X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 12/Sep 07:52

WIZARA YA FEDHA YAKEMEA MIKOPO HOLELA YA MITAANI INAYODHALILISHA WATANZANIA

 Na Mwamvua Mwinyi,KibahaWIZARA ya fedha imetoa rai kwa Watanzania hususan makundi ya akinamama na wajasiriamali kujiepusha na mikopo ya udhalilishaji isiyo rasmi na badala yake watumie Taasisi zilizosajiliwa na kutambulika ili kulinda fedha zao.Aidha imekemea Taasisi zinazotoa huduma za mikopo ambazo hazijasajiliwa kufuata sheria za usajili na kupata leseni ili kuondoa migongano isiyo ya Lazima.Akitoa elimu ya fedha kwa wananchi wa Kibaha, katika ukumbi mkubwa wa mikutano Halmashauri ya Kibaha septemba 11,2024 ,Ofisa Usimamizi wa fedha kutoka Wizara ya Fedha Stanley Kibakaya alieleza utoaji elimu hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alilolitoa baada ya baadhi ya wananchi kulalamikia watoa huduma kutoa riba kubwa."Utekelezaji huu ni agizo la Rais wetu ambalo aliagiza Wizara ya Fedha kupita kwa watanzania kutoa elimu ya fedha,mikopo rafiki isiyo ya udhalilishaji na kueleza umuhimu kutumia Taasisi zinazotambulika kisheria zilizosajiliwa ikiwemo UTT-Amis,Benki na Sacco's."alifafanua Kibakaya.Alieleza utekelezaji wa mpango huo ni wa miaka kumi (10)ambapo utakamilika 2030 na hadi sasa wameshatoa elimu katika mikoa 13 ikiwa ni pamoja na Pwani na Morogoro."Kipengele cha pili ni Wizara ya Fedha kushirikiana na Taasisi za kifedha kufikia watanzania ambapo lengo ni kufikia watanzania asilimia 80 ifikapo 2025" aliongeza kusema Kibakaya.Ramadhani Myonga Ofisa Sheria Mwandamizi na Mtatuzi wa malalamiko ya wateja wa Taasisi za fedha (Benki Kuu ya Tanzania) aliwataka wananchi kuwa na usimamizi mzuri wa fedha Binafsi ili fedha wanayopata iongeze thamani.Vilevile aliwaasa kujenga tabia na tamaduni ya kuwa na vyanzo vya mapato vilivyoendelevu ."Oya ,Kausha Damu sio mikopo rasmi kupitia elimu hii leo badilikeni mkawe mabalozi kutambua Taasisi zilizosajiliwa na kwenda kujiunga nazo kwa ajili ya usalama wa fedha zenu"alieleza Myonga.Awali Ofisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi kutoka UTT-AMIS, Rahim Mwanga, alitoa rai kwa washiriki kuwa na tabia ya kuweka akiba kwa faida yao badala ya kutumia kwa matumizi yasiyo sahihi.Aliwataka wanapokopa watunze kumbukumbu na kufuatilia mikataba kwa Taasisi zinazotoa huduma za mikopo.Mkazi wa Sofu Anna Mwakihaba ,aliishukuru Wizara ya Fedha kwa kuwapa elimu hiyo kwani awali walikuwa hawana uelewa wa masuala ya fedha na mikopo.

Articles similaires

WATANZANIA ASILIMIA 80 KUFIKIWA NA ELIMU YA FEDHA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 05:24

 Na. Saidina Msangi, Kibaha, Pwani.Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau na Taasisi zilizo chini yake imejipanga kutoa elimu ya fedha kwa...

Kamati ya Bunge yapongeza utekelezaji wa mradi wa SEQUIP-AEP

msumbanews.co.tz - 11/Sep 18:19

Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Michael Ng’umbi akitoa maelezo ya utekelezaji wa Mradi wa kuimarisha ubora wa elimu ya...

DKT. BITEKO ASISITIZA MAADILI, WELEDI NA UWAJIBIKAJI KATIKA UNUNUZI WA UMMA

msumbanews.co.tz - 09/Sep 13:54

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezitaka Mamlaka za Udhibiti na Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki kuzingatia weledi,...

WIZARA YA FEDHA YATOA MAFUNZO KWA MAAFISA UNUNUZI WA TAASISI ZA UMMA.

msumbanews.co.tz - 06/Sep 04:51

 Na Chedaiwe Msuya, WF.Wizara ya Fedha inaendelea kutoa mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta...

WANANCHI BAGAMOYO WAPOKEA ELIMU YA FEDHA

msumbanews.co.tz - 09/Sep 07:12

 Na. Saidina Msangi, WF, Bagamoyo, Pwani.Watumishi na wananchi wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, wameishukuru Serikali kwa kuwapa mafunzo ya elimu...

WANANCHI CHALINZE WAJIPANGA KUWEKEZA

msumbanews.co.tz - 07/Sep 07:41

 Na. Saidina Msangi, Chalinze, Pwani.Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze wameishukuru Serikali kwa kuwafikishia elimu ya fedha...

DKT. BITEKO AHIMIZA WANAWAKE KUTUMIA MIFUKO YA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

msumbanews.co.tz - 14/Sep 13:14

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanawake nchini kutumia fursa ya mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi...

ELIMU YA FEDHA YAWAFIKIA WANANCHI WA MKURANGA

msumbanews.co.tz - 11/Sep 05:10

 Na. Saidina Msangi, Mkuranga Pwani.Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, imewasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kwa...

DC Mpogolo aendelea na ziara ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi wa Jimbo la Ukonga

msumbanews.co.tz - 14/Sep 05:47

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo leo Septemba 12 ,2024 ameendelea na ziara ya kutatua kero za Wananchi wa Kata za Kitunda, Kivule, Mzinga...

REA YAENDELEA KUTEKELEZA DHAMIRA YA RAIS SAMIA KWA VITENDO

msumbanews.co.tz - 09/Sep 07:03

Na Mohamed SaifWakala wa Nishati Vijijini (REA) umeanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément