X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 08/Nov 11:56

SERIKALI KUHAKIKI WASTAAFU KIDIJITALI

Na: Farida Ramadhan na Josephine Majura WF, DodomaSerikali inatengeneza mfumo wa kidigitali utakaowawezesha Wastaafu kujihakiki wenyewe (Self verification) kupitia simu zao za mkononi au kwa kutumia huduma za kibenki ili kuwapunguzia Wastaafu gharama na usumbufu wa kusafiri umbali mrefu kwenda kuhakikiwa. Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nachingwea, Mhe. Amandus Julius Chinguile, aliyehoji kwa nini Serikali isiweke utaratibu wa Wastaafu kuhakikiwa kwenye Halmashauri au Kata badala ya utaratibu wa sasa wa kuhakikiwa Mikoani.Mhe. Chande alisema uhakiki wa wastaafu wanaolipwa na Hazina umekuwa ukifanyika katika ngazi ya Halmashauri, hata hivyo, ili kuwapunguzia Wastaafu gharama na usumbufu wa kusafiri umbali mrefu kwenda kuhakikiwa, Serikali inatengeneza mfumo wa kidigitali utakaowawezesha Wastaafu kujihakiki wenyewe.Alisema baada ya kukamilika kwa taratibu zote, Wastaafu watapewa elimu ya jinsi ya kujihakiki wenyewe na watatangaziwa siku ya kuanza kujihakiki.Katika hatua nyengine, Mhe. Chande aliliambia Bunge kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kuimarisha uchumi wa maeneo yote ya nchi ili kuweka mazingira yatakayovutia benki na taasisi za fedha kuanzisha huduma za kibenki katika maeneo mbalimbali nchini.Alitoa maelezo hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Wingwi, Mhe. Omar Issa Kombo, aliyetaka kujua wakati ambao Serikali itajenga Benki za NMB na CRDB kwenye Makao Makuu ya Wilaya ya Micheweni.Mhe. Chande alisema kuwa uamuzi wa kufungua matawi ya benki hufanywa na benki yenyewe ambapo kabla ya kufanya uamuzi huo, benki hufanya upembuzi yakinifu ukiwa na lengo la kuangalia kama kuna uwepo wa biashara ya kutosha ambayo italetea faida.“Mabenki yakishafanya upembuzi yakinifu katika sehemu husika huwasilisha uamuzi/pendekezo lao Benki Kuu ya Tanzania”, alisema Mhe. Chande.Aliongeza kuwa Serikali kupitia Benki Kuu haina kizuizi chochote katika suala la mabenki kufungua matawi, kama benki husika itatimiza masharti yote ya kufungua matawi kama yalivyoainishwa katika kanuni namba 31 ya Kanuni za Utoaji Leseni za Mabenki na Taasisi za Fedha za Mwaka 2014.Mhe. Chande alibainisha kuwa Benki za NMB na CRDB hazina matawi kwenye Makao Makuu ya Wilaya ya Micheweni lakini , wananchi wa Wilaya ya Micheweni wanapata huduma za kibenki kutoka benki za CRDB na NMB kupitia mawakala wa benki, ambapo hadi kufikia Oktoba 2024, kulikuwa na jumla ya mawakala 4 wa Benki ya CRDB na 14 wa Benki ya NMB wanaotoa huduma za kibenki katika Wilaya hiyo.

Articles similaires

CHANDE ASHAURI MABENKI KUTANUA WIGO WA MASOKO NJE YA NCHI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:25

 Na. Peter Haule na Josephine Majura, WF, Dodoma Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), ameitaka Akiba Commercial Bank Plc (ACB)...

Jakaya Kikwete aipongeza NMB kwa Bil. 1 za Matibabu ya Watoto JKCI

msumbanews.co.tz - 04/Nov 08:09

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete, amekiri kuvutiwa na mchango mkubwa wa Benki ya NMB wa Sh. Bilioni 1 kati ya Sh. Bil....

UJENZI WA BARABARA NA MADARAJA BABATI KUFUNGUA UTALII

msumbanews.co.tz - 12/Nov 12:59

 Na. Catherine Sungura, BabatiImeelezwa kwamba ujenzi na matengenezo ya barabara na madaraja unaofanywa na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA ILI KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO YA WANANCHI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:02

 Na. Joseph Mahumi, WF, MorogoroSerikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo...

UINGEREZA KUSAIDIA TANZANIA SEKTA YA AFYA

msumbanews.co.tz - 12/Nov 15:13

 Na. Joseph Mahumi, WF, Dar es Salaam.Tanzania na Uingereza zimesaini hati za Makubaliano ya nyongeza ya kuchangia Mfuko wa Kusaidia Sekta ya Afya...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBU YA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA.

msumbanews.co.tz - 04/Nov 11:16

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali imeendelea kuboresha miundombu ya kutolea...

SERIKALI INAENDELEA KUTEKELEZA MRADI WA KUPELEKA UMEME WA GRIDI MTWARA NA LINDI- MHE.KAPINGA

msumbanews.co.tz - 04/Nov 10:54

 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali inatekeleza mradi wa kuiunganisha Mikoa ya Mtwara na Lindi na  umeme wa gridi kutokea...

ZAIDI YA WANANCHI 32,000 WA VIJIJI VYA WILAYA ZA MOROGORO NA MVOMERO KUANZA KUPATA MAWASILIANO

msumbanews.co.tz - 04/Nov 18:47

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi MaryPrisca Mahundi (Mb), amesema Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia...

Wagonjwa wa moyo kutoka Malawi kutibiwa JKCI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:38

 Serikali ya Jamhuri ya Malawi imeahidi kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ili wagonjwa wa moyo waliopo nchini humo hasa watoto...

REA KUPELEKA UMEME VISIWA VYOTE TANZANIA BARA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:27

 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément