X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 05/Sep 06:14

MAAFISA UNUNUZI WA UMMA WAASWA KUFUATA SHERIA.

 Na Asia Singano, WF- KilimanjaroMaafisa Ununuzi wa Umma nchini wametakiwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za Ununuzi wa Umma ili kufikia malengo ya mabadiliko ya Sheria Mpya ya Ununuzi wa Umma ikiwa ni pamoja na kuwanufaisha wazawa.Rai hiyo ilitolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Kiseo Yusuf Nzowa, wakati akifungua mkutano wa Kikanda, Kanda ya Kaskazini mkoani Kilimanjaro kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu rasmi zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Kanda ya Kaskazini, uliyofanyika mkoani Kilimanjaro.Aliongeza kuwa kutokana na fursa zilizopo katika Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sheria hiyo italeta tija endapo watu wanaohusika na masuala ya ununuzi wa Umma wataifuata sheria hiyo na taratibu zote za ununuzi wa Umma.‘’Tumeona mabadiliko mazuri yaliyopo kwenye Sheria Mpya ya Ununuzi wa Umma, ambayo kwa kiasi kikubwa yananufaisha wazawa, wito wangu kwa wanaohusika na manunuzi waifuate Sheria hii’’ alisema Bw. Nzowa.Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya Kaskazini, Bw. Magai Maregesi, amewashauri Watanzania kujisajili kwenye mfumo mpya wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST), ili kunufaika na Sheria hiyo inayotoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wote wakiwamo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.‘’ Nawasihi Watanzania kuacha kukwepa Mfumo wa NeST kwa kuwa kuna fursa nyingi kwenye Sheria ya Ununuzi ikiwemo fursa za biashara na uwekezaji, bila kujisajili wazabuni hawatatambua uwepo wao kwa wepesi’’ Alisema Bw. Maregesi.Kabla ya Mikutano ya Kikanda inayoendelea kufanyika, ulianza mkutano kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi sahihi ya Takwimu rasmi kwa Wakuu wa mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa, na Waganga Wakuu wa Wilaya Jijini Dodoma hivi karibuni ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck nchemba (Mb).

Articles similaires

CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WA UMMA ZITATULIWE ILI KUKUZA SEKTA YA UMMA KIUCHUMI NA KIJAMII

msumbanews.co.tz - 05/Nov 09:20

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa neno la utangulizi kabla ya...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA ILI KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO YA WANANCHI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:02

 Na. Joseph Mahumi, WF, MorogoroSerikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo...

SERIKALI YAWASIHI WANANCHI KUTUMIA ELIMU YA FEDHA ILI KUKUZA UCHUMI

msumbanews.co.tz - 26/Oct 16:56

 Na. Farida Ramadhani na Joseph Mahumi, WF, Mbeya.Wakazi wa Jiji la Mbeya wametakiwa kutumia elimu waliyoipata katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma...

SERIKALI YAFIKIA ASILIMIA 85 KATIKA UPATIKANAJI WA DAWA

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:32

 Na : Jusline Marco;ArushaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu upatikanaji wa...

MAMENEJA RASILIMALIWATU KATIKA SEKTA YA UMMA AFRIKA WAMUUNGA MKONO RAIS DKT. SAMIA KUTANGAZA SEKTA YA UTALII WA TANZANIA

msumbanews.co.tz - 08/Nov 09:31

Rais wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na...

MAKAMANDA TFS WATAKIWA KUTUMIA TEHAMA KUBORESHA UTENDAJI KAZI

msumbanews.co.tz - 05/Nov 14:13

 Na Happiness Shayo- ArushaWaziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa...

WAZIRI MKUU AKAGUA MIUNDOMBINU YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI DODOMA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:01

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2024) amefanya ziara jijini Dodoma ili kukagua utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi...

CHANDE ASHAURI MABENKI KUTANUA WIGO WA MASOKO NJE YA NCHI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:25

 Na. Peter Haule na Josephine Majura, WF, Dodoma Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), ameitaka Akiba Commercial Bank Plc (ACB)...

PROF. SILAYO AWAPONGEZA WATUMISHI WA TFS KWA KUENDELEA KUKUZA VIPAJI

msumbanews.co.tz - 04/Nov 03:18

Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania TFS imeandaa bonanza la michezo kwa lengo la kuwakutanisha watumishi mbalimbali kutoka katika kanda zote nane...

NAIBU WAZIRI MWANAIDI AWATAKA WADAU KUJIKITA VIJIJINI, ELIMU YA KUPINGA UKATILI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:24

  Na WMJJWM-DodomaNaibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amewataka wadau wanaotoa elimu ya...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément