Naibu Waziri, Ofisi ya Rais- TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amemuelekeza Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Arusha...
Vous n'êtes pas connecté
OR-TAMISEMIOfisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imefanya mapitio ya bajeti kwa kuzingatia muundo wa kanda na gharama za maisha ili kuhakikisha fedha zinazotengwa kwa miradi ya ujenzi zinatosheleza kukamilisha miundombinu muhimu.Hivyo, kuanzia bajeti ya mwaka 2024/25, madarasa yatagharimu kati ya Sh.Milioni 22 hadi 25, huku ujenzi wa zahanati ukigharimu kati ya Sh.Milioni 284 hadi 358.Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba, ameliambia Bunge leo Februari 13, 2025 alipokuwa akichangia taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).Amesema hatua hiyo imetokana na serikali kubaini tofauti kubwa ya gharama za vifaa vya ujenzi kati ya kanda mbalimbali, hali iliyokuwa ikikwamisha utekelezaji wa miradi muhimu kama shule, zahanati na majengo ya utawala.“Tumefanya maboresho ya bajeti ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa viwango sahihi. Kuanzia bajeti ya mwaka 2024/2025, madarasa yatagharimu kati ya shilingi milioni 22 hadi 25, huku ujenzi wa zahanati ukigharimu kati ya shilingi milioni 284 hadi 358,” amesema Mhe. Katimba.Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC, Mhe. Halima Mdee, amesisitiza kuwa kuanzia mwaka wa fedha 2025/2026, taasisi zote za umma zinazotoa huduma katika Serikali za Mitaa zinapaswa kushirikiana katika kuandaa miundombinu muhimu kama barabara, umeme, na maji kabla ya kuanza miradi yoyote ya ujenzi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais- TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amemuelekeza Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Arusha...
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe Victoria Mwanziva anaendelea na ziara maalum ya kata kwa kata kwa malengo ya ukaguzi wa miradi sambamba na kusikiliza na...
Na Denis Chambi , Tanga.SERIKALI imeanza mchakato wa uboreshaji wa miundombinu ya Bomba la Tazama linalosafirisha mafuta kutoka Tanzania hadi...
📌 Anadi soko la mazao jamii ya mikunde India📌 Mnada mazao ya kunde mtandaoni waboresha biashara ya kimataifa📌 Biashara kati ya Tanzania na...
Na. Josephine Majura, WF - Dodoma Bunge limepitisha nyongeza ya mapato na matumizi ya jumla ya shilingi bilioni 945.7 kwa ajili ya kuongeza kwenye...
• Kamati ya Bunge Yataka Kampuni Zingine Kuiga Barrick📍 KahamaNaibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, amesema kuwa Kampuni ya Uchimbaji wa...
Na. Josephine Majura WF- Dodoma Serikali imeeleza kuwa masaa yanayotumiwa na Wabunge wenye sifa ya Mhasibu wa Umma aliyeidhinishwa (CPA), katika...
Na Oscar Assenga, HANDENI. RAIS Dkt Samia Suluhu amemuagiza Waziri wa Tamisemi Mohamed Mchengerwa kuhakikisha wanapeleka kiasi cha Milioni 240 kwa...
📌Aagiza wasimamiwe kwa karibu kumaliza miradi📌Awataka Watendaji TANESCO kuwa na mahusiano mazuri na wananchiNaibu Waziri wa Nishati, Mhe....
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imefanya mafunzo kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za...