X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - Hier 08:00

BIL.81/- KUJENGA BANDARI YA KISASA MBAMBABAY-RUVUMA

Na Mwandishi Wetu MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Bandari ya kisasa ya Mbambabay utakaogharimu Sh.Bilioni 81, utaufungua Mkoa kiuchumi kwa kuuza bidhaa mbalimbali nchi za Malawi na Msumbiji. Kanali Ahmed aliyasema hayo jana alipokuwa akikagua utayari wa Wilaya za Mkoa huo kuhusu ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan na kilele cha Tamasha la Kitaifa la tatu la Utamaduni litakalofanyika uwanja wa Majimaji Manispaa ya Songea. Alisema serikali imeelekeza fedha hizo zitekeleze mradi huo ikiwa ni miongoni mwa miradi mikubwa itakayoipaisha Ruvuma kiuchumi. Alisema ujenzi wa bandari hiyo ukikamilika utasaidia kutoa ajira, kuinua uchumi, kupeleka na kupokea bidhaa mbalimbali ikiwamo mazao, samaki na bidhaa za viwandani katika nchi jirani za Malawi na Msumbiji. “Tunamshukuru Rais kwa kuleta fedha nyingi kutekeleza miradi mbalimbali inayogusa wananchi wetu kwenye sekta ya afya, elimu, miundombinu kama unavyoona hapa kutajengwa bandari hii ambayo Sh.Bilioni 81 zimetolewa kutekeleza mradi huu,”alisema. Aidha, Mkuu huyo alikagua barabara ya Mbinga hadi Mbambay ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami na kwamba barabara hiyo itafungua uchumi wa mkoa huo kwa kuwa ni kiunganishi kati ya Tanzania, Malawi na Msumbiji. Alisema mkoa huo umejiandaa kumpokea Rais Samia katika ziara yake itakayoambatana na matukio mbalimbali ikiwamo Tamasha hilo. “Rais anakuja kwa mara ya kwanza tangu awe Rais wa Tanzania, pia anakuja kwenye tamasha la kitaifa ambalo sisi Ruvuma tumechaguliwa tuwe wenyeji wa hili na kama unavyofahamu ni Mkoa umesheheni tamaduni nyingi,”alisema. Alibainisha kuwa ziara hiyo ya Rais inalenga kukagua miradi ambayo mkoa huo umepokea fedha nyingi kuitekeleza katika sekta mbalimbali.

Articles similaires

KISHINDO CHA TAMASHA LA UTAMADUNI RUVUMA,RAIS SAMIA APONGEZWA

msumbanews.co.tz - 14/Sep 11:05

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Ahmed Abbas Ahmed ,akizungumza na wamiliki wa hoteli kuhusu fursa za Tamasha la Kitaifa la Utamaduni Baadhi ya wamiliki wa...

MAONESHO YA MAVAZI, CHAKULA, NGOMA KUNOGESHA TAMASHA LA UTAMADUNI RUVUMA

msumbanews.co.tz - 17/Sep 11:10

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro,akizungumza kuhusu Tamasha la tatu la utamaduni kitaifa litakaloanza Septemba 20-23, mwaka...

WAZEE TUNDURU WAOIMBA SERIKALI KUFUNGUA SOKO JIPYA LA MADINI YA VITO

msumbanews.co.tz - 12/Sep 07:54

Baadhi ya majengo katika soko jipya la madini ya vito yanayoendelea kujengwa na Halmashauri ya wilaya Tunduru kwa kushirikiana na wadau wa madini...

DKT. BITEKO AAGIZA KIGOMA KUINGIZWA KWENYE GRIDI KABLA YA 2025

msumbanews.co.tz - 16:02

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha linatekeleza kwa kasi...

ZAIDI YA WANANCHI 4300 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI NDELENYUMA RUVUMA

msumbanews.co.tz - 06:27

 WANANCHI zaidi ya elfu 4 wanatarajia kunufaika na huduma ya maji safi na salama, kufuatia Mradi wa Maji wa Bilioni 1.6 ambao umefikia asilimia 86.7...

REA YATUMIA ZAIDI YA BIL. 100 KUTEKELEZA MIRADI YA UMEME VIJIJINI KIGOMA

msumbanews.co.tz - 06:18

Katika kuendelea kuboresha maisha ya wananchi Vijijini, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 100 kutekeleza miradi ya...

REA YATUMIA ZAIDI YA BIL. 100 KUTEKELEZA MIRADI YA UMEME VIJIJINI KIGOMA

msumbanews.co.tz - 06:19

 Katika kuendelea kuboresha maisha ya wananchi Vijijini, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 100 kutekeleza miradi ya...

DKT.JAFO AAGIZA  MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KILWA KUKAMILIKA KWA WAKATI

msumbanews.co.tz - 18/Sep 08:28

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa na viongozi wakitembelea mradi wa bandari ya Uvuvi uliopo Kilwa Masoko wilayani Kilwa...

WAZIRI JAFO ATAKA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KILWA KUKAMILIKA KWA WAKATI

msumbanews.co.tz - 18/Sep 10:27

 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa na viongozi wakitembelea mradi wa bandari ya Uvuvi uliopo Kilwa Masoko wilayani Kilwa...

WAZIRI JAFO ATAKA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KILWA KUKAMILIKA KWA WAKATI

msumbanews.co.tz - 18/Sep 10:27

 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa na viongozi wakitembelea mradi wa bandari ya Uvuvi uliopo Kilwa Masoko wilayani Kilwa...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément