Serikali imeongeza mkazo katika masomo ya Sayansi ikiwa ni pamoja na kujenga shule 26 za wasichana zinazotoa masomo ya Sayansi.Hayo yamesemwa na...
Vous n'êtes pas connecté
Waziri wa Ujenzi,Innocent Bashungwa amewataka Wahandisi kuwajibika katika majukumu pale wanapopatiwa mradi ili kulinda thamani yao. Akizungumza katika Jukwaa la Wahandisi katika ukumbi wa Mlimani City Waziri Bashungwa amesema Wahandisi ni muhimu katika maendeleo kushindwa kuwajibika katika majukumu yao wanarudisha jitihada zinazofanywa na serikali.Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa fursa ya ujenzi wa miradi ambapo wazawa wamepewa kipaumbele.Waziri Bashungwa alikemea kwa tabia ya baadhi ya Wahandisi ambao, mara baada ya kusaini mikataba na kupokea malipo ya awali hukwepa majukumu yao. “Kuna wimbi la Wahandisi ambao baada ya kupata (Advance Payment) , wanaanza kusumbua na kushindwa kutimiza ahadi zao,”amesema Bashungwa.Bashungwa ameitaka bodi ya Usajili Wahandisi (ERB) na Bodi ya Usajili wa Makandarasi ,,(CRB) lazima zisimamie kwa makini tabia na utendaji wake kwa watu hao ili kuepusha ubabaishaji unaoleta hasara kubwa kwa taifa.Katibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhandisi Zena Said amewataka wahandisi wenzake kutendea haki viapo vyao vya taaluma.“Wahandisi lazima wawe waadilifu, wafuate uzalendo na kufanya kazi kwa umakini ili kuleta maendeleo ya kweli,”Amesema kuwa dhamira yake ya kuona wahandisi wanakuwa sehemu ya suluhisho na si tatizo ambapo watakuwa wameisaidia Serikali na maendeleo yakapatikana kutokana na mchango wao.Msajili wa Bodi ya Usajili Wahandisi Tanzania (ERB), Mhandisi Bernard Kavishe, amesema mipango ya bodi ni kuimarisha sekta Wahandisi nchini. “Tumeendelea na mpango wetu wa STEM wa kuhamasisha wanafunzi wa Shule za Sekondari kusoma masomo ya sayansi ili kuongeza nguvu kazi.Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu ya kuvutia, “Kuweka Nguvu Kazi ya Uhandisi kwa Enzi ya Akili Mnemba ya ya umuhimu wa kutumia akili, maarifa, na teknolojia ili kufanikisha miradi yenye ufanisi na uboraWaziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa akizungumza katika mkutano wa mwaka wa Wahandisi uliofanyika jijini Dar es Salaam.Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Mhandisi Bernard Kavishe mkutano wa mwaka wa Wahandisi, jijini Dar es Salaam.Baadhi ya matukio katika picha katika mkutano wa mwaka kwa Wahandisi, jijini Dar es Salaam.
Serikali imeongeza mkazo katika masomo ya Sayansi ikiwa ni pamoja na kujenga shule 26 za wasichana zinazotoa masomo ya Sayansi.Hayo yamesemwa na...
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama wakitembelea na kukagua Ghala la Mpako...
Tanzania ina mifumo kadhaa ya kisheria na udhibiti inayoongoza sekta ya mawasiliano na TEHAMA ili kuhakikisha huduma ya intaneti ya kasi inawafikia...
Waziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa ,Kitila Mkumbo akizngumza wakati akifungua Wiki ya AZAKI iliyoanza rasmi leo Septemba 9-13, 2024 Jijini...
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), amewataka viongozi wa Mfuko wa Mawasiliano...
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amepongeza LESCO kwa kuendelea kusimamia haki na...
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Abdul Mhinte akizungumza jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mkutano wa wataalamu kutoka...
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezitaka Mamlaka za Udhibiti na Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki kuzingatia weledi,...
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...