X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 08/Sep 05:38

KAMATI YA BUNGE YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA FEDHA ZA MIRADI YA REGROW

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ikiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb)imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajenda yake ya kukuza utalii ikiwemo katika miradi ya ujenzi wa kituo cha utalii kwa gharama ya shilingi bilioni 21.4 na kituo cha utafiti kwa shilingi bilioni 1.55 chini ya mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW), Kihesa Kilolo Mkoani Iringa.Ameyasema hayo leo Septemba 7, 2024 wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii katika miradi hiyo mkoani Iringa.“Kwa ujumla kama Kamati tunaendelea kuipongeza Serikali, kumpongeza Rais Samia kwa namna ambavyo anaendelea kusimamia na kutekeleza shughuli mbalimbali za nchi yetu ikiwemo ajenda yake kubwa ya kukuza utalii” amesisitiza Mhe. Mnzava.Amefafanua kuwa kamati imeishauri  Serikali kusimamia miradi hiyo ili ikamilike kwa ufanisi wa hali ya juu na kwa wakati ambapo kwa upande wa Kituo cha utafiti amesema sehemu kubwa ya kazi ya ujenzi wa kituo hicho inakwenda vizuri huku akimuelekeza mkandarasi wa ujenzi wa kituo cha utalii kutimiza wajibu wake ili kukamilisha kazi hiyo.Naye, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa fedha za miradi hiyo huku akisisitiza kuwa ni wajibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kusimamia miradi hiyo itekelezwe kwa wakati.Mhe. Chana ametoa rai kwa Wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kusimamia mikataba yao na kukamilisha miradi kwa wakati. “Nitoe angalizo kwa Wakandarasi walio kwenye miradi ya Wizara ya Maliasili na Utalii ni muhimu sana kutekeleza miradi kutokana na mikataba tuliyowekeana ili ikamilike kwa wakati” amesema.Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Malisili na Utaklii iko Mkoani Iringa kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa miradi iliyo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Articles similaires

KAMATI YA BUNGE YA MAJI NA MAZINGIRA YAIPONGEZA TANGA-UWASA

msumbanews.co.tz - 12/Sep 15:24

 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kiongizwa na mwenyekiti wake Mhe Jackson Kiswaga imetoa pongezi kwa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa...

KAMATI YA BUNGE YA MAJI NA MAZINGIRA YAIPONGEZA TANGA-UWASA

msumbanews.co.tz - 12/Sep 15:24

 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kiongizwa na mwenyekiti wake Mhe Jackson Kiswaga imetoa pongezi kwa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa...

DHAMIRA YA RAIS SAMIA NI KUONA WANANCHI WANANUFAIKA NA MIRADI KATIKA MAENEO YAO- KAPINGA

msumbanews.co.tz - 10/Sep 04:08

 Naibu Waziri Nishati, Mhe.  Judith Kapinga amesema kuwa dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni...

Kamati ya Bunge yapongeza utekelezaji wa mradi wa SEQUIP-AEP

msumbanews.co.tz - 11/Sep 18:19

Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Michael Ng’umbi akitoa maelezo ya utekelezaji wa Mradi wa kuimarisha ubora wa elimu ya...

KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA UWEKEZAJI KIWANDA CHA MKULAZI

msumbanews.co.tz - 09/Sep 06:59

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatuma Toufiq akizungumza wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua...

WAZIRI CHANA ATETA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA

msumbanews.co.tz - 06/Sep 05:00

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Benki ya Dunia ukiongozwa na...

WIZARA YA NISHATI ENDELEENI KUUSIMAMIA MRADI WA JNHPP IPASAVYO-KAMATI YA BUNGE

msumbanews.co.tz - 07/Sep 15:39

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeitaka Wizara ya Nishati kuendelea kuusimamia ipasavyo Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Julius Nyerere...

Kamati ya Bunge Yaipongeza UDSM kwa Maboresho ya Mitaala na Utekelezaji wa Mradi wa HEET

msumbanews.co.tz - 11/Sep 04:51

 KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepongeza juhudi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kuboresha mitaala yake ili kukidhi...

WAZIRI CHANA " SERIKALI ITAWALINDA WANANCHI DHIDI YA WANYAMAPORI WAKALI"

msumbanews.co.tz - 06/Sep 17:20

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema Serikali itaendelea kuweka  mikakati madhubuti za kuwalinda wananchi...

WAZIRI CHANA " SERIKALI ITAWALINDA WANANCHI DHIDI YA WANYAMAPORI WAKALI"

msumbanews.co.tz - 06/Sep 17:20

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema Serikali itaendelea kuweka  mikakati madhubuti za kuwalinda wananchi...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément