X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 24/Feb 05:11

MASAUNI:SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI MCHANGO WA DINI ZOTE

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Dini zote katika kujenga maadili mema ndani ya jamii ya Watanzania hivyo kila mmoja amaowajibu wa kusaidia katika kutekeleza jukumu la malezi.Amesema vijana wakifundishwa mila na desturi sahihi na kushika mafundisho ya dini, na wakawa na hofu ya Mwenyezi Mungu, maovu mengi yatapungua hapa nchini kwani mustakabali wa taifa unaujengwa na sisi wenyewe kwa kusaidiana kuilea jamii katika maadili mema hasa kwa vijana ambao ndio viongozi watarajiwa wa taifa.Waziri Masauni ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar, ameyasema hayo katika mahafali ya Chuo cha Kislamu cha MPF Zanzibar Februari 22, 2025 ambapo alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza ya chuo hicho.“Kuifundisha jamii ni jambo la kuenziwa kwa vile umma wa sasa umekumbwa na vishawishi vibaya ambavyo kwa njia moja ama nyingine huwatoa watu kwenye mwelekeo. Vishawishi vibaya vinaonekana dhahiri katika jamii. Sasa tunaposimama kuichunga jamii, yote kiujumla na mmomonyoko wa maadili si tu tunawasaidia wao waweze kutimiza ndoto zao bali ni kwa ustawi wa taifa letu kwa ujumla ili kufikia malengo tuliojiwekea. “Kipekee nitumie nafasi hii kuwashukuru viongozi wetu wakuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa miongozo na maelekezo mbalimbali wanayotupatia ambayo yameendelea kuleta mafanikio ya maisha bora kwetu Watanzania. “Kuhusu madarasa ya Sayansi ya Malezi ya Nafsi, napenda kumuambia Amir na Kiongozi Mkuu wa MPF karibuni Madina nami ni miongoni mwa Annsar. Hivyo basi nipo tayari kwa ajili ya kufanya kazi kwa karibu nawe na timu yako katika eneo hili na huku tukipata mwongozo na msaada kutoka kwa Mlezi wetu wa Zanzibar Mheshimiwa Mufti Mkuu wa Zanzibar Samahat Sheikh Saleh Omar Kaab.” amesema Waziri Masauni.Amesema anafarijika kuona MPF kupitia Amir Mkuu na Kiongozi kwa namna wanavyotafsiri kwa vitendo maono ya Marais wetu, kwenye eneo la kuyajenga maadili ya vijana, wazee na watoto ambapo pia ni sehemu ya kujenga ufanisi wa watu wetu kwenye maisha yao mmoja mmoja na jumla kama Taifa. “Naomba niendelee kuwashukuru ndugu zangu wa MPF kwa kazi wanazofanya na hapa pia naomba kuweka bayana kuwa mimi ni Mshawishi wa MPF. Hakika mara ya kwanza kupata habari zenu na kuona kwa ufupi juhudi na mafanikio yake nikakubali kuwa mshawishi wao bila kusita na huku sikuwa najua kuwa juhudi zao pia zipo Zanzibar tena jimboni kwangu.”Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni akizungumza katika mahafali ya Chuo cha Kislamu cha MPF Zanzibar Februari 22, 2025 ambapo alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza ya chuo hicho. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibari, Sheikh Abbu Simba na kulia kwake ni Amiri Mkuu wa Chuo cha MPF, Omar Othman Msuya.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni akimkabidhi cheti Asha Ali Hassan mhitimu katika mahafali ya Chuo cha Kislamu cha MPF Zanzibar Februari 22, 2025 ambapo alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza ya chuo hicho. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibari, Sheikh Abbu Simba na kulia kwake ni Amiri Mkuu wa Chuo cha MPF, Omar Othman Msuya.Picha za pamoja katika makundi mbalimbali za matukio

Articles similaires

MAWAZIRI WAKUTANA KUJADILI UCHUMI WA BULUU

msumbanews.co.tz - 14/Feb 04:27

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amesemea Uchumi wa Buluu ni dhana inayochagiza...

MAKAMU WA RAIS ATOA WITO KWA WAANDAAJI WA VIPINDI VYA ELIMU KWA UMMA KUHAMASISHA UHIFADHI WA MAZINGIRA NA MATUMIZI YA NISHATI SAFI

msumbanews.co.tz - 21/Feb 19:32

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi iliyotolewa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)...

KAMATI YA PIC YAONA TIJA UWEKEZAJI KIWANDA CHA UZALISHAJI BIDHAA ZA NGOZI

msumbanews.co.tz - 19/Feb 07:06

 🎈🎈Waziri Ridhiwani Kikwete aihakikishia uwekezaji endelevuKamati ya Bunge ya Uwekezaji na mitaji ya Umma (PIC) imepongeza serikali ya Awamu ya...

TCAA YAWAPA WABUNGE MAFUNZO JUU YA UDHIBITI NA USALAMA WA ANGA

msumbanews.co.tz - 13/Feb 15:31

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imefanya mafunzo kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za...

TCAA YAFANYA MAFUNZO KWA WABUNGE

msumbanews.co.tz - 14/Feb 08:16

 Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imefanya mafunzo kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu...

KAWAIDA: AJENDA YA MITANO TENA NI DKT. SAMIA NA DKT. MWINYI TU, VIJANA TWENDE TUKAGOMBEE

msumbanews.co.tz - 18/Feb 06:50

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC) amewatoa hofu vijana ambao wanataka kuwania nafasi za udiwani, ubunge na uwakilishi kuwa...

TUNDUMA WAMETEKELEZA MAAGIZO YA RAIS SAMIA KWA KUTOA BIL 4.6 MIKOPO YA 10%" - WAZIRI KIKWETE

msumbanews.co.tz - 03:41

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema hatua ya Halmashauri ya Tunduma kutoa...

WAZIRI SIMBACHAWENE ATOA WITO KWA WANANCHI WA CHIPOGOLO KUSHIRIKI MAENDELEO

msumbanews.co.tz - 04:58

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene akizungumza na...

SERIKALI YAJIDHATITI KUBORESHA SEKTA YA KILIMO – DKT BITEKO

msumbanews.co.tz - 14/Feb 09:02

 📌 Anadi soko la mazao jamii ya mikunde India📌 Mnada mazao ya kunde mtandaoni waboresha biashara ya kimataifa📌 Biashara kati ya Tanzania na...

KWA KIKOSI HIKI,CCM HII UNAISHINDAJE EEH! UNAISHINDAJE

msumbanews.co.tz - 16/Feb 20:00

Na Dk. Reubeni LumbagalaChama Cha Mapinduzi (CCM) ni chama kikongwe nchini, sasa kimetimiza miaka 48 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977. Ukongwe wa...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément