X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 13/Nov 13:07

TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA AFYA

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama leo Novemba 13, 2024 amekutana na Mwakilishi mkazi wa Shirika la Afya Duniani (World Health Organization- WHO) Dkt. Charles Sagoe-Moses kwa mara ya kwanza kwa lengo la  kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Afya.Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es Salaam Waziri Mhagama ameishukuru WHO kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika kukabiliana na changamoto za magonjwa ikiwemo magonjwa ya milipuko. "Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, nachukua fursa hii kuwashukuru Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa msaada na ahadi zenu mlizozitoa katika kusaidia na kuboresha huduma za afya nchini," amesema  Waziri MhagamaShirika la Afya Duniani pamoja na Tanzania zimekuwa zikishirikiana kwa miongo kadhaa katika kuboresha Sekta ya afya katika maeneo ya ushirikiano wa kiufundi, mijadala ya kisera, ushauri pamoja na kubadilishana maarifa kwa wataalamu wa afya. Pamoja na mambo mengine Waziri Mhagama ameomba ushirikiano katika suala la Bima ya Afya kwakuwa Sekta ya Afya imefikia hatua muhimu ya kuanza kwa utekelezwaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa Wote ikiwa ni njia ya kusaidiana ili  watu wa hali ya kipato cha chini wapate matibabu bila kikwazo cha fedha."Tunashukuru kwa ushirikiano wa pamoja na Shirika la Afya Duniani lakini pia tunaomba ofisi yako iendelee kuunga mkono na kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za afya na kuhakikisha utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote unafanikiwa," amesema Waziri MhagamaAidha, Waziri Mhagama amelihakikishia Shirika hilo kuwa Serikali chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Shirika la Afya Duniani (WHO) katika kutimiza azma ya kuboresha huduma za afya nchini.Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Charles Sagoe-Moses wakati akijitambulisha kwa Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ameahidi kuwa Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Tanzania hasa katika kuhakikisha afya za Watanzania zinaimarika na kuwalinda na magonjwa hasa ya mlipuko kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo ya kuwezesha utolewaji wa elimu.

Articles similaires

SERIKALI YAFIKIA ASILIMIA 85 KATIKA UPATIKANAJI WA DAWA

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:32

 Na : Jusline Marco;ArushaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu upatikanaji wa...

UINGEREZA KUSAIDIA TANZANIA SEKTA YA AFYA

msumbanews.co.tz - 12/Nov 15:13

 Na. Joseph Mahumi, WF, Dar es Salaam.Tanzania na Uingereza zimesaini hati za Makubaliano ya nyongeza ya kuchangia Mfuko wa Kusaidia Sekta ya Afya...

TANZANIA KUUNGANA NA DUNIA USALAMA WA AFYA KIMATAIFA

msumbanews.co.tz - 13/Nov 14:27

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mwaka 2015, Tanzania iliunga mkono Ajenda ya Mpango wa Kimataifa wa Usalama...

JKCI, MOI NA MNH zaitwa Comoro kwenda kutoa huduma za matibabu ya kibingwa

msumbanews.co.tz - 05/Nov 10:24

Na Mwandishi Maalumu – Dar es Salaam 04/11/2024 Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Watu wa Comoro Mhe. Yousoufa Mohamed Ali ameziomba Taasisi ya...

TATHIMINI YA USIMAMIZI WA HUDUMA ZA AFYA MSINGI KUFANYIKA KILA BAADA YA WIKI MBILI - Dkt. Magembe

msumbanews.co.tz - 11/Nov 13:31

 Na. James Mwanamyoto, OR-TAMISEMINaibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Grace Magembe amewaelekeza watumishi wa Idara ya Afya, Ustawi...

TATHIMINI YA USIMAMIZI WA HUDUMA ZA AFYA MSINGI KUFANYIKA KILA BAADA YA WIKI MBILI - Dkt. Magembe

msumbanews.co.tz - 11/Nov 13:31

 Na. James Mwanamyoto, OR-TAMISEMINaibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Grace Magembe amewaelekeza watumishi wa Idara ya Afya, Ustawi...

BASHUNGWA AONGOZA HARAMBEE JIMBO KATOLIKI BUNDA, MILIONI 272.6 ZAKUSANYWA

msumbanews.co.tz - 12/Nov 07:33

 Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameshiriki Misa Takatifu katika Parokia ya Mtakatifu Paulo na kuongoza harambee ya kumalizia ujenzi wa jengo la...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBU YA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA.

msumbanews.co.tz - 04/Nov 11:16

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali imeendelea kuboresha miundombu ya kutolea...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA ILI KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO YA WANANCHI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:02

 Na. Joseph Mahumi, WF, MorogoroSerikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo...

CHANDE ASHAURI MABENKI KUTANUA WIGO WA MASOKO NJE YA NCHI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:25

 Na. Peter Haule na Josephine Majura, WF, Dodoma Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), ameitaka Akiba Commercial Bank Plc (ACB)...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément