X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 07/Sep 15:39

WIZARA YA NISHATI ENDELEENI KUUSIMAMIA MRADI WA JNHPP IPASAVYO-KAMATI YA BUNGE

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeitaka Wizara ya Nishati kuendelea kuusimamia ipasavyo Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Julius Nyerere (JNHPP) ili ukamilike kwa wakati. Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Kirumbe Ng'enda leo Septemba 07, 2024 wakati wa ziara ya kukagua hatua za utekelezaji wa mradi huo ambao utaingiza megawati 2,115 mara baada ya kukamilika."Wizara iendelee kusimamia kwa umakini mradi huu ili mashine zote Tisa ziweze kukamilika kama ilivyopangwa." Amesema Mhe. Ng'endaAidha, kamati hiyo imeipongeza Serikali kwa kuhakikisha mashine zilizosalia zinaendelea kukamilika na kufanya kazi ambapo hadi sasa zimekamilika mashine tatu ambazo zinazalisha kiasi cha megawati 705 na mashine namba sita ipo kwenye hatua za mwisho  kukamilishwa.Kwa upande wake Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Wizara ya Nishati imekuwa ikifanya kazi kwa ushirikiano na kamati hiyo ya Bunge ikiwa ni pamoja na kupokea maelekezo, ushauri na mapendekezo ya Kamati."Kazi kubwa ya Kamati ni kutusimamia sisi Serikali, na sisi tunahakikisha kuwa maelekezo yenu yote yanatekelezwa na mafanikio yake yanaonekana katika miradi mbalimbali kama JNHPP ambao utekelezaji wa mradi wake umefikia asilimia 98." Amesema KapingaAmeongeza kuwa, Wizara  ya Nishati chini ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,  Mhe. Dkt. Doto Biteko itaendelea kuusimamia mradi huo ila ukamilike kwa wakati.Ameeleza kuwa, Mkandarasi wa mradi ameshalipwa takriba shilingi trilioni 6.3 kati ya shilingi trillioni 6.5 zinazopaswa kulipwa.

Articles similaires

KAMATI YA BUNGE YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA FEDHA ZA MIRADI YA REGROW

msumbanews.co.tz - 08/Sep 05:38

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ikiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb)imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa...

KAMATI YA BUNGE YA MAJI NA MAZINGIRA YAIPONGEZA TANGA-UWASA

msumbanews.co.tz - 12/Sep 15:24

 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kiongizwa na mwenyekiti wake Mhe Jackson Kiswaga imetoa pongezi kwa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa...

KAMATI YA BUNGE YA MAJI NA MAZINGIRA YAIPONGEZA TANGA-UWASA

msumbanews.co.tz - 12/Sep 15:24

 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kiongizwa na mwenyekiti wake Mhe Jackson Kiswaga imetoa pongezi kwa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa...

DHAMIRA YA RAIS SAMIA NI KUONA WANANCHI WANANUFAIKA NA MIRADI KATIKA MAENEO YAO- KAPINGA

msumbanews.co.tz - 10/Sep 04:08

 Naibu Waziri Nishati, Mhe.  Judith Kapinga amesema kuwa dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni...

KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA UWEKEZAJI KIWANDA CHA MKULAZI

msumbanews.co.tz - 09/Sep 06:59

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatuma Toufiq akizungumza wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua...

SERIKALI KUVUTIA WAWEKEZAJI UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI- DKT. BITEKO

msumbanews.co.tz - 10/Sep 16:13

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali itaendelea kuvutia wawekezaji katika tafiti na uchimbaji wa mafuta na...

Kamati ya Bunge Yaipongeza UDSM kwa Maboresho ya Mitaala na Utekelezaji wa Mradi wa HEET

msumbanews.co.tz - 11/Sep 04:51

 KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepongeza juhudi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kuboresha mitaala yake ili kukidhi...

Kamati ya Bunge yapongeza utekelezaji wa mradi wa SEQUIP-AEP

msumbanews.co.tz - 11/Sep 18:19

Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Michael Ng’umbi akitoa maelezo ya utekelezaji wa Mradi wa kuimarisha ubora wa elimu ya...

KAMATI ZA MAAFA WILAYA ZATAKIWA KUWEKA MIPANGO YA DHARURA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 08:04

Serikali imezitaka Kamati za Usimamizi wa Maafa Ngazi ya Wilaya kuhakikisha zinajiandaa kikamilifu na kuweka mpango wa dharula wa utendaji na uratibu...

KAMATI ZA MAAFA WILAYA ZATAKIWA KUWEKA MIPANGO YA DHARURA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 08:04

Serikali imezitaka Kamati za Usimamizi wa Maafa Ngazi ya Wilaya kuhakikisha zinajiandaa kikamilifu na kuweka mpango wa dharula wa utendaji na uratibu...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément