X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 06/Sep 17:10

DKT. KIRUSWA AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUMTUMBUA ALIYEKUWA DC LONGIDO

 Mbunge wa Jimbo la Longido Mkoani Arusha ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Lemomo Kiruswa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo Marko Ng'umbi.Dkt. Kiruswa amesema kuwa Wilaya ya Longido imepata heshima kubwa kutoka kwa Rais Dkt. Samia kumtengua aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo ambaye alidhalilisha uongozi wa Wilaya kuanzia viongozi wa mila,Chama pamoja na Watumishi wa Halmashauri kwani aliwaburuza vibaya na walimvumilia nakumlea kwani jamii ya kimaasai inausikivu mkubwa na inapenda sana amani,nidhamu na hekima."Ila kwa kauli zake mwenyewe kaja kukitukana Chama cha Mapinduzi na Serikali kwamba ilibeba uchaguzi wa mkuu 2020 jambo ambalo sio la kweli kabisa,Wilaya hii ni ngome ya CCM na imetamalaki tangu mzee Lekule alipoanzisha wilaya hii watu wote wanashinda kwa haki na kwa kufuata utaratibu katika wilaya hii"Ameongezea KiruswaKwa upande wake Mkuu mpya wa Wilaya ya Longido Salum Kali akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kilimahewa Kata ya Mundarara amesema amejipanga kuwatumikia wananchi na kwamba namba yake ya simu anayogawa kwa wananchi itapatikana saa 24,na kwamba muda wote wamwambie kero na atawafikia."Naomba niwahakikishie wilaya yenu ipo salama.Kero zenu nimezisikia suala la daraja Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) watakuja,pia mmesema kuna shida ya zahanati na kituo,"amesema.Nitapita kijiji kwa kijiji,serikali inapaswa iwepo itatue kero zenu,mmesema mnashida ya malisho mimi ni mwakilishi wa Rais Samia Suluhu Hassan, nitahakikisha nasimamia vizuri na kutatua kila kero,ni wajibu wetu kama viongozi wa serikali.Akizungumza katika Mkutano wa hadhara katika Kata ya Mundarara Katibu wa NEC,Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa CCM,Amos Makalla,amewaomba radhi wanachi wa Longido kwa kauli ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido, Marco Ng'umbi kwamba zililenga kuwachonganisha kwani Chama cha Mapinduzi kinaheshimu uchaguzi wa haki na kushinda kwenye sanduku la kura na sio vinginevyo"Yale maneno yameshapita,zile zilikuwa kauli zake yeye,sijui alienda porini kufanya nini kama alienda kutafuta shamba au kuchimba dawa anajua yeye,"amesema.Amesema CCM inajivunia utekelezaji wa Ilani ya CCM,hatuhitaji mbeleko,hapa ni ngome yetu hivyo hakukua na sababu za kutofuata misingi ya uchaguzi.

Articles similaires

WANANCHI LONGIDO WATAKA SHULE ZA BWENI KUIMARISHWA ULINZI

msumbanews.co.tz - 07/Sep 11:12

Wananchi wa Wilaya ya Longido Mkoani Arusha wameiomba serikali kujengea uzio shule zote za serikali za bweni zilizopo katika wilaya hiyo lengo ni...

Dc Ilala awataka Viongozi wa Matawi, Mashina, Mitaa na Kata kutimiza majukumu yao kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

msumbanews.co.tz - 15/Sep 05:19

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala  Mhe. Edward Mpogolo amewataka Viongozi wa Matawi, Mashina, Mitaa na Kata  Kutimiza Majukumu yao kuelekea Uchaguzi wa...

SILAA WATAKA WANA CCM UKONGA KUNADI MAENDELEO YA RAIS DKT. SAMIA

msumbanews.co.tz - 10/Sep 06:04

Mbunge wa Jimbo la Ukonga ambaye pia ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry Silaa amewataka wanachama wa Chama cha...

WAZIRI JAFO ATAKA WANANCHI KUACHA KUCHANGANYA MAZAO

msumbanews.co.tz - 10:06

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama wakitembelea na kukagua Ghala la Mpako...

KAMATI ZA MAAFA WILAYA ZATAKIWA KUWEKA MIPANGO YA DHARURA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 08:04

Serikali imezitaka Kamati za Usimamizi wa Maafa Ngazi ya Wilaya kuhakikisha zinajiandaa kikamilifu na kuweka mpango wa dharula wa utendaji na uratibu...

KAMATI ZA MAAFA WILAYA ZATAKIWA KUWEKA MIPANGO YA DHARURA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 08:04

Serikali imezitaka Kamati za Usimamizi wa Maafa Ngazi ya Wilaya kuhakikisha zinajiandaa kikamilifu na kuweka mpango wa dharula wa utendaji na uratibu...

Dc Mpogolo awahakikishia Wakazi wa Mtaa wa Kipunguni kulipwa fidia zao

msumbanews.co.tz - 14/Sep 05:34

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewahakikishia wakazi wa Mtaa wa Kipunguni kata ya Kipawa waliopisha ujenzi wa uwanja wa Ndege wa...

POLISI WAPIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA CHADEMA ,CCM WALAANI UTEKAJI

msumbanews.co.tz - 14/Sep 05:02

Jeshi la polisi nchini Tanzania limepiga marufuku maandamano yaliyokuwa yamepangwa na chama cha upinzani Chadema kufanyika jijini Dar es Salaam tarehe...

NGORONGORO WANAIPENDA CCM NA NI NGOME YA CCM

msumbanews.co.tz - 07/Sep 07:46

 KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla, amesema Ngorongoro ni ngome ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hakuna chama...

DC Mpogolo aendelea na ziara ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi wa Jimbo la Ukonga

msumbanews.co.tz - 14/Sep 05:47

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo leo Septemba 12 ,2024 ameendelea na ziara ya kutatua kero za Wananchi wa Kata za Kitunda, Kivule, Mzinga...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément