X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 24/Sep 06:24

MAANDAMANO YA CHADEMA YAHAMIA MITANDAONI

 Katika hali inayoleta maswali na sintofahamu wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) unaweza kusema wamemsusia Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Freeman Mbowe katika kushiriki maandamano yaliyopangwa kufanyika leo, Jumatatu Septemba 23.2024 jijini Dar es SalaamLicha ya ukweli kwamba kabla ya leo, kumeshuhudiwa mivutano baina ya CHADEMA, Jeshi la Polisi na serikali kwa ujumla ambapo mivutano hiyo imetokana na Jeshi la Polisi kuweka ngumu maandamano hayo jambo ambalo lilipingwa vikali na CHADEMA ambapo kupitia Mbowe waliahidi lazima waingie barabarani kuandamana.Polisi walitanda maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam na miji mikuu wakionyesha uimara wa kulinda amani, huku ikionesha wazi kutokua na muitikio kutoka kwa wananchi na hata wafuasi wa Chadema kama ilivyotarajiwa. Baadhi ya wananchi wamesema wafusi wengi wameandamana kwenye mitandao.Wadau mbalimbali hapa nchini na pengine hata nje ya mipaka ya Tanzania waliokuwa wanaofuatilia sakata hilo walitarajia pengine kuona idadi kubwa ya wafuasi wa chama hicho wakijitokeza barabarani kama sehemu ya hatua ya kuunga mkono viongozi wa kitaifa wa chama chao waliokuwa wamesita kujitokeza kushiriki maandaman .Katika kile ambacho unaweza kutafsiri kama usaliti kwa Mwenyekiti wao wa Taifa, viongozi wengi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA hawajajitokeza barabarani tofauti na ilivyotarajiwa hapo awali, au kama ilivyoshuhudiwa hamasa iliyojitokeza kwenye mitandao ya kijamii kabla ya leo.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya nje John Mrema iliyoeleza kulaani kushikiliwa kwa baadhi ya viongozi na wanachama wao leo, Jumatatu Septemba 23.2024 imeonesha kuwa wanachama wasiozidi 50 wanashikiliwa na Polisi, ambapo kati ya hao wapo baadhi ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho, lakini polisi ilitoa orodha ya watu 14 iliyowakamata.Hadi sasa viongozi waliothibitika kukamatwa ni pamoja na Freeman Mbowe mwenyewe, Makamu Mwenyekiti CHADEMA Tanzania Bara Tundu Lissu, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara Benson Kigaila, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini Godbles Lema na wengineo

Articles similaires

CHAGUENI VIONGOZI WAADILIFU-PINDA

msumbanews.co.tz - 27/Sep 05:41

Na Mwandishi Wetu, MLELE Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. Geophrey Pinda amewataka wananchi na...

MAWASILIANO NA MAHUSIANO YA UMMA YANAZIDI KUPATA UMUHIMU MKUBWA DUNIANI

msumbanews.co.tz - 24/Sep 05:49

 Imebainika kuwa taaluma ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma inazidi kupata umuhimu mkubwa katika ulimwengu wa sasa, ambapo uwazi, uaminifu, na...

DKT. BITEKO AAGIZA KIGOMA KUINGIZWA KWENYE GRIDI KABLA YA 2025

msumbanews.co.tz - 19/Sep 16:02

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha linatekeleza kwa kasi...

MBUNGE WA MSALALA ASISITIZA UWT KUJIANDIKISHA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA CCM

msumbanews.co.tz - 16/Sep 19:13

 MBUNGE  wa Jimbo la Msalala, Mheshimiwa Iddi Kassim Iddi, amewataka wanawake wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) Kijiji cha Kakola, Kata ya...

TAEC KUSHIRIKIANA NA ATC KUTOA STASHAHADA YA NYUKLIA

msumbanews.co.tz - 19/Sep 07:44

 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof. Najat Kassim Mohamed amesema Taasisi hiyo itakuwa mlezi wa programu maalumu ya...

VIONGOZI WATAKIWA KUYASEMEA MEMA YALIYOFANYWA NA RAIS SAMIA

msumbanews.co.tz - 21/Sep 05:42

 MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewataka viongozi wa Chama na Serikali ngazi ya Kata, kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa...

MACHIFU: RAIS SAMIA AHESHIMIWE

msumbanews.co.tz - 22/Sep 07:31

Mwenyekiti wa Machifu Tanzania Chifu Antonia Matalu akizungumza kwenye mjadala wa Machifu kuhusu mustakabali wa Tanzania kwenye masuala ya amani, mila...

HAKIKISHENI MRADI WA PROGRAMU YA KUIMARISHA KADA YA UALIMU UNAKAMILIKA KWA WAKATI DKT. MAHERA

msumbanews.co.tz - 29/Sep 06:53

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Charles Mahera Wilson amewataka watekelezaji wa Programu ya Kuboresha Kada ya Ualimu...

MAGARI YENYE MFUMO MBOVU WA BREKI YAKAMATWA MKOANI SONGWE

msumbanews.co.tz - 18/Sep 07:03

Wamiliki wa vyombo vya moto nchini wametakiwa kuhakikisha Madereva wa vyombo hivyo wanafuata sheria za usalama barabarani na kuacha mara moja tabia ya...

MAGARI YENYE MFUMO MBOVU WA BREKI YAKAMATWA MKOANI SONGWE

msumbanews.co.tz - 18/Sep 07:03

Wamiliki wa vyombo vya moto nchini wametakiwa kuhakikisha Madereva wa vyombo hivyo wanafuata sheria za usalama barabarani na kuacha mara moja tabia ya...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément