X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - Hier 07:44

TAEC KUSHIRIKIANA NA ATC KUTOA STASHAHADA YA NYUKLIA

 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof. Najat Kassim Mohamed amesema Taasisi hiyo itakuwa mlezi wa programu maalumu ya diploma ya masomo ya teknolojia ya nyuklia itakayoanzishwa na chuo cha ufundi Arusha (ATC).Prof. Najat ameyasema hayo katika ofisi za TAEC kanda ya kaskazini eneo la Njiro jijini Arusha baada ya kufanya kikao cha pamoja Kati ya uongozi wa TAEC na uongozi wa chuo cha ufundi Arusha kwa lengo la kuanza maandalizi ya kuanzisha diploma hiyo ya masomo ya nyuklia ambapo TAEC itakuwa mlezi kwa kutoa wataalamu wake watakaoongoza mchakato wa kuwezesha mtaala wa masomo hayo kufanikiwa.Prof. Najat ameongeza kuwa TAEC kwa kuwa ina wataalamu wa teknolojia ya  nyuklia imetenga muda wa mwaka mmoja kwa kushirikiana na chuo cha ufundi Arusha kwa ajili ya kuwaandaa walimu wa chuo hicho kwa kuwapatia mafunzo kwa njia ya nadharia na vitendo ili kuwajengea uwezo  walimu watakaokuwa na   dhamana ya  kufundisha masomo hayo.Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania ndiyo taasisi pekee ya serikali iliyopewa dhamana ya kusimamia matumizi salama ya mionzi nchini, kuhamasisha na  kuendeleza teknolojia ya nyuklia katika sekta mbalimbali kama vile afya, kilimo, mifugo, nishati, migodi, viwanda, maji na kufanya tafiti mbalimbali kwa kutumia Teknolojia ya Nyuklia sambamba na kutoa ushauri kwa serikali juu ya mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohusisha matumizi salama ya  teknolojia ya nyuklia.

Articles similaires

KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA UJENZI WA MAABARA YA TAEC ZANZIBAR

msumbanews.co.tz - 10/Sep 20:13

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu Utamaduni na Michezo Husna Sekiboko ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh. Dkt....

HAKIELIMU YAZINDUA MRADI WA MAJARIBIO KUWEZESHA WALIMU KUFUNDISHA KWA VITENDO

msumbanews.co.tz - 13/Sep 05:26

 Shirika la HakiElimu Tanzania limezindua mradi wa majaribio ambao umelenga kukuza ufundishaji wa walimu,kupitia teknolojia ambayo itamwezesha...

NG'UMBI AWATAKA WADAU KUONGEZA USHIRIKIANO KATIKA ELIMU

msumbanews.co.tz - 16:38

Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Prof. Michael Ng’umbi akifafanua jambo wakati wa mahojiano maalum kuhusu hali ya elimu nchini kupitia...

SHULE 26 ZAJENGWA NCHINI KUONGEZA MKAZO MASOMO YA SAYANSI KWA WASICHANA

msumbanews.co.tz - 09/Sep 11:21

Serikali imeongeza mkazo katika masomo ya Sayansi ikiwa ni pamoja na kujenga shule 26 za wasichana zinazotoa masomo ya Sayansi.Hayo yamesemwa na...

𝗖𝗖𝗠 MERU 𝗪𝗔𝗞𝗢𝗦𝗛𝗪𝗔 𝗡𝗔 𝗠𝗜𝗨𝗡𝗗𝗢𝗠𝗕𝗜𝗡𝗨 YA 𝗖𝗛𝗨𝗢 𝗡𝗔 𝗦𝗛𝗨𝗟𝗘 𝗠𝗔𝗔𝗟𝗨𝗠 𝗣𝗔𝗧𝗔𝗡𝗗𝗜

msumbanews.co.tz - 17:20

Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arumeru Bw. Kennedy Mpumilwa ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia...

ELIMU YA FEDHA YAWAFIKIA WANANCHI WA MKURANGA

msumbanews.co.tz - 11/Sep 05:10

 Na. Saidina Msangi, Mkuranga Pwani.Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, imewasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kwa...

WANANCHI LONGIDO WATAKA SHULE ZA BWENI KUIMARISHWA ULINZI

msumbanews.co.tz - 07/Sep 11:12

Wananchi wa Wilaya ya Longido Mkoani Arusha wameiomba serikali kujengea uzio shule zote za serikali za bweni zilizopo katika wilaya hiyo lengo ni...

MA RC NA MA DC WAAGIZWA KUSIMAMIA UBAINISHAJI WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

msumbanews.co.tz - 18/Sep 06:23

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amewaagiza  wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha  wanasimamia zoezi la ubainishaji wa...

MA RC NA MA DC WAAGIZWA KUSIMAMIA UBAINISHAJI WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

msumbanews.co.tz - 18/Sep 06:23

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amewaagiza  wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha  wanasimamia zoezi la ubainishaji wa...

MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA ELIMU ATEMBELEA MRADI WA EASTRIP, NIT

msumbanews.co.tz - 14/Sep 05:06

 KUPITIA Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) inatekeleza mradi wa EASTRIP (East Africa Skills for...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément