Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewataka Viongozi wa Matawi, Mashina, Mitaa na Kata Kutimiza Majukumu yao kuelekea Uchaguzi wa...
Vous n'êtes pas connecté
Mkuu wa wilaya ya ilala Edward Mpogolo amewataka viongozi wa chama na serikali kuwa na mahusiano mazuri katika kazi zao.Akiongea na viongozi wa chama na serikali katika ziara yake kwenye kata ya liwiti, tabata na kimanga Mpogolo ameeleza mahusiano ya viongozi hao yanasaidia kuelewa kazi zinazofanywa katika miradi ya maendeleo hivyo wasione ugeni kushirikiana.Ameongeza kuwa hata katiba ya nchi inatambua mahusiano na mfumo wa chama chenye dhamana na serikali iliyopo madarani kupitia ilani inayotekelezeka. Akielezea kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu amewataka wananchi kushiriki, kujiandikisha na kupiga kura na kudumisha umoja, upendo na mshikamano. Amesema viongozi wahamasishe wananchi kujiandikisha katika daftari litalikuwa katika maeneo ya mitaa wanayoishi zoezi ambalo litaanza tarehe 11 hadi 20 mwezi ujao na uchaguzi ni novemba 27 mwaka huu. Akijibu kero zilizowasilishwa katika mkutano uwo Mpogolo amesema kero zinazohusu elimu hasa uzio katika shule ya sekondari liwiti iliyopakana na shule mbili za msingi halmashauri itahakikisha inatatuliwa kwa wakati. Kero nyingine aliyoitolea ufafanuzi ni kuhusu mto msimbazi ambao ni kilio kwa wananchi na serikali tayari imeona na kuanza kutafuta njia ya kuondoa kero hiyo kwa kuwa mto uwo umekuwa na tabia ya kuhama hama. Kuhusu kero ya barabara katika kata ya tabata, liwiti na kimanga ameleeza barabara hizo zipo zilizoingia katika mradi wa Dmpd na nyingine zitashughulikiwa na tarura.Aidha Mkuu wa wilaya ya ilala Edward Mpogolo amewataka viongozi, wazazi na walezi kusimamia maadili ya watoto kwa ujumla hasa waliomaliza darasa la saba wasipate mimba na magonjwa ya zinaa.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewataka Viongozi wa Matawi, Mashina, Mitaa na Kata Kutimiza Majukumu yao kuelekea Uchaguzi wa...
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,CPA Amos Makalla, amesema chama hicho hakipo tayari kusimamisha...
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo leo Septemba 12 ,2024 ameendelea na ziara ya kutatua kero za Wananchi wa Kata za Kitunda, Kivule, Mzinga...
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewahakikishia wananchi wa Kata za Mnyamani,Vingunguti na Buguruni kuwa Serikali inaendelea kuboresha...
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewahakikishia wananchi wa Kata za Mnyamani,Vingunguti na Buguruni kuwa Serikali inaendelea kuboresha...
Mbunge wa Jimbo la Ukonga ambaye pia ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry Silaa amewataka wanachama wa Chama cha...
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha linatekeleza kwa kasi...
Na Mwandishi Wetu,Manyara .Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amejitokeza...
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogogolo, leo anaendelea na ziara yake katika Jimbo la Segerea yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wanchi...
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogogolo, leo anaendelea na ziara yake katika Jimbo la Segerea yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wanchi...