Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga leo Septemba 17, 2024 amefungua kikao kazi cha Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania...
Vous n'êtes pas connecté
Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga leo Septemba 17, 2024 amefungua kikao kazi cha Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Jijini Mwanza.Lengo la kikao hicho ni kujitathmini, kujipanga na kukumbushana masuala mbalimbali ya Taasisi, ikiwemo maelekezo mbalimbali ya Serikali ya uendeshaji wa kampuni.Amewasisitize na kuwakumbusha umuhimu wa kufanya kazi kwa umoja, ubunifu, weledi na upendo baina ya uongozi wa TPDC na wafanyakazi." Wizara ipo pamoja nanyi kuhakikisha azma na malengo makuu ya Serikali kwa TPDC yanafikiwa na zaidi", Amesisitiza Mhe. Kapinga. Aidha, amewakumbusha kuendelea kuyapa mkazo masuala yanayohusu wafanyakazi kwani ndio kiungo muhimu cha kufanikiwa kwa mipango na malengo mbalimbali ya TPDC."Ni vema masuala yanayohusu motisha zao ikiwemo mishahara kuhuishwa inapobidi na kuboreshwa kama hali ya kifedha inaruhusu", Amesema Mhe. Kapinga.Ameongeza kuwa itasaidia kuwapa morali ya kuendelea kufanya kazi TPDC na kuvutia pia wafanyakazi wazuri sokoni.Ametaka changamoto za wafanyakazi kukaimu nafasi za uongozi muda mrefu bila kuthibitishwa na changamoto za kupandishwa madaraja na nyinginezo zifanyiwe kazi ili kupunguza malalamiko kwa wafanyakazi.
Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga leo Septemba 17, 2024 amefungua kikao kazi cha Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania...
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amepongeza LESCO kwa kuendelea kusimamia haki na...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amepongeza Baraza la Ushauri wa Masuala ya...
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezitaka Mamlaka za Udhibiti na Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki kuzingatia weledi,...
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde amezipongeza Kampuni za uzalishaji wa makaa ya mawe kwa kuongeza uzalishaji na kuzitaka kuelekeza zaidi...
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha linatekeleza kwa kasi...
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema Serikali itaendelea kuweka mikakati madhubuti za kuwalinda wananchi...
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema Serikali itaendelea kuweka mikakati madhubuti za kuwalinda wananchi...
Na. Joseph Mahumi na Peter Haule, WF, DodomaSerikali imesema inaendelea kuweka mikakati na mbinu mbalimbali za muda mfupi, wa kati na mrefu katika...
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii yaahidi kuendelea kuimarisha juhudi za mazingira za kikanda na...