X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 19/Sep 05:50

DC MPOGOLO ATAKA VIONGOZI KUWA NA MAHUSIANO MEMA

 Mkuu wa wilaya ya ilala Edward Mpogolo amewataka viongozi wa chama na serikali kuwa na mahusiano mazuri katika kazi zao.Akiongea na viongozi wa chama na serikali katika ziara yake kwenye kata ya liwiti, tabata na kimanga Mpogolo ameeleza mahusiano ya viongozi hao yanasaidia kuelewa kazi zinazofanywa katika miradi ya maendeleo hivyo wasione ugeni kushirikiana.Ameongeza kuwa hata katiba ya nchi inatambua mahusiano na mfumo wa chama chenye dhamana  na serikali iliyopo madarani kupitia ilani inayotekelezeka. Akielezea kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu amewataka wananchi kushiriki, kujiandikisha na kupiga kura na kudumisha umoja, upendo na mshikamano. Amesema viongozi wahamasishe wananchi kujiandikisha katika daftari litalikuwa katika maeneo ya mitaa wanayoishi zoezi ambalo litaanza tarehe 11 hadi 20 mwezi ujao na uchaguzi ni novemba 27 mwaka huu. Akijibu kero zilizowasilishwa katika mkutano uwo Mpogolo amesema kero zinazohusu elimu hasa uzio katika shule ya sekondari liwiti iliyopakana na shule mbili za msingi halmashauri itahakikisha inatatuliwa kwa wakati. Kero nyingine aliyoitolea ufafanuzi ni kuhusu mto msimbazi ambao ni kilio kwa wananchi na serikali tayari imeona na kuanza kutafuta njia ya kuondoa kero hiyo kwa kuwa mto uwo umekuwa na tabia ya kuhama hama. Kuhusu kero ya barabara katika kata ya tabata, liwiti na kimanga ameleeza barabara hizo zipo zilizoingia katika mradi wa Dmpd na nyingine zitashughulikiwa na tarura.Aidha Mkuu wa wilaya ya ilala Edward Mpogolo amewataka viongozi, wazazi na walezi kusimamia maadili ya watoto kwa ujumla hasa waliomaliza darasa la saba wasipate mimba na magonjwa ya zinaa.

Articles similaires

TGNP YATOA MAFUNZO KWA WANAWAKE WAGOMBEA SERIKALI ZA MITAA

msumbanews.co.tz - 28/Oct 07:43

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umefanya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji ...

RC MTAKA : NJOMBE TUPO TAYARI KWA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

msumbanews.co.tz - 04/Nov 05:03

Mkoa wa Njombe unajiandaa kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024. Uchaguzi huo ni fursa muhimu kwa...

CCM DODOMA MJINI YAANZA KUWANOA MABALOZI KUJIANDAA NA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

msumbanews.co.tz - 06/Nov 16:57

Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Dodoma Mjini kimeanza mikutano ya ndani ya kuwajengea uwezo wenyeviti wa mashina(Mabalozi) kuelekea Uchaguzi wa...

UCHAGUZI SIO VURUGU WALA SIO VITA, UCHAGUZI NI HAKI YA KIKATIBA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 07:59

 Wananchi wa Mkoa wa Songwe pamoja na viongozi wa vyama vya siasa wametakiwa kufanya kampeni za kistaarabu na kushiriki uchaguzi kwa amani kipindi...

TGNP YATOA MAFUNZO YA UONGOZI KWA VIONGOZI WA VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA

msumbanews.co.tz - 02/Nov 14:38

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), wameendesha mafunzo kwa viongozi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa kutoka mikoa  ya Kilimanjaro, Manyara, Dodoma,...

NLD watoa wito kwa TAMISEMI kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.

msumbanews.co.tz - 05/Nov 13:38

 Na Denis Chambi, Tanga.CHAMA cha National league for Democracy 'NLD' kimeitaka  Ofisi ya Rais tawala za mika na Serikali za mitaa 'TAMISEMI'...

DC MPOGOLO AWATAKA WABUNIFU NA WAKADIRIAJI MAJENZI KUWA WAZALENDO

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:38

 Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ametoa wito kwa Wabunifu na Wakadiriaji majenzi nchini kuwa Wazalendo, Waadilifu na Wabunifu kwa Taifa katika...

RC BATILDA AIPONGEZA HANDENI DC KWA MAANDALIZI MAZURI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

msumbanews.co.tz - 06/Nov 12:16

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dk Batilda Burian amaeipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa maandalizi mazuri ya uchaguzi wa Serikali za...

MIRADI YA TACTIC KUIMARISHA MAZINGIRA YA UFANYAJI WA BIASHARA NCHINI- MHE. KATIMBA.

msumbanews.co.tz - 02/Nov 16:02

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema kukamilika kwa Miradi ya TACTIC mkoani...

UJENZI WA SOKO LA MWANGA NA KATONGA UTAIMARISHA MAZINGIRA YA BIASHARA KIGOMA- MHE. KATIMBA.

msumbanews.co.tz - 02/Nov 16:10

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema ujenzi wa Soko la Kisasa la Mwanga na Soko la...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément