X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 10/Sep 10:08

Tanga kujenga Maktaba ya Kisasa Kumuenzi Sheikh Shaaban Robert.

Na Denis Chambi,  Tanga.MKUU wa wilaya ya Tanga Japhari Kubecha amesema kuwa  Serikali kwa kushirikiana na wadau pamoja na familiya ya aliyekuwa mtunzi wa vitabu hapa nchini Sheikh Shaaban Robert watajenga maktaba ya kisasa  kutunza kumbukumbu zake pamoja na kufanya tamasha maalum kila mwaka ili kumuenzi kwa kazi nzuri ambazo alizifanya ikiwa ni pamoja na kuinadi Lugha ya Kiswahili.Kubecha ameeleza hayo September 8,2024 mara baada ya kutembelea kaburi lake na  kushiriki dua maalum ya kumwombea pamoja na kuitembelea familiya yake iliyopo katika Kijiji cha Vibandani Kata ya Masiwani jijini Tanga ambapo amesema kuwa kama mzawa ambaye aliitangaza wilaya hiyo pamoja na Mkoa kwa ujumla kupitia kazi zake jamii haina budi kuendelea kurithishwa  na kumkumbuka kwa kazi ambazo alizifanya."Leo tumeshauriana na familiya  tujipange kuona namna ambavyo tunaweza kumuenzi Shaaban Robert  kikamilifu bado hatujapata nafasi nzuri ya kumuenzi kama wana Tanga kwa sababu yako mambo makubwa ameyafanga ikiwemo kutumia vipawa vyake  kutangaza na kuinadi Lugha yetu adhimu ya Kiswahili yapo mambo nimewaomba kama familiya wayaangalie na kuyaratibu na yale yanayotuhusu sisi kama Serikali tutakuwa tayari kuyafanya " alisema Kubecha."Nimepita kuona alipozikwa yeye na watoto wake nimeiona pia maktaba hii ambayo aliichorea wafadhili ambayo sasa ni chakavu na kwa kweli imepoteza ule ubora wake sasa tunakwenda  kukaa kama Serikali kwa kushirikiana na wadau tuone ni kwa namna gani tutakwenda kuijenga maktaba ya kisasa lakini kuweka mkakati wa kuwa na kumbukizi angalau kila mwaka tutakuwa tunafanya tamasha la kumuenzi Sheikh Shaban Robert katika eneo hili ambalo aliishi""Sisi kama Serikali ya wilaya ya Tanga tunaahidi  kushirikiana na familiya pamoja na wadau kuendelea kuenzi mambo yote mazuri ambayo Sheikh Shaban Robert aliyafanya na hasa kukuza Lugha ya Kiswahili unapotaja vinara wa Lugha yetu adhimu ya Kiswahili huwezi kuacha kumtaja Sheikh Shaaban Robert, Lugha yetu ameipambanua duniani na wapo watu wamekuwa ma Profesa , ma Daktari wa falsafa kupitia  kupitia vitabu vya Sheikh Shaaban Robert kwa hiyo tuna kila sababu ya kumuenzi kama Mwana Tanga kwa sababu aliitangaza wilaya yetu na Mkoa wetu kwa ujumla" alisema Mkuu huyo wa wilaya. Akizungumza kwa niaba ya familiya mjukumu wa Marehemu Sheikh Shaaban Robert, Mustafa Akili  ameishukuru Serikali ya wilaya ya Tanga kwa kuja na wazo la kumuenzi  Babu yao ambaye pamoja na kuwa kielelezo cha familiya ameitambulisha kitaifa na kimataifa ."Tunashukuru kuhusu suala la Maktaba tumeshalifikisha kwa Mkuu wa wilaya natumaini kwamba watalifanyia kazi tutakaa kama familiya na kupanga kwa kushirikiana na Serikali tuone jinsia ya kumuenzi Babu yetu"Sheikh Shaaban Robert ambaye alizaliwa mwaka 1909  katika Kijiji cha Vibandani kata ya Masiwani halmashauri ya Jiji la Tanga alifariki mwaka 1962 kwa tatizo la upungufu wa damu mwilini . Vizazi na vizazi hususani watanzania wanaendelea kumkumbuka kupitia kazi zake za utunzi wa vitabu vya Tamthiliya na Riwaya mbalimbali zikiwemo  Kusadikika, Kufikirika , Adili na nduguze , ,Mwafrika aimba ,Almas za Afrika, Pambo la Lugha , Utu bora mkulima, Mithali na mifano ya mkulima na nyinginezo 

Articles similaires

Tanga kujenga Maktaba ya Kisasa Kumuenzi Sheikh Shaaban Robert.

msumbanews.co.tz - 10/Sep 10:08

Na Denis Chambi,  Tanga.MKUU wa wilaya ya Tanga Japhari Kubecha amesema kuwa  Serikali kwa kushirikiana na wadau pamoja na familiya ya aliyekuwa...

Familiya ya King Majuto yaomba Umeme , Maji kumuenzi baba yao.

msumbanews.co.tz - 10/Sep 10:13

 Na Denis Chambi Tanga Familiya ya aliyekuwa mwigizaji maarufu hapa nchini Alhaji Amri Athumani  'King Majuto'   imeiomba Serikali kuwafikishia ...

Familiya ya King Majuto yaomba Umeme , Maji kumuenzi baba yao.

msumbanews.co.tz - 10/Sep 10:13

 Na Denis Chambi Tanga Familiya ya aliyekuwa mwigizaji maarufu hapa nchini Alhaji Amri Athumani  'King Majuto'   imeiomba Serikali kuwafikishia ...

RAIS SAMIA ANAAMINI KATIKA USHIRIKIANO NA VIONGOZI WA DINI -DKT. BITEKO

msumbanews.co.tz - 17/Sep 14:00

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na viongozi wa dini ili kuwawezesha kutimiza...

KAMATI ZA MAAFA WILAYA ZATAKIWA KUWEKA MIPANGO YA DHARURA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 08:04

Serikali imezitaka Kamati za Usimamizi wa Maafa Ngazi ya Wilaya kuhakikisha zinajiandaa kikamilifu na kuweka mpango wa dharula wa utendaji na uratibu...

KAMATI ZA MAAFA WILAYA ZATAKIWA KUWEKA MIPANGO YA DHARURA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 08:04

Serikali imezitaka Kamati za Usimamizi wa Maafa Ngazi ya Wilaya kuhakikisha zinajiandaa kikamilifu na kuweka mpango wa dharula wa utendaji na uratibu...

RC TANGA AAGIZA KUCHUKUA TAHADHARI YA UGONJWA WA HOMA YA NYANI.

msumbanews.co.tz - 10/Sep 09:42

 Na Denis Chambi, Tanga.MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani ameitaka Hospital ya rufaa ya mkoa  Bombo kuwa ya  mfano kwa kuchukua...

WAZEE TUNDURU WAOIMBA SERIKALI KUFUNGUA SOKO JIPYA LA MADINI YA VITO

msumbanews.co.tz - 12/Sep 07:54

Baadhi ya majengo katika soko jipya la madini ya vito yanayoendelea kujengwa na Halmashauri ya wilaya Tunduru kwa kushirikiana na wadau wa madini...

WMA YAHIMIZA USHIRIKIANO KUTOKA SEKTA BINAFSI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 08:08

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...

WMA YAHIMIZA USHIRIKIANO KUTOKA SEKTA BINAFSI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 08:08

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément