X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 16/Feb 06:26

KWENYE URAIS TUMESHAMALIZA-MAJALIWA

▪️Asisitiza Rais Dkt. Samia tunaye na tunaenda naye.▪️Asema Rais Samia ni mgombea aliyejipambanua kwa uhodari na uimara wake kiutendaji▪️Amtaja Dkt. Nchimbi kuwa kiongozi mchapakazi na anatosha kwenye nafasi ya ugombea mwenza.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kimeshamaliza mchakato wa kupata mgombea Urais wa Chama hicho katika uchaguzi Mkuu utakaofanya mwaka 2025.Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi (Februari 15, 2025) wakati Mkutano Mkuu Maalum Chama cha Mapinduzi Jimbo la Itilima, uliofanyika katika uwanja wa Stand Mpya ya Itilima, mkoani Simiyu.Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi chama hicho kimewapa ridhaa ya kuendelea kuwatumikia Watanzania katika kipindi cha 2025-2030.“Mama yupo na sisi, tunaye na tunaenda nae, Mwaka huu tumewaleta wagombea bora kabisa ambao wamethibitisha bila shaka kwamba utendaji wao umetukuka katika kipindi walichokuwa wanawatumikia watanzania”.Amesema kuwa katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt. Samia imeshuhudiwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imegusa moja kwa moja maisha ya Watanzania kwenye sekta za elimu, kilimo, afya, maji, miundombinu na uwezeshaji wananchi kiuchumi.“Chama cha Mapinduzi kina Sera imara zinazotekelezeka na watanzania wanakiamini Chama cha Mapinduzi, kinakubalika na ndicho kinachotumainiwa kutokana na uwezo wake wa hali ya juu wa kuwatumikia Watanzania, Mwaka huu tunalojukumu la kuwaambia watanzania nini tumefanya na nini tutafanya katika kuwajibika q ww wa na kusimamia maendeleo ya Watanzania”.Kwa Upande wake, Mbunge wa jimbo la Itilima Silanga Njalu amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoomgozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeipatia Wilaya ya Itilima takribani shilingi bilioni 85 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.Akitolewa mfano kwenye sekta ya Maji Mheshimiwa Njalu amesema kuwa Rais Dkt. Samia aliridhia kutoa kiasi cha shilingi bilioni 11 kwa ajili ya kuanzisha miradi midogo midogo ya maji “Alifanya hivi wakati utekelezaji wa mradi wa maji kutoka ziwa victoria ukiendelea”.Ameongeza kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais Dkt. Samia ilitoa zaidi ya shilingi bilioni 8 kwa ajili ya utoaji wa pembejeo na utaalam kwenye sekta ya kilimo. “Pia tumepokea zaidi ya shilingi bilioni 41 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya umeme”.

Articles similaires

UJENZI KITUO CHA KUPOZA UMEME HANDENI KUIMARISHA UPATIKANAJI UMEME- RAIS SAMIA

msumbanews.co.tz - 13:53

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha...

WAZAZI SHINYANGA MJINI WAPONGEZA UJENZI WA MADARAJA CHIBE - OLD SHINYANGA, IBINZAMATA MAKABURINI

msumbanews.co.tz - 22/Feb 06:19

 Muonekano wa sehemu ya Daraja la Chibe - Old ShinyangaWajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakiwa katika...

RAIS SAMIA AZINDUA JENGO LA HALMASHAURI HANDENI, ATOA WITO KWA WATUMISHI KUTOJIVUNIA VYEO

msumbanews.co.tz - 11:40

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Februari 25, 2025 , amezindua rasmi Jengo la Halmashauri ya...

TUNDUMA WAMETEKELEZA MAAGIZO YA RAIS SAMIA KWA KUTOA BIL 4.6 MIKOPO YA 10%" - WAZIRI KIKWETE

msumbanews.co.tz - 03:41

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema hatua ya Halmashauri ya Tunduma kutoa...

REA YAANZA KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 16,275 MKOANI SIMIYU

msumbanews.co.tz - 19/Feb 05:42

 🎈🎈Mitungi 3,255 yaanza kusambazwa wilayani MaswaMkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Kenani Kihongosi, leo tarehe 18 Februari, 2025 amezindua rasmi...

RAIS SAMIA AIVUSHA WIZARA YA MAJI KUTOKA KUWA YA LAWAMA NA KUWA WIZARA YA MFANO

msumbanews.co.tz - 14:14

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Februari 25, 2025 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji wa miji 28...

BUNGE LAPITISHA NYONGEZA YA BAJETI YA SH. BILIONI 945.7 KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025

msumbanews.co.tz - 14/Feb 14:28

Na. Josephine Majura, WF - Dodoma Bunge limepitisha nyongeza ya mapato na matumizi ya jumla ya shilingi bilioni 945.7 kwa ajili ya kuongeza kwenye...

RAIS SAMIA AKABIDHI BOTI 35 KWA WAVUVI TANGA

msumbanews.co.tz - 09:01

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumatano Februari 26, 2025 amekabidhi boti 35 za kisasa kwa...

BARRICK YACHANGIA SHILINGI TRILIONI 3.6 PATO LA SERIKALI KWA KIPINDI CHA MIAKA 4

msumbanews.co.tz - 14/Feb 08:44

Meneja wa Barrick nchini, Dk.Melkiory Ngido akitoa taarifa ya utendaji wa Barrick na Twiga kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na...

ULEGA ATAKA WATAALAMU WAKUNE VICHWA KUONDOA KERO YA FOLENI MIJINI

msumbanews.co.tz - 13/Feb 18:11

 WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewataka wataalamu wa wizara hiyo kutumia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika mkoani Singida kubuni njia...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément