuwa hatufahamu hatari zinazotuzunguka lakini leo wataalam wametufahamisha na kutupatia mbinu za kudhibiti hatari hizo,” amesema Bi Berena Bilal.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete, akizungumza na wachimbaji na wapondaji wa kokoto waliowezeshwa na OSHA kwa kupatiwa mafunzo ya usalama na afya pamoja na vifaa vya kujikanga katika machimbo ya Masasi, Mjimwema, Kigamboni Jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Ngelela Maganga, akimkabidhi kiongozi wa wachimbaji na wapondaji wa kokoto wa eneo la Boko Magereza, sanduku la huduma ya kwanza mara baada ya kuwapa mafunzo ya usalama na afya kazini.Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya usalama na afya kwa wachimbaji na wapondaji wa kokoto Kigamboni Jijini Dar es Salaam.Mkufunzi wa Huduma ya Kwanza wa OSHA, Bi. Moteswa Meda akiwaongoza washiriki wa mafunzo ambao ni wapondaji wa kokoto wa eneo la Boko Magereza kufanya mazoezi ya kutoa huduma ya kwanza kwa vitendo.

Articles similaires

WAJASIRIAMALI WA NCHI WANACHAMA EAC WAHAMASISHWA KUWA WABUNIFU

msumbanews.co.tz - 05/Nov 18:44

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulrmavu, Zuhura Yunus akizungumza wakati hafla ya Siku ya Tanzania iliyofanyika...

OUT YATOA MAFUNZO KUIMARISHA UFUATILIAJI NA USIMAMIZI WA MIRADI SERIKALINI

msumbanews.co.tz - 27/Oct 08:36

Mafunzo ya ufuatiliaji na tathmini yanayoendeshwa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa watumishi wa mamlaka za serikali za mitaa pamoja tawala za...

SERIKALI YAFIKIA ASILIMIA 85 KATIKA UPATIKANAJI WA DAWA

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:32

 Na : Jusline Marco;ArushaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu upatikanaji wa...

WAZIRI MKUU AKAGUA MIUNDOMBINU YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI DODOMA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:01

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2024) amefanya ziara jijini Dodoma ili kukagua utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi...

JKCI, MOI NA MNH zaitwa Comoro kwenda kutoa huduma za matibabu ya kibingwa

msumbanews.co.tz - 05/Nov 10:24

Na Mwandishi Maalumu – Dar es Salaam 04/11/2024 Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Watu wa Comoro Mhe. Yousoufa Mohamed Ali ameziomba Taasisi ya...

SERIKALI ITAENDELEA KUWATUMIA WATAFITI NCHINI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 16:47

 Na : Jusline Marco : ArushaWaziri wa nchi,ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawane amesema serikali ya...

Wagonjwa wa moyo kutoka Malawi kutibiwa JKCI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:38

 Serikali ya Jamhuri ya Malawi imeahidi kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ili wagonjwa wa moyo waliopo nchini humo hasa watoto...

WALIMU WAKUU 17,793 WANOLEWA KUSIMAMIA SHULE KWA UFANISI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 05:54

Serikali kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) imewezesha mafunzo Walimu Wakuu 17,793 katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara kuhusu...

TGNP YATOA MAFUNZO KWA WANAWAKE WAGOMBEA SERIKALI ZA MITAA

msumbanews.co.tz - 28/Oct 07:43

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umefanya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji ...

TFS HAKIKISHENI MNAJIKITA KWENYE TEHAMA MKAKUSANYE MAPATO ZAIDI : WAZIRI CHANA

msumbanews.co.tz - 06/Nov 07:00

Waziri wa Maliasili na Utali,Balozi Dkt Pindi Chana amemwagiza Kamishina wa Wakala wa Huduma na Misitu{TFS},Professa Do Santos Silayo kuhakikisha...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément