X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 10/Sep 04:38

PROF. MKUMBO; SERIKALI HAITAKUWA KIKWAZO KWA AZAKI

 Waziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa ,Kitila Mkumbo akizngumza wakati akifungua Wiki ya AZAKI iliyoanza rasmi leo Septemba 9-13, 2024 Jijini Arusha. Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation For Civil Society FCS - Justice Rutenge, akizunguza lipokuwa akitoa hotuba yake ya utanguliza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya AZAKI , Jijini Arusha. Mkurugenzi Mkazi wa Trademark Africa Elibariki Shammy, akizungumza katika mkutano huo.Waziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa, Kitila Mkumbo amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Asasi za Kiraia nchini nakwamba haitakuwa kikwazo kwao katika shughuli zake za kuleta maendeleo, sanjari na kutoa mawazo yatakayojenga zaidi ili kutafuta fursa zilizopo ndani na nje ya nchi.Profesa Mkumbo amesema hayo wakati akifungua Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) iliyoanza rasmi leo Septemba 9, 2024 jijini Arusha.Profesa Mkumbo amsema ni vema sasa Asasi za Kiraia zikashirikiana na serikali katika kutoa maoni yao ikiwemo kukaa meza moja kutaua changamoto zinazoibuka sanjari na kutafuta fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi katika kukuza uchumiProf. Mkumbo amesema, lengo kuu la serikali ni kuhakikisha ustawi wa watu wote unakuwa, na ili kufika huko ni vema zaidi kujifunza kupitia kwa watu, kuwa wabunifu na kutoa maoni katika kuhakikisha Dira ya Mendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 inaleta tija zaidi hususan katika uwekezaji kwenye elimu, miundombinu ikiwemo umeme wa uhakika.‘’AZAKI zihakikishe zinaisemea jamii changamoto ambazo wanaziona na kutatuliwa ili kuisaidia serikali kuzishughulikia na si kuilalamikia kuwa haifanyi kazi ilihali hawajazibainisha ili zifanyiwe kazi na jamii iweze kupata mabadiliko’’. Amesema Mkumbo.Amesema nchi zilizoendelea zimepiga hatua katika maendeleo kwa sababu ya umeme hivyo uwepo wa Bwawa la mwalimu Nyerere nchini Tanzania hadi kukamilika kwake utawezesha umeme kupatikana kwa wingi ikiwemo uchumi kukua kupitia viwanda vinavyozalisha bidhaa ndani ya nchi na kuuza bidhaa hizo nje ya nchi kwakushirikiana na sekta binafsi hususan za kilimo .Naye rais wa Foundation For Civil Society (FCS), Dk Stigmata Tenga amesisita kuwa lazima mabadiliko ya watanzania yatokee kupitia AZAKI ambazo ndio husemea wananchi wenye changamoto mbalimbali katika sekta za afya ,elimu, miundombinu ya barabara ikiwemo utoaji wa fursa za fedha kupitia taasisi mbalimbali zinazowawezesha wananchi kujikwamua kimaisha kupitia mikopo yenye riba nafuu na kuongeza kuwa rasilimali watu ni muhimu kuzingatiwa katika kuwaletea wananchi maendeleo.Wakati huo huo, Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark Africa Elibariki Shammy amesema mkakati wa serikali ni kuhakikisha biashara za kidigitali zinakua zaidi kwa kushirikisha vijana kwa kasi kubwa kupitia biashara kwa kuwawekea mazingira rafiki yatakayowasaidia kujikwamua kiuchumi kupitia fursa mbalimbali zilizopo nchini.Awali Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Isabelle Mignucci ameshukuru ushikiano kati ya serikali ya Tanzania na mashirika mbalimbali unaoleta tija katika maendeleo sanjari na kuhakikisha vijana wanapata fursa za maendeleo kupitia teknolojia na ubunifu unaoleta tija zaidi katika ukuaji wa uchumi.Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Isabelle Mignucc akizunguza alipokuwa akitoa hotuba yake katika maadhimisho hayo Jijini Arusha.  

Articles similaires

WIKI YA AZAKI KUHAMASISHA JAMII KUSHIRIKI DIRA 2050, UCHAGUZI

msumbanews.co.tz - 09/Sep 07:02

 Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society FCS- Justice Rutenge, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jijini...

DKT. BITEKO AAGIZA KIGOMA KUINGIZWA KWENYE GRIDI KABLA YA 2025

msumbanews.co.tz - 16:02

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha linatekeleza kwa kasi...

DKT. BITEKO ASISITIZA MAADILI, WELEDI NA UWAJIBIKAJI KATIKA UNUNUZI WA UMMA

msumbanews.co.tz - 09/Sep 13:54

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezitaka Mamlaka za Udhibiti na Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki kuzingatia weledi,...

SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KUHUSU SUALA LA UHABA WA FEDHA ZA KIGENI

msumbanews.co.tz - 07/Sep 07:35

 Na. Joseph Mahumi na Peter Haule, WF, DodomaSerikali imesema inaendelea kuweka mikakati na mbinu mbalimbali za muda mfupi, wa kati na mrefu katika...

WAZIRI MAVUNDE AYATAKA MAKAMPUNI YA MAKAA YA MAWE KUWEKEZA KATIKA UZALISHAJI WA UMEME

msumbanews.co.tz - 17/Sep 05:17

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde amezipongeza Kampuni za uzalishaji wa makaa ya mawe kwa kuongeza uzalishaji na kuzitaka kuelekeza zaidi...

BoT, AZAKI WAJADILI KUBORESHA HUDUMA JUMUISHI ZA FEDHA KWA JAMII

msumbanews.co.tz - 08:23

 Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema itaendelea kufanya jitihada mbalimbali za kusaidia ukuaji wa huduma za malipo kidigitali kwa kuweka miundombinu...

Naibu waziri Mkuu Amewataka Maafisa manunuzi na ugavi nchini kufanya kazi Kwa uadilifu ,uwajibikaji na uwazi

msumbanews.co.tz - 10/Sep 18:08

NAIBU waziri mkuu Dk Dotto Biteko amewataka maafisa manunuzi na ugavi nchini kufanya kazi zao Kwa uadilifu ,uwajibikaji uwazi na maadili katika...

WANAWAKE LONGIDO WAJENGEWA UWEZO KUTAMBUA HAKI ZAO

msumbanews.co.tz - 12/Sep 06:22

 Wanawake kutoka jamii ya kimaasai katika Tarafa ya Longido wilaya ya Longido mkoa wa Arusha wameonyesha furaha yao baada ya shirika la Legal...

WMA YAHIMIZA USHIRIKIANO KUTOKA SEKTA BINAFSI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 08:08

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...

WMA YAHIMIZA USHIRIKIANO KUTOKA SEKTA BINAFSI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 08:08

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément