X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 19/Sep 07:44

TAEC KUSHIRIKIANA NA ATC KUTOA STASHAHADA YA NYUKLIA

 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof. Najat Kassim Mohamed amesema Taasisi hiyo itakuwa mlezi wa programu maalumu ya diploma ya masomo ya teknolojia ya nyuklia itakayoanzishwa na chuo cha ufundi Arusha (ATC).Prof. Najat ameyasema hayo katika ofisi za TAEC kanda ya kaskazini eneo la Njiro jijini Arusha baada ya kufanya kikao cha pamoja Kati ya uongozi wa TAEC na uongozi wa chuo cha ufundi Arusha kwa lengo la kuanza maandalizi ya kuanzisha diploma hiyo ya masomo ya nyuklia ambapo TAEC itakuwa mlezi kwa kutoa wataalamu wake watakaoongoza mchakato wa kuwezesha mtaala wa masomo hayo kufanikiwa.Prof. Najat ameongeza kuwa TAEC kwa kuwa ina wataalamu wa teknolojia ya  nyuklia imetenga muda wa mwaka mmoja kwa kushirikiana na chuo cha ufundi Arusha kwa ajili ya kuwaandaa walimu wa chuo hicho kwa kuwapatia mafunzo kwa njia ya nadharia na vitendo ili kuwajengea uwezo  walimu watakaokuwa na   dhamana ya  kufundisha masomo hayo.Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania ndiyo taasisi pekee ya serikali iliyopewa dhamana ya kusimamia matumizi salama ya mionzi nchini, kuhamasisha na  kuendeleza teknolojia ya nyuklia katika sekta mbalimbali kama vile afya, kilimo, mifugo, nishati, migodi, viwanda, maji na kufanya tafiti mbalimbali kwa kutumia Teknolojia ya Nyuklia sambamba na kutoa ushauri kwa serikali juu ya mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohusisha matumizi salama ya  teknolojia ya nyuklia.

Articles similaires

MAKAMANDA TFS WATAKIWA KUTUMIA TEHAMA KUBORESHA UTENDAJI KAZI

msumbanews.co.tz - 05/Nov 14:13

 Na Happiness Shayo- ArushaWaziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa...

RAIS DKT. SAMIA AMWAGA AJIRA KWA WAALIMU 29,879

msumbanews.co.tz - 01/Nov 09:27

 Elimu ndio kipaumbele cha Serikali ya Awamu ya Sita, kwa kuzingatia hilo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia walimu wapya 29,879 wa Shule za...

RAIS SAMIA ANATARAJIWA KUZINDUA MFUMO WA MIKOPO WENYE THAMANI YA BILIONI 2.3..

msumbanews.co.tz - 07/Nov 04:30

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzindua rasmi mfuko wa mikopo wenye kianzio cha shilingi bilioni 2.3...

Chuo cha Uhasibu Arusha kutoa mafunzo ya Uhasibu, Tehama na Uongozi Comoro

msumbanews.co.tz - 05/Nov 09:55

Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Profesa Eliamani Sedoyeka anaongoza ujumbe wa chuo hicho katika mazungumzo na Chuo Kikuu cha Comoro ili...

PROF. SILAYO AWAPONGEZA WATUMISHI WA TFS KWA KUENDELEA KUKUZA VIPAJI

msumbanews.co.tz - 04/Nov 03:18

Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania TFS imeandaa bonanza la michezo kwa lengo la kuwakutanisha watumishi mbalimbali kutoka katika kanda zote nane...

CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WA UMMA ZITATULIWE ILI KUKUZA SEKTA YA UMMA KIUCHUMI NA KIJAMII

msumbanews.co.tz - 05/Nov 09:20

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa neno la utangulizi kabla ya...

OUT YATOA MAFUNZO KUIMARISHA UFUATILIAJI NA USIMAMIZI WA MIRADI SERIKALINI

msumbanews.co.tz - 27/Oct 08:36

Mafunzo ya ufuatiliaji na tathmini yanayoendeshwa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa watumishi wa mamlaka za serikali za mitaa pamoja tawala za...

AICC NI MUHIMILI WA SEKTA YA UTALII NCHINI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 09:36

 Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kimeelezwa kuwa ni moja ya muhimili muhimu katika kufanikisha agenda ya Rais Samia Suluhu Hassan...

PROF. MKENDA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEKITI WA BARAZA LA CHUO KIKUU MZUMBE

msumbanews.co.tz - 01/Nov 18:10

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Baraza na Menejimenti ya Chuo Kikuu...

MANISPAA YA MOSHI KUONGEZA NGUVU KATIKA VIKUNDI VYA VIKOBA UTOAJI WA ELIMU YA CHANJO.

msumbanews.co.tz - 07/Nov 04:38

Na. Elimu ya Afya kwa UmmaKatika kuhakikisha huduma za chanjo zinafanikiwa kwa ufasaha na kuleta tija katika jamii, Manispaa ya Moshi Mkoani...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément