X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 10/Sep 18:08

Naibu waziri Mkuu Amewataka Maafisa manunuzi na ugavi nchini kufanya kazi Kwa uadilifu ,uwajibikaji na uwazi

NAIBU waziri mkuu Dk Dotto Biteko amewataka maafisa manunuzi na ugavi nchini kufanya kazi zao Kwa uadilifu ,uwajibikaji uwazi na maadili katika utendaji wa kazi na kuepuka vitendo vya rushwa Ili kuonyesha thamani halisi ya matumizi ya fedha za ummaDk Biteko ameyasema hayo Leo wakati akimuwakilisha Rais Samia Suluhu katika ufunguzi wa Jukwaa la 16 la Ununuzi wa Umma kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambapo amesema serikali ya Tanzania imeonesha dhamira yake ya kuimarisha na kuboresha mfumo wa ununuzi wa umma kupitia teknolojia ya kidigitali.Aidha alisisitiza umuhimu wa maboresho yaliyofanywa katika sekta ya ununuzi wa umma nchini Tanzania ambapo aliishukuru Wizara ya Fedha pamoja na mamlaka nyingine husika kwa kazi kubwa waliyofanya katika kuboresha usimamizi wa ununuzi wa umma, hasa kwa kuanzisha mfumo mpya wa kielektroniki unaoitwa National e-Procurement System of Tanzania (NeST).Alibainisha kuwa Mfumo huu umekuwa msaada mkubwa katika kuongeza uwazi, uwajibikaji, na ufanisi katika matumizi ya fedha za umma, hasa kwenye miradi ya ununuzi, Katika mfumo wa NeST, taratibu za ununuzi zimeboreshwa na gharama za uendeshaji zimepungua kwa kiasi kikubwa.Alifafanua kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikiboresha sheria za ununuzi wa umma kwa lengo la kuongeza thamani ya fedha na kupambana na ubadhirifu wa mali za umma huku alikifafanua kuwa Kwa kupitia maboresho ya sheria ya ununuzi ya mwaka 2023, Serikali imeweka mikakati madhubuti kuhakikisha kuwa taasisi zote za umma zinatumia mfumo wa kielektroniki wa ununuzi wa umma.Kuhusu maendeleo ya ushirikiano wa Afrika Mashariki, aliwataka washiriki wa Jukwaa hili kuhakikisha wanaboresha mifumo yao ya ununuzi wa umma kwa kutumia teknolojia za kisasa ili kuleta tija na ufanisi zaidi huku Akisisitiza kuwa ununuzi endelevu ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii, na kimazingira, hivyo mifumo ya kidigitali inapaswa kuchochea maendeleo haya.Aidha alitoa wito kwa taasisi zote za umma kuhakikisha zinatumia mfumo wa NeST, huku akisisitiza kwamba taasisi zote zitakazokaidi maagizo haya zitaadhibiwa ,aliwataka washiriki wa jukwaa hili kuhakikisha kuwa wanakuza viwango vya kikanda vya ununuzi endelevu ambavyo vitaimarisha usawa wa kijamii, ukuaji wa uchumi, na uendelevu wa mazingira.Kwa upande wake 00 alisema Kongamano la mwaka huu linaongozwa na kauli mbiu isemayo "matumizi ya mifumo ya kidigitali Kwa ununuzi wa umma endelevu"ilikuhakikisha kunakuwa na ufanisi na tija katika manunuzi ya umma serikali ilianza maamuzi ya Kutumia mifumo ya kieletroniki katika ununuzi wa umma nchini kwetuAlisema mpaka Sasa mifumo miwili imekamilika na mmoja unaendeleaje na inafanya kazi Kwa ufanisi na hadi kufikia agosti 31 ,2024 jumla ya taasisi nunuzi 1151 ziliweza kuhuisha taarifa zao na kuanza Kutumia mifumo jumla ya taasisi nunuzi 1048 zilitangaza mipango ya ununuzi ya mwaka.Kwa upande wake mkurugenzi wa PPRA Denisi Simba alisema kuwa katika jukwaa hilo washiriki watapata fursa ya kubadilishana uzoefu wa namna teknolojia inavyoweza kuleta mabadiliko katika sekta ya ununuzi .

Articles similaires

DKT. BITEKO ASISITIZA MAADILI, WELEDI NA UWAJIBIKAJI KATIKA UNUNUZI WA UMMA

msumbanews.co.tz - 09/Sep 13:54

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezitaka Mamlaka za Udhibiti na Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki kuzingatia weledi,...

WIZARA YA FEDHA YATOA MAFUNZO KWA MAAFISA UNUNUZI WA TAASISI ZA UMMA.

msumbanews.co.tz - 06/Sep 04:51

 Na Chedaiwe Msuya, WF.Wizara ya Fedha inaendelea kutoa mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta...

WATAALAMU WA UNUNUZI NA MIPANGO WAAHIDI KUCHAPA KAZI KWA VITENDO

msumbanews.co.tz - 07/Sep 11:58

 Na: Josephine Majura, WF, MwanzaWakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango wameahidi kwenda kutekeleza kwa vitendo yote waliyojifunza...

WMA YAHIMIZA USHIRIKIANO KUTOKA SEKTA BINAFSI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 08:08

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...

WMA YAHIMIZA USHIRIKIANO KUTOKA SEKTA BINAFSI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 08:08

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...

MAAFISA UNUNUZI WA UMMA WAASWA KUFUATA SHERIA.

msumbanews.co.tz - 05/Sep 06:14

 Na Asia Singano, WF- KilimanjaroMaafisa Ununuzi wa Umma nchini wametakiwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za Ununuzi wa Umma ili kufikia malengo...

TANZANIA YAWEKEZA KIMKAKATI KATIKA SEKTA YA TEHAMA ILI KUKUZA UCHUMI WA KIDIJITALI

msumbanews.co.tz - 08:01

Tanzania ina mifumo kadhaa ya kisheria na udhibiti inayoongoza sekta ya mawasiliano na TEHAMA ili kuhakikisha huduma ya intaneti ya kasi inawafikia...

UGONJWA WA FMD WAJADILIWA KUTOVUKA MIPAKA YA NCHI ZA EAC NA SADC

msumbanews.co.tz - 10/Sep 17:36

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Abdul Mhinte akizungumza jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mkutano wa wataalamu kutoka...

WIZARA YA FEDHA IMEHITIMISHA KUTOA MAFUNZO YA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA KANDA YA KUSINI

msumbanews.co.tz - 07/Sep 11:55

 Na Chedaiwe Msuya,WFWizara  ya Fedha imehitimisha utoaji wa mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi kwa Umma  katika mikoa ya Mtwara, Lindi na...

SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KUHUSU SUALA LA UHABA WA FEDHA ZA KIGENI

msumbanews.co.tz - 07/Sep 07:35

 Na. Joseph Mahumi na Peter Haule, WF, DodomaSerikali imesema inaendelea kuweka mikakati na mbinu mbalimbali za muda mfupi, wa kati na mrefu katika...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément