X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - Aujourd'hui 09:01

RAIS SAMIA AKABIDHI BOTI 35 KWA WAVUVI TANGA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumatano Februari 26, 2025 amekabidhi boti 35 za kisasa kwa wavuvi wa Mkoa wa Tanga, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa ukopeshaji wa boti kwa wavuvi nchini.Mradi huu, unaosimamiwa na Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, unalenga kusaidia wavuvi katika Ukanda wa Pwani, Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa ili kuongeza tija katika sekta ya uvuvi na kuhakikisha uvuvi endelevu. Awamu ya kwanza ya mradi huu ilianza mwaka wa fedha 2022/2023 kwa gharama ya shilingi bilioni 11.5, ambapo boti 160 zilikopeshwa kwa wanufaika 3,163.Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa boti hizo zitasaidia si tu kuongeza uzalishaji wa mazao ya uvuvi, bali pia kudhibiti uvuvi haramu. Alieleza kuwa vijana 113 kutoka Mkoa wa Tanga, ambao hapo awali walijihusisha na uvuvi haramu, wameamua kubadili maisha yao na sasa wanajiunga na vikundi vya uvuvi halali kupitia mpango huu wa mikopo nafuu.Katika bajeti ya mwaka 2024/2025, Serikali imetenga boti 120 kwa ajili ya wavuvi, ambapo boti 70 zitapelekwa Ukanda wa Pwani (Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, na Mtwara), boti 29 zitapelekwa Ziwa Victoria, na boti 21 zitapelekwa Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa.Boti 35 zilizokabidhiwa leo zina thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4.477, na moja ya boti hizo imekabidhiwa kwa kikundi cha vijana wa Tanga, ambao wameahidi kuwa walinzi wa rasilimali za uvuvi ndani ya taifa.Huu ni mwendelezo wa juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuinua sekta ya uvuvi na kuhakikisha kuwa wavuvi wanapata nyenzo bora za kazi kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Articles similaires

RAIS SAMIA KUZINDUA DARAJA LA PANGANI NA BOTI ZA UVUVI.

msumbanews.co.tz - 04:16

 Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo anaendelea na ziara yake mkoani Tanga ambapo pamoja na mambo mengine,...

KWENYE URAIS TUMESHAMALIZA-MAJALIWA

msumbanews.co.tz - 16/Feb 06:26

▪️Asisitiza Rais Dkt. Samia tunaye na tunaenda naye.▪️Asema Rais Samia ni mgombea aliyejipambanua kwa uhodari na uimara wake...

MKATABA UJENZI WA MAABARA ZA SAYANSI OUT, WASAINIWA

msumbanews.co.tz - 21/Feb 12:23

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), kimesaini mkataba na kampuni ya kandarasi ya Arm-Strong International Ltd ya jijini Mwanza kuanza ujenzi wa...

UJENZI KITUO CHA KUPOZA UMEME HANDENI KUIMARISHA UPATIKANAJI UMEME- RAIS SAMIA

msumbanews.co.tz - 13:53

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha...

DCEA YATEKETEZA EKARI 336 ZA MASHAMBA YA BANGI NA KUKAMATA KILO 148 ZA MIRUNGI DODOMA

msumbanews.co.tz - 19/Feb 05:48

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, imeteketeza ekari 336 za mashamba ya...

MSIGWA AIPONGEZA WIZARA YA NISHATI USIMAMIZI MRADI WA JNHPP

msumbanews.co.tz - 17/Feb 04:55

 📌 Asema mradi umefikia asilimia 99.8📌 Awaasa watanzania kujivunia mradi wa Julius NyerereKatibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na...

WAZIRI KIKWETE AZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI BIL.1.6 WILAYANI SONGWE

msumbanews.co.tz - 04:56

 Wananchi wamshukuru Rais Samia kwa kutenga fedha za miradiWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi , Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani...

SERIKALI YAJIDHATITI KUBORESHA SEKTA YA KILIMO – DKT BITEKO

msumbanews.co.tz - 14/Feb 09:02

 📌 Anadi soko la mazao jamii ya mikunde India📌 Mnada mazao ya kunde mtandaoni waboresha biashara ya kimataifa📌 Biashara kati ya Tanzania na...

WAZIRI KIKWETE: NI FURAHA YA KILA MZAZI KUONA MWANAE ANASOMA NA KUFANIKIWA, AZINDUA SHULE YA GHOROFA TUNDUMA.

msumbanews.co.tz - 05:28

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe. Ridhiwani Kikwete, amewataka wanafunzi  kusoma kwa bidii ili...

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUTEKELEZA MRADI WA MAKAA YA MAWE MCHUCHUMA NA KATEWAKA

msumbanews.co.tz - 18/Feb 07:46

  ...... Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb.) ameliagiza Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kukamilisha majadiliano na...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément