Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof. Najat Kassim Mohamed amesema Taasisi hiyo itakuwa mlezi wa programu maalumu ya...
Vous n'êtes pas connecté
Shirika la HakiElimu Tanzania limezindua mradi wa majaribio ambao umelenga kukuza ufundishaji wa walimu,kupitia teknolojia ambayo itamwezesha Mwanafunzi kupata picha halisi ya kitu anachofundishwa.Akizungumza leo Septemba 12,2024 Jijini Dar es salaam Mkuu wa Programu Shirika la HakiElimu Bw.Godfrey Boniventura wakati wa uzinduzi wa mradi huo amesema kuwa mradi huo umekusudia kumfundisha mwanafunzi kwa vitendo na sio nadharia pekee ambapo wanafunzi watafundishwa kwa kutumia vitu katika picha na maumbo yake halisi."Hata kama unataka kumfundisha mtu awe makenika (fundi wa gari) labda kufunga mguu wa gari(shock up) unamfundisha kwa maumbo halisi na kumuonesha inapofungwa ambapo anapata picha halisi kwa namna ya kufanya". Amesema.Aidha Boniventura amesema baada ya mradi huo wa majaribio kukamilika wanatarajia kutanua wigo kwa kushirikisha taasisi mbalimbali za elimu nchini.Aidha Boniventura amesema Taasisi ya Hamk ,Save the Children na taasisi 5 za kitaaluma zimeshiriki katika kuhakikisha utekelezaji mzuri wa mradi huo wa majaribio ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ambapo itakuwa njia nzuri ya kupima ufanisi na umuhimu wake katika mazingira ya Kitanzania.Kwa upande wake kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dkt. Abdalah Ngodu ametoa shukrani zake kwa waandaaji wa mradi huo ambapo anatarajia kuona ubunifu na mipango yenye matokeo kwenye maisha ya wanafunzi kwa kuzalisha ujuzi wenye kuleta tija kwa jamii.Aidha amesema kuwa ukuaji wa kasi wa teknolojia,unachangia uhitaji wa zana za kisasa kama teknolojia ya VR na XR ambao pia ni sehemu ya maudhui ya mradi huo ambapo inatoa mwanya kwa wakufunzi na wanafunzi kujifunza mtandaoni kwa pamoja kabla ya kufanya vitendo katika ulimwengu halisi.Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali (VTA), Dkt. Bakari Ali Silima amesema uingizwaji wa mfumo wa kidijitali wa maudhui ya mafunzo katika teknolojia ya vipimo vitatu na matumizi ya miundombinu ya TEHAMA, kutawezesha kutumia mwalimu mmoja kutoa mafunzo kwa wanafunzi wengi katika maeneo tofauti kwa wakati mmoja.Mradi huo wa majaribio unatarajiwa kufanyika kwa miaka miwili ambapo umefadhiliwa na kampuni ya 3D BEAR na kuratibiwa nchini na Chuo kikuu Cha Hamk,Shirika la Save The Children,HakiElimu pamoja na vyuo vikuu Vitano.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof. Najat Kassim Mohamed amesema Taasisi hiyo itakuwa mlezi wa programu maalumu ya...
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezitaka Mamlaka za Udhibiti na Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki kuzingatia weledi,...
KUPITIA Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) inatekeleza mradi wa EASTRIP (East Africa Skills for...
Waziri wa Ujenzi,Innocent Bashungwa amewataka Wahandisi kuwajibika katika majukumu pale wanapopatiwa mradi ili kulinda thamani yao. Akizungumza...
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepongeza juhudi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kuboresha mitaala yake ili kukidhi...
NAIBU waziri mkuu Dk Dotto Biteko amewataka maafisa manunuzi na ugavi nchini kufanya kazi zao Kwa uadilifu ,uwajibikaji uwazi na maadili katika...
Wajasiriamali wadogo wapatao 500 wanaojihusisha na uchimbaji na uchakataji kokoto Jijini Dar es Salaam wamewezeshwa vifaa kinga na kupatiwa mafunzo...
Wajasiriamali wadogo wapatao 500 wanaojihusisha na uchimbaji na uchakataji kokoto Jijini Dar es Salaam wamewezeshwa vifaa kinga na kupatiwa mafunzo...
Mkuu wa Idara ya Utafiti kutoka Haki Elimu Makumba Mwemezi amesema utafiti uliofanywa na Taasisi hiyo umebaini kuwa asilimia 44.4 ya vijana katika...
Kampuni ya simu za mkononi Airtel kupitia kwa Mkurugenzi wa Biashara Joseph Muhele amesema kuwa mtandao huo mwaka huu 2024 unaendelea kufangua...