X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 31/Aug 07:37

SERIKALI ITAENDELEA NA UJENZI WA KITUO CHA AFYA TARIME VIJIJINI.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Mhe. Dkt Festo Dugange amesema Serikali itaendelea na ujenzi wa kituo cha afya katika Kata ya Susuni iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ili kuwasogezea karibu huduma za afya Wananchi wa kata hiyo.Mhe. Dkt. Dugange amesema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma, katika kipindi cha Maswali na Majibu, wakati akijibu swali la Mbunge wa Tarime Vijijini Mhe. Mwita Waitara aliyeuliza Je, Ni lini Serikali itajenga kituo cha afya Kata ya Susuni Jimbo la Tarime Vijijini?Mhe. Dkt Dugange amesema Kata ya Susuni iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ina jumla ya Vijiji vitano (5) vya Matamankwe, Kiongera, Keroti, Kikomili na ⁠Nyabilongo. Kati ya vijiji hivyo, Vijiji viwili (2) vya Matamankwe na Kiongera vina zahanati, Kata haina Kituo cha Afya.Amesema Serikali imepanga kuipandisha hadhi Zahanati ya Kiongera kuwa kituo cha afya ambapo katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali imepeleka fedha shilingi Milioni 207 kwenye Zahanati ya Kiongera kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Wazazi lenye huduma ya upasuaji wa dharura na jengo la Maabara”.Sanjali na hayo Dkt. Dugange amesema Serikali itaendelea kutenga fedha katika bajeti mbalimbali zitakazotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini ili kukamilisha mradi huo wa ujenzi wa kituo cha afya katika Kata ya Susuni.“Katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri itatenga shilingi Milioni 150 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa miundombinu iliyosalia ikiwa ni pamoja na ujenzi wa jengo la kufulia, jengo la kuhudumia Wagonjwa wa nje (OPD) na jengo la Wodi ya kulaza Wagonjwa.” Dkt Dugange.

Articles similaires

WAZIRI CHANA " SERIKALI ITAWALINDA WANANCHI DHIDI YA WANYAMAPORI WAKALI"

msumbanews.co.tz - 06/Sep 17:20

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema Serikali itaendelea kuweka  mikakati madhubuti za kuwalinda wananchi...

WAZIRI CHANA " SERIKALI ITAWALINDA WANANCHI DHIDI YA WANYAMAPORI WAKALI"

msumbanews.co.tz - 06/Sep 17:20

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema Serikali itaendelea kuweka  mikakati madhubuti za kuwalinda wananchi...

PINDI CHANA AZINDUA ZAHANATI YA IVILIKINGE-MAKETE

msumbanews.co.tz - 04:19

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amezindua rasmi zahanati ya Ivilikinge...

DHAMIRA YA RAIS SAMIA NI KUONA WANANCHI WANANUFAIKA NA MIRADI KATIKA MAENEO YAO- KAPINGA

msumbanews.co.tz - 10/Sep 04:08

 Naibu Waziri Nishati, Mhe.  Judith Kapinga amesema kuwa dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni...

RC TANGA AAGIZA KUCHUKUA TAHADHARI YA UGONJWA WA HOMA YA NYANI.

msumbanews.co.tz - 10/Sep 09:42

 Na Denis Chambi, Tanga.MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani ameitaka Hospital ya rufaa ya mkoa  Bombo kuwa ya  mfano kwa kuchukua...

KAMATI YA BUNGE YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA FEDHA ZA MIRADI YA REGROW

msumbanews.co.tz - 08/Sep 05:38

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ikiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb)imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa...

DC Mpogolo aendelea na ziara ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi wa Jimbo la Ukonga

msumbanews.co.tz - 14/Sep 05:47

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo leo Septemba 12 ,2024 ameendelea na ziara ya kutatua kero za Wananchi wa Kata za Kitunda, Kivule, Mzinga...

Kamati ya Bunge yapongeza utekelezaji wa mradi wa SEQUIP-AEP

msumbanews.co.tz - 11/Sep 18:19

Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Michael Ng’umbi akitoa maelezo ya utekelezaji wa Mradi wa kuimarisha ubora wa elimu ya...

Wakazi wa Kata za Mnyamani, Buguruni na Vingunguti kuboreshewa huduma za kijamii

msumbanews.co.tz - 15/Sep 05:16

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewahakikishia wananchi wa Kata za Mnyamani,Vingunguti na Buguruni kuwa Serikali inaendelea kuboresha...

Wakazi wa Kata za Mnyamani, Buguruni na Vingunguti kuboreshewa huduma za kijamii

msumbanews.co.tz - 15/Sep 05:16

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewahakikishia wananchi wa Kata za Mnyamani,Vingunguti na Buguruni kuwa Serikali inaendelea kuboresha...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément