X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 07/Sep 07:31

WAZIRI RIDHIWANI AIPONGEZA LESCO

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amepongeza LESCO kwa kuendelea kusimamia haki na uwajibikaji wa masuala ya kazi, uchumi na kijamii.“Nitumie fursa hii kuwapongeza kwa moyo wa dhati kwa kutekeleza vema majukumu yenu kwa ufanisi ili kuhakikisha malengo ya kuanzishwa LESCO yanatimia” amesema. Mhe. Ridhiwani ametoa pongezi hizo leo Septemba 4, 2024 Jijini Dodoma alipokutana na Wajumbe wa Baraza la  Ushauri wa Masuala ya Kazi, Uchumi na Kijamii (LESCO) kwa lengo la kufahamiana na kuagana nao wajumbe wa baraza hilo ambalo uongozi wake umefikia ukomo.Aidha, amesema katika kipindi cha miaka 3, LESCO imefanya kazi nzuri ya kuishauri serikali kuhusu sera zinazohusu masuala ya Ajira na Kazi; upangaji wa kima cha chini cha mshahara katika sekta binafsi; Uridhiaji wa mikataba ya Shirika la Kazi Duniani; na ushirikishwaji wa wadau wa Utatu (Serikali, Waajiri na Wafanyakazi) katika masuala  ya  kazi, Uchumi na jamii.Vile vile, Mhe. Ridhiwani ametoa rai kwa wajumbe wa baraza hilo kuendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri ili kuhakikisha sekta ya kazi na ajira inazingatia misingi ya kazi zenye staha kwa maslahi ya wafanyakazi na waajiri.Awali akizungumza Mwenyekiti wa LESCO Dkt. Samwel Nyantahe ameishukuru Serikali kwa kutoa ushirikiano katikia kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yao.

Articles similaires

CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WA UMMA ZITATULIWE ILI KUKUZA SEKTA YA UMMA KIUCHUMI NA KIJAMII

msumbanews.co.tz - 05/Nov 09:20

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa neno la utangulizi kabla ya...

SERIKALI ITAENDELEA KUWATUMIA WATAFITI NCHINI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 16:47

 Na : Jusline Marco : ArushaWaziri wa nchi,ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawane amesema serikali ya...

UTPC YAIOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI MASLAHI YA WATUMISHI VYOMBO VYA HABARI.

msumbanews.co.tz - 02/Nov 15:20

 Chama cha Wafanyakazi katika vyombo vya habari nchini(JOWUTA) kimetaka serikali kusimamia sheria za kazi kwa wafanyakazi katika vyombo vya habari...

WAJASIRIAMALI WA NCHI WANACHAMA EAC WAHAMASISHWA KUWA WABUNIFU

msumbanews.co.tz - 05/Nov 18:44

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulrmavu, Zuhura Yunus akizungumza wakati hafla ya Siku ya Tanzania iliyofanyika...

MIRADI YA TACTIC KUIMARISHA MAZINGIRA YA UFANYAJI WA BIASHARA NCHINI- MHE. KATIMBA.

msumbanews.co.tz - 02/Nov 16:02

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema kukamilika kwa Miradi ya TACTIC mkoani...

UJENZI WA SOKO LA MWANGA NA KATONGA UTAIMARISHA MAZINGIRA YA BIASHARA KIGOMA- MHE. KATIMBA.

msumbanews.co.tz - 02/Nov 16:10

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema ujenzi wa Soko la Kisasa la Mwanga na Soko la...

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WAELEKEZWA KUFANYA MSAWAZO WA WALIMU

msumbanews.co.tz - 07/Nov 09:37

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amewaelekeza wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafanya msawazo wa...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA ILI KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO YA WANANCHI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:02

 Na. Joseph Mahumi, WF, MorogoroSerikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo...

CHANDE ASHAURI MABENKI KUTANUA WIGO WA MASOKO NJE YA NCHI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:25

 Na. Peter Haule na Josephine Majura, WF, Dodoma Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), ameitaka Akiba Commercial Bank Plc (ACB)...

SERIKALI YAFIKIA ASILIMIA 85 KATIKA UPATIKANAJI WA DAWA

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:32

 Na : Jusline Marco;ArushaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu upatikanaji wa...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément