X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 14/Feb 08:16

TCAA YAFANYA MAFUNZO KWA WABUNGE

 Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imefanya mafunzo kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali(PAC) na Sheria Ndogo juu ya uendeshaji wa  Mamlaka  katika majukumu yake ya Ki udhibiti na Uongozaji ndege.Pia utekelezaji wa miradi mbalimbali  yenye lengo la kuendelea  kuliweka anga la Tanzania salama. Semina hiyo imefanyika Februari 13, 2025  Bungeni Jijini DodomaLengo la semina hiyo  ni kuwajengea uelewa wa pamoja waheshimiwa wabunge kuhusu Mamlaka na namna inavyotekeleza viwango vya kimataifa kwa mujibu wa taratibu za Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO).Katika semina hiyo Kamati hizo ziliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Hesabu za Serikali(PAC) Mhe Japhet Hasunga kwa niaba ya  wenyekiti wa Kamati zote mbili ambapo  Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile   na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania (TCAA) Bw.Salim Msangi akiambatana  na wataalamu wake  walitoa ufafanuzi kuhusu mambo mbalimbali kufuatilia maswali ya waheshimiwa wabunge.Mhe. Hasunga amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada anazofanya kwa  kutenga fedha zaidi za kutekeleza miradi ya mamlaka ikiwemo Ujenzi wa Chuo cha kisasa cha  Usafiri wa Anga  Tanzania (CATC,) mradi ambao hadi kukamilika kwake utagharimu shilingi bil 78. Pia  amempongeza Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David kihenzile aliyekuwepo kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa kwa kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kupatikana kwa fedha za kutekeleza miradi hiyo.“Leo tumepata mafunzo ya muhimu sana hasa namna Mamlaka inavyosimamia shughuli mbalimbali zinazokuwa zikiendelea kwa watoa huduma mbalimbali, sisi kama Kamati za Bunge tunasimamia na kuangalia namna taasisi zetu za umma zinavyotekelea majukumu yake tumejifunza  namna marubani wanavyorusha ndege, mawasiliano baina ya muongozo ndege na rubani yanavyofanyika kwa usalama na tumeridhika" amesema Mje. HasungaAidha, akifunga mafunzo hayo Mhe. Hasunga ameiomba Serikali kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi ya Mamalaka inayoendelea ili kuzidi kuboresha usalama wa anga letu na kuendelea kuvutia jumuiya za kimataifaKwa upande wake Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile amewashukuru wabunge wa kamati zote mbili kwa kutenga mda wao na kupata mafunzo kupitia semina hiyo licha ya kuwa na ratiba ngumu za shughuli za Bunge zinazoendelea na kuahidi Wizara na taasisi zake zitaendelea kushirikiana na kamati zote.Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa anga  Tanzania Salim Msangi alitoa taarifa za miradi, mikakati na shughuli mbalimbali za  maendeleo zinazotekelezwa na Mamlaka ambazo zinachangia anga la Tanzania kuwa salama kitaifa na kimataifa.

Articles similaires

TCAA YAWAPA WABUNGE MAFUNZO JUU YA UDHIBITI NA USALAMA WA ANGA

msumbanews.co.tz - 13/Feb 15:31

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imefanya mafunzo kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za...

BARRICK NI KIELELEZO BORA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI NCHINI- DKT. KIRUSWA

msumbanews.co.tz - 16/Feb 06:20

 • Kamati ya Bunge Yataka Kampuni Zingine Kuiga Barrick📍 KahamaNaibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, amesema kuwa Kampuni ya Uchimbaji wa...

DKT. BITEKO ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA

msumbanews.co.tz - 16/Feb 06:21

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Bitekoakizungumza na Watanzania waishio India pamoja na watumishi wa Ubaloziwa Tanzania...

SERIKALI INATAMBUA MASAA YA WABUNGE WENYE CPA KWENYE KAMATI YA PAC, LAAC, PIC NA BAJETI

msumbanews.co.tz - 14/Feb 12:48

 Na. Josephine Majura WF- Dodoma Serikali imeeleza kuwa masaa yanayotumiwa na Wabunge wenye sifa ya Mhasibu wa Umma aliyeidhinishwa (CPA), katika...

ULEGA ATAKA WATAALAMU WAKUNE VICHWA KUONDOA KERO YA FOLENI MIJINI

msumbanews.co.tz - 13/Feb 18:11

 WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewataka wataalamu wa wizara hiyo kutumia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika mkoani Singida kubuni njia...

MAKAMU WA RAIS ATOA WITO KWA WAANDAAJI WA VIPINDI VYA ELIMU KWA UMMA KUHAMASISHA UHIFADHI WA MAZINGIRA NA MATUMIZI YA NISHATI SAFI

msumbanews.co.tz - 21/Feb 19:32

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi iliyotolewa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)...

CHAMWINO YAPONGEZWE KWA USIMAMIZI WA THAMANI YA FEDHA.

msumbanews.co.tz - 16/Feb 08:38

 Kamati ya kudumu ya Bunge ya TAMISEMI imeipongeza Halmashauri ya Chamwino Kwa kuonyesha na kusimamia thamani ya fedha katika ujenzi  wa miradi...

TAMISEMI YAWEKA WAZI VIWANGO VIPYA UJENZI WA MADARASA NA ZAHANATI

msumbanews.co.tz - 14/Feb 04:24

 OR-TAMISEMIOfisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imefanya mapitio ya bajeti kwa kuzingatia muundo wa kanda na gharama za...

KAMATI YA BUNGE YAMPONGEZA WAZIRI RIDHIWANI KIKWETE KWA USIMAMIZI WA MIRADI YA NSSF ARUSHA

msumbanews.co.tz - 18/Feb 06:56

 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imempongeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe....

Les derniers communiqués

  • Aucun élément