X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - Hier 06:23

MA RC NA MA DC WAAGIZWA KUSIMAMIA UBAINISHAJI WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amewaagiza  wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha  wanasimamia zoezi la ubainishaji wa watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kupata fursa ya elimu.Akifungua maadhimisho ya miaka 30 ya elimu jumuishi  Patandi Jijini Arusha Mhe. Mchengerwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama kufuatlia wazazi wanaowaficha watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kupata elimu kama stahiki ya mtoto wa Kitanzania.“Nawaelekeza Viongozi wote wa Mikoa na Halmashauri nchini kusimamia zoezi la ubainishaji na utambuzi wa awali wa watoto kwa wakati ili kubaini wenye mahitaji maalumu, kuwahimiza na kuhakikisha wazazi na walezi wanawapeleka watoto wao katika shule zilizoshauriwa na wataalamu ili wakaandikishwe na kuanza masomo na taarifa ya utekelezaji wake itolewe” amesema  Mhe. Mchengerwa. Mchengerwa amesema hadi kufikia mwaka 2020 kulikuwa na wanafunzi wenye mahitaji maalumu 28,482 lakini idadi hiyo imeongezeka mpaka wanafunzi 78,429 mwaka 2024 na Serikali imetenga jumla ya shule 6,088 zinazopokea wanafunzi hao na kuwapatia afua stahiki ambapo shule takriban 309 zina mabweni kwa ajili ya wanafunzi hao.Naye Dkt. Magreth Matonya, Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Maalumu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia amesema malengo ya maadhimisho hayo ni kutangaza fursa za wanafunzi wenye mahitaji maalum zinazotolewa na Serikali, kutangaza mafanikio yaliyopatikana, kutoa elimu ya uhamasishaji na pia kufanya tathmini ya elimu jumuishi. Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Maafisa Elimu wa Mikoa, Maafisa Elimu Watu Wazima Mikoa yote, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Elimu Msingi na Sekondari, Maafisa kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maafisa Elimu Maalum wa Halmashauri na Wadau mbalimbali wanaoihunga mkono Serikali.

Articles similaires

MA RC NA MA DC WAAGIZWA KUSIMAMIA UBAINISHAJI WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

msumbanews.co.tz - 06:23

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amewaagiza  wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha  wanasimamia zoezi la ubainishaji wa...

𝗖𝗖𝗠 MERU 𝗪𝗔𝗞𝗢𝗦𝗛𝗪𝗔 𝗡𝗔 𝗠𝗜𝗨𝗡𝗗𝗢𝗠𝗕𝗜𝗡𝗨 YA 𝗖𝗛𝗨𝗢 𝗡𝗔 𝗦𝗛𝗨𝗟𝗘 𝗠𝗔𝗔𝗟𝗨𝗠 𝗣𝗔𝗧𝗔𝗡𝗗𝗜

msumbanews.co.tz - 17:20

Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arumeru Bw. Kennedy Mpumilwa ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia...

WIZARA YA FEDHA YATOA MAFUNZO KWA MAAFISA UNUNUZI WA TAASISI ZA UMMA.

msumbanews.co.tz - 06/Sep 04:51

 Na Chedaiwe Msuya, WF.Wizara ya Fedha inaendelea kutoa mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta...

WAZIRI MCHENGERWA ATAKA UDHIBITI WA MPOX - MIPAKANI

msumbanews.co.tz - 13:55

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa ya pembezoni mwa nchi na...

WAZIRI JAFO ATAKA WANANCHI KUACHA KUCHANGANYA MAZAO

msumbanews.co.tz - 10:06

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama wakitembelea na kukagua Ghala la Mpako...

DC Mpogolo aendelea na ziara ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi wa Jimbo la Ukonga

msumbanews.co.tz - 14/Sep 05:47

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo leo Septemba 12 ,2024 ameendelea na ziara ya kutatua kero za Wananchi wa Kata za Kitunda, Kivule, Mzinga...

NG'UMBI AWATAKA WADAU KUONGEZA USHIRIKIANO KATIKA ELIMU

msumbanews.co.tz - 16:38

Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Prof. Michael Ng’umbi akifafanua jambo wakati wa mahojiano maalum kuhusu hali ya elimu nchini kupitia...

ELIMU YA FEDHA YAWAFIKIA WANANCHI WA MKURANGA

msumbanews.co.tz - 11/Sep 05:10

 Na. Saidina Msangi, Mkuranga Pwani.Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, imewasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kwa...

WANANCHI LONGIDO WATAKA SHULE ZA BWENI KUIMARISHWA ULINZI

msumbanews.co.tz - 07/Sep 11:12

Wananchi wa Wilaya ya Longido Mkoani Arusha wameiomba serikali kujengea uzio shule zote za serikali za bweni zilizopo katika wilaya hiyo lengo ni...

MAAFISA UNUNUZI WA UMMA WAASWA KUFUATA SHERIA.

msumbanews.co.tz - 05/Sep 06:14

 Na Asia Singano, WF- KilimanjaroMaafisa Ununuzi wa Umma nchini wametakiwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za Ununuzi wa Umma ili kufikia malengo...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément