X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - Aujourd'hui 04:58

TIMU YA WASHAURI KUTOKA AfDB YAVUTIWA NA UKUAJI WA UCHUMI

Na. Peter Haule na Farida Ramadhani, WF, DodomaWashauri Waandamizi wa Wakurugenzi Watendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wameanza ziara ya siku tano nchini kwa ajili ya kuelewa vipaumbele vya maendeleo ya Tanzania na namna AfDB inavyoweza kuchangia shughuli zenye matokeo chanya na kubadilisha  maisha ya watanzania.Akizungumza kuhusu ziara hiyo, baada ya kukutana na ujuembe huo jijini Dodoma, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, alisema kuwa ziara ya Washauri hao ni sehemu ya ajenda ya kila mwaka ya Bodi ya Wakurugenzi Watendaji wa AfDB katika nchi wanachama wa Kanda. Alisema pamoja na kuelewa vipaumbele hivyo, washauri hao watapata fursa ya kuelezewa mwenendo wa uchumi wa nchi, kujadili miradi inayotekelezwa nchini kwa kushirikiana na Benki hiyo ikiwa ni pamoja na kuangalia changamoto zilizopo na namna ya kuzitatua.“Uchumi wa Tanzania umeendelea kuwa imara ambapo kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2024 uchumi umekua kwa asilimia 5.4 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 4.8 kwa mwaka 2023, ambapo ukuaji huo umechochewa na uwekezaji kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na miradi ya nishati, maendeleo ya jamii na miundombinu ya usafirishaji”, alisema Bi. Shaaban.Aidha, alieleza kuwa mfumuko wa bei umeendelea kuwa imara kwa wastani wa asilimia 3.1 kwa mwaka 2024 ikilinganishwa na asilimia 3.8 kwa mwaka 2023.Vilevile alisema kuwa Tanzania inatekeleza zaidi ya miradi 29 Tanzania Bara na Zanzibar ikiwa na thamani ya takribani dola za Marekani bilioni 3.91 ikiwemo ya maji, miundombinu, nishati, kilimo, sekta binafsi na uendelezaji wa ujuzi, iliyosainiwa kati ya mwaka 2015 na 2025.Kwa upande wake Kiongozi wa Timu ya Wataalam ya Washauri wa Wakurugenzi Watendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bi. Betty Ngoma, alisema kuwa, wamekuja Wizara ya Fedha ili kujua maendeleo ya uchumi lakini pia mikakati mbalimbali inayotumika katika kukuza uchumi wa nchi.Bi. Ngoma, ameipongeza Tanzania kwa namna inavyoimarisha uchumi wake na namna ilvyoweza kusimamia vema utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inatekelzwa kupitia ufadhili wa Benki hiyo. Alisema wapo nchini ili waweze kujionea miradi inayotekelezwa kwa ufadhili wa Benki hiyo Tanzania Bara na Zanzibar na kujionea juhudi zinazofanywa na Serikali katika kukuza uchumi wake.

Articles similaires

BARRICK NI KIELELEZO BORA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI NCHINI- DKT. KIRUSWA

msumbanews.co.tz - 16/Feb 06:20

 • Kamati ya Bunge Yataka Kampuni Zingine Kuiga Barrick📍 KahamaNaibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, amesema kuwa Kampuni ya Uchimbaji wa...

BARRICK YACHANGIA SHILINGI TRILIONI 3.6 PATO LA SERIKALI KWA KIPINDI CHA MIAKA 4

msumbanews.co.tz - 14/Feb 08:44

Meneja wa Barrick nchini, Dk.Melkiory Ngido akitoa taarifa ya utendaji wa Barrick na Twiga kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na...

BARRICK YACHANGIA SHILINGI TRILIONI 3.6 SERIKALINI KWA KIPINDI CHA MIAKA MINNE

msumbanews.co.tz - 14/Feb 04:23

 • Yachangia Zaidi ya Shilingi Trilioni 11 katika Uchumi wa Tanzania• Gawio la Zaidi ya Shilingi Bilioni 412 latolewa kwa SerikaliKampuni ya...

TANZANIA YAPONGEZWA KWA UKUAJI MZURI WA UCHUMI NA MAENDELEO YA RASILIMALI WATU

msumbanews.co.tz - 21/Feb 19:23

 Na. Farida Ramadhani na Joseph Mahumi, WF, DodomaWashirika wa Maendeleo nchini wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa maendeleo mbalimbali hususan...

MKURUGENZI MOSHI ATOKWA MACHOZI, CCM NA CHADEMA WAKIMPA ZAWADI .

msumbanews.co.tz - 17/Feb 04:57

Mkurugenzi wa Halmashauriya Manispaa ya Moshi Mwajuma NAsombe akizungumza wakati wa kikao cha mwisho cha Bajeti cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri...

WAKANDARASI WASIMAMIWE KUTEKELEZA MIRADI YA NISHATI KWA WAKATI - KAPINGA

msumbanews.co.tz - 05:16

 📌Aagiza wasimamiwe kwa karibu kumaliza miradi📌Awataka Watendaji TANESCO kuwa na mahusiano mazuri na wananchiNaibu Waziri wa Nishati, Mhe....

MAWAZIRI WAKUTANA KUJADILI UCHUMI WA BULUU

msumbanews.co.tz - 14/Feb 04:27

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amesemea Uchumi wa Buluu ni dhana inayochagiza...

WANANCHI WA PASUA NA MAJENGO WAFURAHIA FURSA ZA UWEKEZAJI

msumbanews.co.tz - 14/Feb 03:45

 Na. Eva Ngowi, WF, KILIMANJAROSerikali imetoa rai kwa Wananchi kuwekeza fedha zao sehemu sahihi na salama badala ya kuwekeza fedha mahali ambapo...

MAFUNZO HAYA YA OFISI YA WAZIRI MKUU YANAWAJENGEA UWEZO VIJANA KUPATA KIPATO

msumbanews.co.tz - 16/Feb 20:06

Na: Dk. Reubeni Lumbagala, Tanga.Moja ya changamoto kubwa inayoikabili dunia kwa sasa na Tanzania ikiwepo ni tatizo la ajira hasa kwa vijana. Nchini...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément