Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...
Vous n'êtes pas connecté
Na Mwandishi Wetu MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Bandari ya kisasa ya Mbambabay utakaogharimu Sh.Bilioni 81, utaufungua Mkoa kiuchumi kwa kuuza bidhaa mbalimbali nchi za Malawi na Msumbiji. Kanali Ahmed aliyasema hayo jana alipokuwa akikagua utayari wa Wilaya za Mkoa huo kuhusu ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan na kilele cha Tamasha la Kitaifa la tatu la Utamaduni litakalofanyika uwanja wa Majimaji Manispaa ya Songea. Alisema serikali imeelekeza fedha hizo zitekeleze mradi huo ikiwa ni miongoni mwa miradi mikubwa itakayoipaisha Ruvuma kiuchumi. Alisema ujenzi wa bandari hiyo ukikamilika utasaidia kutoa ajira, kuinua uchumi, kupeleka na kupokea bidhaa mbalimbali ikiwamo mazao, samaki na bidhaa za viwandani katika nchi jirani za Malawi na Msumbiji. “Tunamshukuru Rais kwa kuleta fedha nyingi kutekeleza miradi mbalimbali inayogusa wananchi wetu kwenye sekta ya afya, elimu, miundombinu kama unavyoona hapa kutajengwa bandari hii ambayo Sh.Bilioni 81 zimetolewa kutekeleza mradi huu,”alisema. Aidha, Mkuu huyo alikagua barabara ya Mbinga hadi Mbambay ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami na kwamba barabara hiyo itafungua uchumi wa mkoa huo kwa kuwa ni kiunganishi kati ya Tanzania, Malawi na Msumbiji. Alisema mkoa huo umejiandaa kumpokea Rais Samia katika ziara yake itakayoambatana na matukio mbalimbali ikiwamo Tamasha hilo. “Rais anakuja kwa mara ya kwanza tangu awe Rais wa Tanzania, pia anakuja kwenye tamasha la kitaifa ambalo sisi Ruvuma tumechaguliwa tuwe wenyeji wa hili na kama unavyofahamu ni Mkoa umesheheni tamaduni nyingi,”alisema. Alibainisha kuwa ziara hiyo ya Rais inalenga kukagua miradi ambayo mkoa huo umepokea fedha nyingi kuitekeleza katika sekta mbalimbali.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...
MBUNGE wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu amesema kazi ya Rais Dkt Samia Suluhu anayoifanya ya Maendeleo katika Mkoa wa Tanga sio ya kutafuta kwa...
Imeelezwa kuwa, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umepeleka umeme kwa wananchi wapatao 2,400 wa vijiji nane (8) vya Tarafa ya Lupembe, Wilaya ya...
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa kipaumbele kwenye ujenzi wa miradi ya nishati jadidifu nchini ili kusaidia utunzaji wa mazingira, kuzalisha...
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba madelu (Mb), akiteta jambo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika...
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema kukamilika kwa Miradi ya TACTIC mkoani...
Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ametoa wito kwa Wabunifu na Wakadiriaji majenzi nchini kuwa Wazalendo, Waadilifu na Wabunifu kwa Taifa katika...
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema ujenzi wa Soko la Kisasa la Mwanga na Soko la...
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2024) amefanya ziara jijini Dodoma ili kukagua utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi...
Na. Joseph Mahumi, WF, MorogoroSerikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo...