X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 06/Sep 04:51

WIZARA YA FEDHA YATOA MAFUNZO KWA MAAFISA UNUNUZI WA TAASISI ZA UMMA.

 Na Chedaiwe Msuya, WF.Wizara ya Fedha inaendelea kutoa mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu kwa Maafisa Ununuzi wa Taasisi za Umma ili kuhakikisha wana uelewa wa kutosha kuhusu Sheria mpya ya Ununuzi wa Umma Sura namba 410.Mafunzo haya yanakusudia kuongeza uwajibikaji na ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini. Maafisa Ununuzi wametakiwa kuzingatia sheria hiyo ili kuepuka ukiukwaji wa taratibu na kuhakikisha kwamba miradi yote ya umma inatekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia thamani ya pesa.Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Mbeya, Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Pascal Manono, alisisitiza umuhimu wa maafisa kuwa na weledi wa Sheria hiyo mpya. Mafunzo yalihusisha Wakuu wa Vitengo vya Usimamizi na Ununuzi, Ugavi na Wakuu wa Idara za Mipango kutoka Mikoa ya Njombe, Mbeya, Songwe, na Rukwa. “Sheria ya Ununuzi ya mwaka huu imeweka mkazo maalum kwa makundi maalumu kama watu wenye ulemavu, na kuwapa fursa ya kushiriki katika zabuni za umma kwa kufuata miongozo iliyowekwa.”alisema Bw. Manono.Katika mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Frola Tenga, alieleza kuwa Sheria hiyo mpya inatoa upendeleo kwa kampuni na wataalamu wa ndani ili kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki katika miradi ya kimkakati ya Serikali. “Lengo ni kuzisaidia kampuni ya ndani kukua na kushiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi kwa kushiriki katika zabuni za umma. Hii itaziwezesha kampuni za ndani kukuza kipato chao na kushindana kikamilifu katika soko la ndani na la kimataifa”. alisema Bi. TengaWashiriki wa mafunzo hayo walitoa maoni yao kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma kuendelea kusimamia Sheria na kutoa miongozo kwa viongozi wa juu ili kuepuka uvunjifu wa sheria na kanuni zilizowekwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Walisema kuwa ni muhimu kwa viongozi wa taasisi za umma kufuata mfumo rasmi wa ununuzi ili kuepuka ukiukwaji wa sheria ambao unaweza kuleta athari kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.Katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mgeni Rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Rodrick Mpogolo, aliwataka Maafisa Mipango kutumia takwimu rasmi na sahihi wakati wa kupanga mipango ya maendeleo. Alisisitiza kuwa matumizi sahihi ya takwimu ni muhimu katika kuhakikisha mipango inayowekwa inakidhi mahitaji halisi ya wananchi na kusaidia kukuza uchumi unaoendana na hali halisi ya wananchi.Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Bw. Rodrick Mpogole, akizungumza wakati wa Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi na Wakuu wa Maafisa Mipango wa Halmashauri za Mbeya, Songwe, Njombe, Rukwa kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Flora Tenga akizungumza wakati wa Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi na Wakuu wa Maafisa Mipango  wa Halmashauri za Mbeya, Songwe, Njombe, Rukwa kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.Meneja wa Kanda wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma- PPRA, Pascal Manono akizungumza wakati wa Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi na Wakuu wa Maafisa Mipango  wa Halmashauri za Mbeya, Songwe, Njombe, Rukwa kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.Baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi na Wakuu wa Maafisa Mipango wa Halmashauri za Mbeya, Songwe, Njombe, Rukwa  wakiwa kwenye mafunzo ya Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Articles similaires

MAAFISA UNUNUZI WA UMMA WAASWA KUFUATA SHERIA.

msumbanews.co.tz - 05/Sep 06:14

 Na Asia Singano, WF- KilimanjaroMaafisa Ununuzi wa Umma nchini wametakiwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za Ununuzi wa Umma ili kufikia malengo...

WATAALAMU WA UNUNUZI NA MIPANGO WAAHIDI KUCHAPA KAZI KWA VITENDO

msumbanews.co.tz - 07/Sep 11:58

 Na: Josephine Majura, WF, MwanzaWakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango wameahidi kwenda kutekeleza kwa vitendo yote waliyojifunza...

WIZARA YA FEDHA IMEHITIMISHA KUTOA MAFUNZO YA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA KANDA YA KUSINI

msumbanews.co.tz - 07/Sep 11:55

 Na Chedaiwe Msuya,WFWizara  ya Fedha imehitimisha utoaji wa mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi kwa Umma  katika mikoa ya Mtwara, Lindi na...

Naibu waziri Mkuu Amewataka Maafisa manunuzi na ugavi nchini kufanya kazi Kwa uadilifu ,uwajibikaji na uwazi

msumbanews.co.tz - 10/Sep 18:08

NAIBU waziri mkuu Dk Dotto Biteko amewataka maafisa manunuzi na ugavi nchini kufanya kazi zao Kwa uadilifu ,uwajibikaji uwazi na maadili katika...

WMA YAHIMIZA USHIRIKIANO KUTOKA SEKTA BINAFSI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 08:08

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...

WMA YAHIMIZA USHIRIKIANO KUTOKA SEKTA BINAFSI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 08:08

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...

DKT. BITEKO ASISITIZA MAADILI, WELEDI NA UWAJIBIKAJI KATIKA UNUNUZI WA UMMA

msumbanews.co.tz - 09/Sep 13:54

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezitaka Mamlaka za Udhibiti na Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki kuzingatia weledi,...

WAZIRI JAFO: WIZI WA KUCHEZEA VIPIMO NI KOSA KISHERIA

msumbanews.co.tz - 12/Sep 07:50

 WAZIRI  wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo amehimiza wananchi jijini Mwanza kuzingatia matumizi sahihi ya vipimo kila mara wanapofanya...

WMA, TAKUKURU WATEKELEZA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA

msumbanews.co.tz - 09/Sep 07:07

 Na Veronica Simba, WMA DodomaWakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Dodoma imetoa elimu ya vipimo kwa Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa...

ELIMU YA FEDHA YAWAFIKIA WANANCHI WA MKURANGA

msumbanews.co.tz - 11/Sep 05:10

 Na. Saidina Msangi, Mkuranga Pwani.Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, imewasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kwa...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément